Maneno ya kishujaa ya Garatwa, Diwani wa CHADEMA wa Kata ya Nyansurura, Serengeti

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
NIMEMALIZA SALAMA NIKIWA CHADEMA

Leo tarehe 10 June, 2020 nimehitimisha rasmi wajibu wangu kama Diwani wa Kata ya Nyansurura ndani ya Halmashauri yetu ya Wilaya ya Serengeti.

Nimeutimiza wajibu huu nikiwa CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA na nimeomba tena ridhaa ya Chama chetu kuwa Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CHADEMA.

Nawashukuru sana Wananchi na Viongozi wenzangu wote wa Chama na Serikali tulioshirikiana pamoja wakati wote ambao nilikuwa Mwakilishi wa Wananchi wa Kata yetu.

Naishukuru sana familia yangu hasa Mke wangu Mpendwa Magdalena Wilbert na Watoto wetu Emanuel, Ibrahim na Mussa kwa Ushirikiano wa karibu walionipa ikiwemo kunitia Moyo.

Furaha yangu kubwa ni kuona nimehitimisha Kipindi hiki cha Miaka mitano nikiwa CHADEMA na nitaendelea kuwa CHADEMA hata nikiukosa Uwakilishi.

Garatwa,
Diwani & M/Kiti CHADEMA Serengeti.
10 June, 2020.

Hakika haya ni maneno ya kishujaa sana kutoka kwa huyu diwani pamoja na majaribu yoote ya kununuliwa lkn alipambana na kutimiza ndoto yake ya kuwahudumia walio mchagua.

Hongera Mh. Diwani

FB_IMG_1591795273213.jpeg
 
Hakika jamaa kapigana kishujaa kawazidi hata wale walio aminiwa na kupewa ubunge.

Wamekubali kununuliwa kwa vipande 30
Hongera sana Mheshimiwa Diwani,umepigana vita hadi mwisho haukuingiwa na tamaa ya fedha au vishawishi vya kijinga hakika Tanzania inakosa wanasiasa wengi wenye msimamo kama wako.
 
Chombo inazama mkuu, lakini kama Mwenyekiti Serengeti hakikisha huu mtikisiko hauathiri maeneo yako
 
NIMEMALIZA SALAMA NIKIWA CHADEMA

Leo tarehe 10 June, 2020 nimehitimisha rasmi wajibu wangu kama Diwani wa Kata ya Nyansurura ndani ya Halmashauri yetu ya Wilaya ya Serengeti.

Nimeutimiza wajibu huu nikiwa CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA na nimeomba tena ridhaa ya Chama chetu kuwa Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CHADEMA.

Nawashukuru sana Wananchi na Viongozi wenzangu wote wa Chama na Serikali tulioshirikiana pamoja wakati wote ambao nilikuwa Mwakilishi wa Wananchi wa Kata yetu.

Naishukuru sana familia yangu hasa Mke wangu Mpendwa Magdalena Wilbert na Watoto wetu Emanuel, Ibrahim na Mussa kwa Ushirikiano wa karibu walionipa ikiwemo kunitia Moyo.

Furaha yangu kubwa ni kuona nimehitimisha Kipindi hiki cha Miaka mitano nikiwa CHADEMA na nitaendelea kuwa CHADEMA hata nikiukosa Uwakilishi.

Garatwa,
Diwani & M/Kiti CHADEMA Serengeti.
10 June, 2020.

Hakika haya ni maneno ya kishujaa sana kutoka kwa huyu diwani pamoja na majaribu yoote ya kununuliwa lkn alipambana na kutimiza ndoto yake ya kuwahudumia walio mchagua.

Hongera mh DiwaniView attachment 1474261
Msafara wa kenge hakosekani mtoto wa mamba!
 
Diwani huyu sasa nadhani ni wakati wake kuwania ubunge maana kama ni mtihani kafauru kwa grade A
hongera mhe. wewe unajitambua, sio kudanganya watu eti unahamia CCM kuunga mkono, ht upinzani unaunga mkono
 
Diwani huyu sasa nadhani ni wakati wake kuwania ubunge maana kama ni mtihani kafauru kwa grade A
Kuna picha moja wakati Magufuli yupo kule alikua ndo pekee amevaa gwanda za CDM katikati ya msitu wa Mafisi
 
Nakumbuka, huyu dogo anajiamini sana na ana mapenzi ya kweli ya chama chake

Back
Top Bottom