Maneno ya Inocent Mugy kuhusu simu bandia zilizozimwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kutoka TCRA wametoa ufanunuzi wa kufungiwa kwa simu feki....

Ni June 16, 2016 ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki walizifungia simu feki zenye IMEI bandi.

Meneja wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mugy Anaeleza idadi ya IMEI zilizokamata na mtambo wao ambao umehusika kuzifungia simu feki.

‘Tukizungumza ambavyo vimezimwa kinachofanyika kuzifunga zile IMEI bandi ambazo kwa jana tumefanikiwa kuzifunga simu zenye IMEI zipatazo laki sita na elfu 3 kwa maana ya kwamba unakuta simu moja ina IMEI mbili kwasababu simu yenye laini mbili ina IMEI mbili sasa ziko simu zenye IMEI hadi nne‘- Innocent Mugy

‘Kwahiyo ambacho tumeblock jana usiku ni IMEI laki sita ikiwa ina maana hizi ni ambazo zinatumika kwenye simu feki, modern ya internet na IPAD, sasa sisi hatuwezi kutaja idadi ya simu ngapi tumezifungia ila tunachokijua ni kwamba IMEI laki sita ndio zimefungiwa zilizopo kwenye simu‘– Innocent Mugy

Zoezi hili bado linaendelea ambapo sasa hivi mtambo utakuwa unahakikisha simu zinazoingia bandi zitakuwa zinafungiwa, IMEI ni namba tambulishi kama unakumbuka tulisema kwamba kila simu inayotengezwa inapewa namba tambulishi, sasa simu ili itengenezwe lazima ipite kwenye mchakato kuhakikisha kuna vitu ambavyo havitakiwi viwepo kwenye simu-

Innocent Mungy
 
Nimewasiliana na ndugu na jamaa zangu hakuna hata mmoja aliyefungiwa simu, tena wengine wana simu hata majina na sura hazieleweki. TCRA wawe wa kweli kwa hili, nini hasa ilikuwa nyuma ya hii propoganda!!?
 
Mbona mi ninazo mbili na niliuliza kwa kutuma imei wakaniambia ni feki but now zinafanya kazi kama kawaida?
simu inaweza ikawa feki ila siku hizi watu wananunua imei number nakubadilisha.....watengenezaji wananunua imei....simu feki ila kwenye mitambo inaonesha imei yake imepitishwa FCE
 
‘Zoezi hili bado linaendelea ambapo sasa hivi mtambo utakuwa unahakikisha simu zinazoingia bandi zitakuwa zinafungiwa, IMEI ni namba tambulishi kama unakumbuka tulisema kwamba kila simu inayotengezwa inapewa namba tambulishi, sasa simu ili itengenezwe lazima ipite kwenye mchakato kuhakikisha kuna vitu ambavyo havitakiwi viwepo kwenye simu
Ruttashobolwa Inavyoonekana zoezi limeisha !!.. wanasubiri simu mpya !
 
Duuh kazi ipo mimi nina Sony experia fueki hahahahahah inagonga mzigo now, kazi ipo ninasubiri waniblock nilitupe lakini ngoja nitume msg, kupiga vya mwisho mwisho na mawhatsapp ya fujo
 
Mi najiuliza tu topic kuwekwa kwa jukwaa la siasa na si Technology au Habari na hoja mchanganyiko.

Kuna muingiliano wowote baina yake...?.
 
Back
Top Bottom