Maneno ya Dotto Bulendu kwa mkuu wa wilaya ya Arumeru

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
1,887
2,000
Nimeichota kwa mwanafalsasa Herbert Faustine, eti hii ni kauli ya mkuu wa wilaya ya Arumeru aliyemkamata mwandishi wa habari kwa kumtuhumu kuandika habari za uchochezi. Eti kasema "KAMA KUNA MWANAUME NA AJE KUNIHOJI".

MAONI YANGU

Siamini kama maneno haya yanatoka kwa rafiki yangu Mnyeti, ni mtu ninayemfahamu na ni rafikiyangu. Siamini kama Mnyeti huyu anaweza kutia maneno makali na ya dhihaka kama haya! Wakati wa awamu ya kwanza,mwalimu Nyerere alikuwa na utamaduni wa kuwakuza vijana kiuongozi. Mwalimu aliwajenga kwanza vijana kabla hajawakabidhi madaraka makubwa.

Ndani ya chama,vijana walilelewa kuanzia ngazi ya chipukizi. Mwalimu alijenga vyuo vya uongozi na vyuo maalum kwa ajili ya kuwajenga vijana kifalsafa, wajue maadili ya kiongozi bora na hata kujua maadili ya kiongozi. Katika kuwajengea heshima viongozi, mwalimu aliwajengea viongozi mpaka maeneo yao maalum kwa ajili burudani(leaders club). Mwalimu aliwahimiza vijana wake wawe viongozi na sio watawala, mwalimu siku zote alihubiri uongozi bora na si utawala bora.

Taifa sasa linaongozwa na watawala badala ya viongozi. Watu wanaopewa madaraka badala ya kuongoza wao wanatawala. Huu ni ugonjwa mbaya unaowatafuna vijana wenye nafasi, badala ya kuongoza wao wanatawala! Leo unashangaa baadhi ya viongozi wetu wanatoa kauli zenye utata, zisizounganisha watu, zinazochochea chuki balada ya upendo, zinazochochea mpasuko badala ya umoja, masikitiko badala ya furaha, kukata tamaa badala ya matumaini.

Vijana mliopewa nafasi jueni dhamana iliyo mbele yenu, ongozeni watu badala ya kuwatawala. Mkitaka kutawala hamtaweza fanikiwa, ongozeni ili mfanikiwe. Unabaki kustaajabu, viongozi wetu wanataka nini hasa? Ndani ya mwaka mmoja karibu waandishi wa habari watano wamekutana na mkono wa watawala. Kama viongozi wangekuwa wanatuongoza, tusingesikia kauli za vitisho bali furaha na kuonesha njia.

Pole sana Halfan Lihundi.

By Dotto Bulendu
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,843
2,000
Kwani aliyempa madaraka wala hana habari kuwa somebody is misusing power. Lakini aliwaambia kuwa weka ndani, they are doing the same. Mnyeti siyo wa kumlalamikai! Bulendu, sikulaumu una haki ya kuogopa. But Mnyeti is not the right person to blame! Tunatafuta weak point!
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,053
2,000
hivi kitabu kinaitwa Bosi kilipotelea wapi? kiliandika yote haya. naombeni mnisaidie kwa kukipata.
 

KirilOriginal

JF-Expert Member
Feb 13, 2012
2,140
2,000
Hovyo kabisa huyu mkuu wa wilaya, siku ya mwenge hapa wilayani alilewa akawa anaongea matusi makubwa aibu tupu, na kwa kuwa hakuna wa kumfanya lolote inabidi tujinyamazie
Mkuu wa nchi amepanga safu yake anajua anachokitaka kwa hawa watu na ndicho wanachokifanya na roho yake inaburudika kwa matendo yao, I mean prezida haya mambo anayahusudu sana
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
5,511
2,000
The Britons always say,"Birds of the same feather fly together"
Kwamba ndege wa manyoya yanayofanana huruka pamoja!
Hii maana yake ni kwamba Rais Magufuli ameweka/teua Wakuu wa Wilaya na Mikoa wenye tabia kama zake, yaani ubabe,umwamba,jeuri, arrogancy and very sturbborn!! Angalia tabia za kina Makonda, Mrisya Gambo,Mnyeti and all the like!
 

wizzy more

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
432
250
Nchi inaongozwa kilevi c hata yule mwngne aliingia bungen amelewa ndo wale wale akuna tofaut kati ya mfunko wa ndoo na wa soda vyote vinafunka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom