Jing chu
JF-Expert Member
- May 9, 2019
- 385
- 592
Wakuu bila shaka hamjambo!
Kuna mzee kaniambia kijana siku hizi ndoa zenu mkigombana mwezi unaisha hamjapatana. Hii ni ajabu sana. Nikamuuliza kwa nini mzee, akasema tatizo ni aina ya nyumba na vitanda mnavyotumia, sisi zamani tulijenga nyumba yenye vyumba vilivyotosheleza wanafamilia hakuna chumba za ziada wala cha wageni, mgeni akija alikuwa anapishwa au analala na wenyeji. Mkigombana usiku mnajikuta mnaelewana tu.
Akaendelea kusema, vitanda vyetu vilikuwa vyembamba yaani upana usiozidi 3½ kwa 6 kwa hiyo mkigombana ni rahisi kuyamaliza usiku wake maana mpende msipende mtaamshana hisia tu.
Sasa hivi kitanda 6×6 mkigombana ni kama mnaishi vijiji tofauti, Mara atoke chumbani akalale chumba kingine. Ajabu sana!
Eti wakuu hii ina uhusiano wowote?