GANG MO
JF-Expert Member
- Dec 6, 2016
- 2,087
- 2,193
Nimeichota kwa mwanafalsasa Herbert Faustine, eti hii ni kauli ya mkuu wa wilaya ya Arumeru aliyemkamata mwandishi wa habari kwa kumtuhumu kuandika habari za uchochezi. Eti kasema "KAMA KUNA MWANAUME NA AJE KUNIHOJI".
MAONI YANGU
Siamini kama maneno haya yanatoka kwa rafiki yangu Mnyeti, ni mtu ninayemfahamu na ni rafikiyangu. Siamini kama Mnyeti huyu anaweza kutia maneno makali na ya dhihaka kama haya! Wakati wa awamu ya kwanza,mwalimu Nyerere alikuwa na utamaduni wa kuwakuza vijana kiuongozi. Mwalimu aliwajenga kwanza vijana kabla hajawakabidhi madaraka makubwa.
Ndani ya chama,vijana walilelewa kuanzia ngazi ya chipukizi. Mwalimu alijenga vyuo vya uongozi na vyuo maalum kwa ajili ya kuwajenga vijana kifalsafa, wajue maadili ya kiongozi bora na hata kujua maadili ya kiongozi. Katika kuwajengea heshima viongozi, mwalimu aliwajengea viongozi mpaka maeneo yao maalum kwa ajili burudani(leaders club). Mwalimu aliwahimiza vijana wake wawe viongozi na sio watawala, mwalimu siku zote alihubiri uongozi bora na si utawala bora.
Taifa sasa linaongozwa na watawala badala ya viongozi. Watu wanaopewa madaraka badala ya kuongoza wao wanatawala. Huu ni ugonjwa mbaya unaowatafuna vijana wenye nafasi, badala ya kuongoza wao wanatawala! Leo unashangaa baadhi ya viongozi wetu wanatoa kauli zenye utata, zisizounganisha watu, zinazochochea chuki balada ya upendo, zinazochochea mpasuko badala ya umoja, masikitiko badala ya furaha, kukata tamaa badala ya matumaini.
Vijana mliopewa nafasi jueni dhamana iliyo mbele yenu, ongozeni watu badala ya kuwatawala. Mkitaka kutawala hamtaweza fanikiwa, ongozeni ili mfanikiwe. Unabaki kustaajabu, viongozi wetu wanataka nini hasa? Ndani ya mwaka mmoja karibu waandishi wa habari watano wamekutana na mkono wa watawala. Kama viongozi wangekuwa wanatuongoza, tusingesikia kauli za vitisho bali furaha na kuonesha njia.
Pole sana Halfan Lihundi.
By Dotto Bulendu