Maneno ya busara ya Zitto yalivyochukuliwa juu juu

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
NAKUOMBA UFUATILIE KWA MAKINI KAULI ZA ZITO HAPA CHINI UTAELEWA VIZURI. TUWE MAKINI NA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO VINACHUKUA MANENO NUSU NUSU KWA INTEREST ZAO. NIMEPENDA GAZETI LA MWANANCHI, LIMEANDIKA MANENO YA ZITO KWA UPANA WAKE: FUATILIA... NUKUU HAPA CHINI

"CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?" Alihoji Zitto.
"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.

"Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.

"Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi."

"Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu," alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

aliongeza kusema KUNA WATU WANAJIFANYA WAO NI CHADEMA ZAIDI YAKE WAKATI YEYE ANA MIAKA 16 CDM
 
Mi nashukuru kwa kuniachia wazi jimbo,watu wa kigoma kaskazini nipeni jimbo,niko tayari kushirikiana naye na kuendeleza mikakati mizuri ya maendeleo aliyoianzisha
 
Maneno yake mafupi kwenye FB wall yake:

"Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005"
 
Mwanzo wa CDM kuwa imara.
1.Kauli za zitto
2.Kupoteza umeya mwanza
Mtake msitake tatizo si Mh zitto kutanganza kuwania urais 2015 laaa.Tatizo kuwa Mh ZITTO alikuwa hana cha kwa waambia watu walioudhulia mkutano huwo.Swali langu je walioandaa mkutano ndo lilikuwa lengo la kumwalika zitto pale.? Amini na usiamini Mh ZITTO anakwenda kama kinyonga.Kauli hizi zinaweza kuwa zinamsaidia au azimsaidiii huko twendako. Nanukuu msemo wa Marehemu BA,WA TAIFA JK.(Nyumba isipokuwa na msingi IMARA ikikumbwa na dhoruba itapata nyufa zinaweza kuwa kubwa au kidogo) Fikiri
 
watu wakikuchukia hata useme nini hawaoni,kifupi kuna wapinzani wa zito ndani ya chadema ambao wanachukulia urafiki wake na wana CCM au uwazi wake wa fkra ni kukosa adabu kwa viongozi wa juu au usaliti
 
NAKUOMBA UFUATILIE KWA MAKINI KAULI ZA ZITO HAPA CHINI UTAELEWA VIZURI. TUWE MAKINI NA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO VINACHUKUA MANENO NUSU NUSU KWA INTEREST ZAO. NIMEPENDA GAZETI LA MWANANCHI, LIMEANDIKA MANENO YA ZITO KWA UPANA WAKE: FUATILIA... NUKUU HAPA CHINI

"CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?" Alihoji Zitto.
"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha.
Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.

"Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.
.
.
.

"

Hapo kwenye blue colour,
Katiba ya nchi inasemaje kuhusu umri wa kugombea urais ??
Au katiba imeshabadilika ??
Na wewe mwandishi wa hoja hii unaandika '...Maneno ya 'Busara' ya Zitto...' !!! Huku ukijua kuwa hawezi kuwa na sifa kwa kigezo cha umri kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya nchi !!
Au Zitto hajui ??
Na yeye kama mbunge na mwana siasa anatamka kugombea urais huku akijua kuwa hatakuwa na sifa ifikapo mwaka 2015 !!
Hayo ndio maneno ya 'Busara' uliyoyanukuu !!
Kweli kazi ipo hapa JF !!
 
Amefanya ki2 cha msingi. Nadhani wengine wangeiga hasa kama wanashindwa kutekeleza ahadi katika majimbo yao.

zzk, sijajua amesaidia vipi jimbo lake, ila angeendelea kidogo kwa ajili ya kuokoa mkoa wa kigoma hasa katika masual nyeti kama barabara na umeme kushirikiana na wenzake wa upinzani. Baado ana muda na hayo anayosema, kama kweli anajiona ni productive.
 
Kitu kimoja nafurahishwa nacho ni vile viongozi wakuu katika CDM wameamua kupiga kimya katika kauli za Nyepesi Zuberi Kabwe. Huyu ni kibaraka anayetumiwa ili kukigawa chama cha CDM kwani ni dhahiri CCM inamgwaya Dr. Slaa na inahofu kuwa akisimama tena, na mgombea akawa EL mwenye kashfa, patachimbika na ukizingatia now days wananchi hasa wa huko vijijini ambako jua linachelewa kutoka na kuwahi kuzama, ndio wamezibuka na sio wa kudanganywa tena.

Mimi nafikiri sio Nyepesi tu, watokee watu wengi tu wengine wachukue form za kugombea urais ndani ya CDM, lakini baada ya hapo si kuna NEc ya CDM....ambayo itam'bashe asiyestahili. Halfu ikatuletea mtu wa ukweenh....hah hah!

Zito yupo katika mkakati mzito wa CCM na tiss, ili kupunguza upinzani katika kuhakikisha walioshika rasilimali za nchi au wanao nufaika na mikataba mibovu wanaendelea kubunya hadi mwisho......kwani Zito ni nani has ili akisema jambo tayari libebeshwe vichwa vya habari kama sio mpango mahususi wakumpaisha?

Humu katk JF, ndugu Ritz anajua kuwa endapo waziri mkuu (mjiuzuru kwa kashfa) akipita kama mgombea wa CCM, kikwazo ni Slaa.....sasa anakuja na ishu ya ukanda baada ya kuona ishu ya udini, inawatufuna walioianzisha.

Kibanga Msese
 
Mwanzo wa CDM kuwa imara.
1.Kauli za zitto
2.Kupoteza umeya mwanza
Mtake msitake tatizo si Mh zitto kutanganza kuwania urais 2015 laaa.Tatizo kuwa Mh ZITTO alikuwa hana cha kwa waambia watu walioudhulia mkutano huwo.Swali langu je walioandaa mkutano ndo lilikuwa lengo la kumwalika zitto pale.? Amini na usiamini Mh ZITTO anakwenda kama kinyonga.Kauli hizi zinaweza kuwa zinamsaidia au azimsaidiii huko twendako. Nanukuu msemo wa Marehemu BA,WA TAIFA JK.(Nyumba isipokuwa na msingi IMARA ikikumbwa na dhoruba itapata nyufa zinaweza kuwa kubwa au kidogo) Fikiri

safu nyembamba ya uongozi ndio chanzo cha yote
 
chadema tutasimama imara daima...haijalishi ni jinsi gani mtampamba zitto,ukweli utabaki pale pale jamaa anatumika na chadema aitaingia kwenye mtego wake...
 
Hapo kwenye blue colour,
Katiba ya nchi inasemaje kuhusu umri wa kugombea urais ??
Au katiba imeshabadilika ??
Na wewe mwandishi wa hoja hii unaandika '...Maneno ya 'Busara' ya Zitto...' !!! Huku ukijua kuwa hawezi kuwa na sifa kwa kigezo cha umri kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya nchi !!
Au Zitto hajui ??
Na yeye kama mbunge na mwana siasa anatamka kugombea urais huku akijua kuwa hatakuwa na sifa ifikapo mwaka 2015 !!
Hayo ndio maneno ya 'Busara' uliyoyanukuu !!
Kweli kazi ipo hapa JF !!

Katiba ya nchi inasemaje kuhusu umri wa kugombea urais ??
Au katiba imeshabadilika ?
?

mkuu umeuliza maswali haya,which means hujui,sasa kwanini usijipe muda ujibiwe kwanza hayo maswali ili uwe kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuponda ukiwa umeelimika kupitia jukwaa hili?
 
chadema tutasimama imara daima...haijalishi ni jinsi gani mtampamba zitto,ukweli utabaki pale pale jamaa anatumika na chadema aitaingia kwenye mtego wake...

vipi mliposhindwa vibaya kweny uchaguzi wa meya mwanza,zitto alitumika pia kuhakikisha mnashindwa u M4C ndio ilitumiwa na ccm kuwashinda?
 
mvumilivu hula mbivu. Zitto angesubiri had 2025 basi tungeongea mengine humu.
 
Kitu kimoja nafurahishwa nacho ni vile viongozi wakuu katika CDM wameamua kupiga kimya katika kauli za Nyepesi Zuberi Kabwe. Huyu ni kibaraka anayetumiwa ili kukigawa chama cha CDM kwani ni dhahiri CCM inamgwaya Dr. Slaa na inahofu kuwa akisimama tena, na mgombea akawa EL mwenye kashfa, patachimbika na ukizingatia now days wananchi hasa wa huko vijijini ambako jua linachelewa kutoka na kuwahi kuzama, ndio wamezibuka na sio wa kudanganywa tena.

Mimi nafikiri sio Nyepesi tu, watokee watu wengi tu wengine wachukue form za kugombea urais ndani ya CDM, lakini baada ya hapo si kuna NEc ya CDM....ambayo itam'bashe asiyestahili. Halfu ikatuletea mtu wa ukweenh....hah hah!

Zito yupo katika mkakati mzito wa CCM na tiss, ili kupunguza upinzani katika kuhakikisha walioshika rasilimali za nchi au wanao nufaika na mikataba mibovu wanaendelea kubunya hadi mwisho......kwani Zito ni nani has ili akisema jambo tayari libebeshwe vichwa vya habari kama sio mpango mahususi wakumpaisha?

Humu katk JF, ndugu Ritz anajua kuwa endapo waziri mkuu (mjiuzuru kwa kashfa) akipita kama mgombea wa CCM, kikwazo ni Slaa.....sasa anakuja na ishu ya ukanda baada ya kuona ishu ya udini, inawatufuna walioianzisha.

Kibanga Msese

Hawako kimya kama unavyodhani mkuu,nao wanaweweseka kama nyie tu na kauli ya zitto kuonyesha nia.,msikie freemani mbowe anachosema hapa

Siongozi Genge la wasaka URAIS - Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.

Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa CDM kwa sasa ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka.Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C

Source: Tanzania Daima​
 
Back
Top Bottom