Maneno ya Kiswahili Yaliyopotea

Bazazi,

Mkuu yapo pia maneno yaliyobadilishwa maana kabisa ambapo leo ukiyaongea mbele za watu utaonekana ni chizi, mfano neno, "Tongoza" na neno "uroda",

Tongoza ni kumbembeleza mtu hadi akubali shida yako. Na uroda ni ile hali ya raha anayopata mtu anapokuwa katika chombo cha usafiri kama gari, mnyama, ndege, meli au bembea nk.

Neno lililopotea hadhirani ninalokumbuka ni:-

Kikwasa-----pini.
 
Pishi... Kipimo cha ujazo
Kibaba... Kipimo cha ujazo

Mfano...
Niuzie mchele pishi moja na vibaba viwili
 
Skuna halikuwa neno kamili la kiswahili. Schooner ni glasi ya kuwekea vinywaji (hasa bia) ambayo ni pana kwa juu halafu kueleka kwenye kitako inakuwa nyembamba. Neno skuna lilikuwa linatumiwa katika kiswahili kwa viatu ambavyo visigino vyake vilikuwa na maumbo yanayofanana na glasi hizo

1565738813942.png
1565738852560.png
 
Neno ambalo najua limesahaulika kabisa na huenda hakuna hata anayelijua hapa JF ni "tinabuu." Kama kuna anayejua lilikuwa na maana gani aseme.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom