Maneno ya Lowassa kwa Rais Magufuli katika Mkutano Mkuu CCM 2020

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
Mwenyekiti nakushukuru sana kunipa heshima hii sikuitengemea nilikuwa najua Mawaziri Wakuu Wastaafu wapo wataongea kwa niaba yangu nashukuru sana.

Hakuna ubishi kwamba toka umechukua nchi; nchi inakwenda vizuri sana! Hakuna ubishi, yako mambo waliyokuwa wanasema hayawezekani sasa yanawezekana chini ya uongozi wako. Hakuna ubishi. Nchi imetulia na inakwenda kwa speed sana! Tunakuomba uendelee kufinya! Speed isipungue!; Iendelee vile vile kama ilivyoanza” - Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa

Mkutano Mkuu CCM 2020
Dodoma

TANZANIA INAZIDI KUFANIKIWA katika vita ya kiuchumi na KAZI INAENDELEA kujenga uchumi imara kwa Taifa*
#ccm2020

IMG-20200711-WA0284.jpg
 
Maskini Edo, imebidi tu aingie keenye team ya praise and worship maana mkwe wake anaozea jela na tangu ameunga mkono juhudi ahadi ya mkwe kuachiwa haijatimizwa
Mwenyekiti nakushukuru sana kunipa heshima hii sikuitengemea nilikuwa najua Mawaziri Wakuu Wastaafu wapo wataongea kwa niaba yangu nashukuru sana.

Hakuna ubishi kwamba toka umechukua nchi; nchi inakwenda vizuri sana! Hakuna ubishi, yako mambo waliyokuwa wanasema hayawezekani sasa yanawezekana chini ya uongozi wako. Hakuna ubishi. Nchi imetulia na inakwenda kwa speed sana! Tunakuomba uendelee kufinya! Speed isipungue!; Iendelee vile vile kama ilivyoanza” - Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa

Mkutano Mkuu CCM 2020
Dodoma

TANZANIA INAZIDI KUFANIKIWA katika vita ya kiuchumi na KAZI INAENDELEA kujenga uchumi imara kwa Taifa*
#ccm2020

View attachment 1503652
 
Lowasa anastahili sana heshima, ametoka Kimya kimya na ametulia bila kumtukana yeyote.
 
Mimi tangu aliposema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka namuunga mkono.

Aliona mbali
 
''Baba wa watu ni mpole na mstaarabu, hajawahi kunitukana kwenye kampeni zake''

Sitaki shobo
 
CDM walindandia treni ya mwendo kasi kwa mbele. Hawa wazee kamwe hawaachi uccm wao
Mkongwe mwenzangu hata wewe unadanganyika? Hapa hakuna u-CCM hata kidogo bali kuna ''uzoea vya bure''. Hawa hawaongozwi na itikada au falsafa. Wanaongozwa na matumbo yao na mazoea yao ya kukaa viti vya mbele kama mafarisayo. Popote wanapoona hizo fursa zipo watakimbilia huku wakiimba mapambio. Leo hii CCM ikitoka madarakani watahama na kuhamia penye fursa. Lowassa kilimchotoa CCM ni kutaka madaraka. Sasa hivi ameoana afya yake haimruhusu kufanya pilika pilika ndiyo akaaamua kurudisha majeshi. Ila watu wa aina hii bado wanahitajika. Tusichoke kuwapokea wakija upande wetu. Watu wa aina hii japo wanaongozwa na tumbo ila hapo hapo wanafaida zake japo hazionekani waziwazi.
 
Back
Top Bottom