Maneno ya Busara ya Obama, ana haki kushangiliwa. Nani ataweza kumuenzi Madiba kwa vitendo!

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,597
2,000
Rais Obama ameongea maneno ya Busara sana, Amesema viongozi wengi ni wanafiki.

Obama amesema viongozi wengi wanamsifia Mandela kwa maneno, hawawezi kutenda hata moja. Jeee Rais wetu ataweza kumuenzi Mandela? Je ataweza kufanya mabadiliko muhimu ili kuunda Taifa la upinde?

taifa la upinde/rainbow nation. yaani taifa la rangi zote. Yaani hakuna ubaguzi. wengine wasome st, international schools, na wengine wasome St kayumba. Je kikwete ataweza kuleta Katiba mpya inayotakiwa?

Je Kutakuwa na TUme Huru ya Uchaguzi?

msome Obama hapa chini

"With honesty, regardless of our station or circumstance, we must ask: how well have I applied his lessons in my own life?" he asked.
Obama warned world leaders that "we cannot allow our progress to cloud the fact that our work is not done."
"Around the world today, we still see children suffering from hunger, and disease; run-down schools, and few prospects for the future. Around the world today, men and women are still imprisoned for their political beliefs; and are still persecuted for what they look like, and how they worship, and who they love. That is happening today," he said to cheers from the exuberant crowd, braving the rain to celebrate Mandela's life.
"There are too many people who happily embrace Madiba's legacy of racial reconciliation, but passionately resist even modest reforms that would challenge chronic poverty and growing inequality," Obama cautioned. "There are too many leaders who claim solidarity with Madiba's struggle for freedom, but do not tolerate dissent from their own people. And there are too many of us who stand on the sidelines, comfortable in complacency or cynicism when our voices must be heard."


Source: South Africa, Soka city and Yahoo, BBC, CNN, Reutars
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,597
2,000
Sasa Tanzania tuelekee kwenye mabadiliko

Iundwe tume ya Ukweli na usuluhishi, mafisadi warudishe pesa kutoka Uswisi wasamehewe

Waliomtesa uliomboka wajitokeze wasamehewe

Walioiba kura wajiuzulu

Kuwe na tume huru

Katiba mpya
 

Mipangomingi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,712
2,000
Ni maneno machache lkn yana uzito wa kitabu cha kurasa 1,000. Kweli ifikie mahali vioongozi wa kitaifa na watu wa mataifa pia wabadilike na wafikirie kiutu zaidi. Sote ni binaadamu. Kweli inaingia akilini kiongozi unaiba au unatumia madaraka vibaya na kudhulumu haki ya mtoto au mama mjamzito ambaye hana uwezo wa kula hata mlo mmoja; maji anafuata km 20 tena yaliyochanganyika na kinyesi cha wanayama, hali ya kuwa wewe unaeiba unakaa masaki au Osterbay?

Utajiita msomi kweli kwa kuiba fedha za kumsaidia huyo mama mjamzito au mtoto wa kijijini? Kweli una ubinaadamu wewe uliesoma Harvard, Cambridge hata kutumukiwa PhD nk kisha unamdhulumu mtu mwenye shida hizi kwa kukwapua fedha ambazo zingetumika kumletea maji au huduma ya Afya? Kweli wewe mtu unayelipwa Mil 10 kwa mwezi na posho kibao, still unamdhulumu asiyeweza hata kupata sh. 100 kwa siku? Hii elimu yako itakuwa imekusaidia nini? Halafu inakuwa nini unapokuwa na nyumba 10 za wizi? Halafu inakuwa nini unapokuwa na Bilions Uswizi, New jersy au Singapore? Kwanini hizo pesa ulizoiba usiwekeze nchini mwako? Tujipime!

Hapana, tuliopata nafasi ya kusoma, kutembea, kupata mali au kupata nafasi ya kuwatudumia watu tufikiri tena. Hivi tunavyofikiri sasa sivyo jamani.
 

kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,174
0
Obama anajua sana kupanga maneno, ukimsikiliza unaweza kusema malaika si ndo huyu.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,597
2,000
CCM ni tofauti na TANU

CCM ni tofauti na ANC

Nitajie viongozi wa ANC ama wa SOUTH AFRICA wanaotuhumiwa kuwa na PESA USWISI?
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
41,588
2,000
Obama alichoongea cha maana leo ni aliposema

Mandela led his nation towards justice..


na kuna siku alisema 'Mandela took history with his hands'

..
 

BALAKI

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
371
0
Obama kakiri kweli kwamba hata wao kama viongoz hawajaweza kumuenzi mandela kwa vitendo, sembuse huko tz ambako wanaoiba mali za umma wanaonekana mashujaa, tena wakihama walikozaliwa na kwenda kwa majiji makubwa, huku wakiwaacha maskini ndugu n majiran wa kijijin kwao wakiwa hawana hakika hata ya mlo mmoja kwa siku achilia mbali maji ambayo ngeweza chimba angalau kisima kimoja tu na akakumbukwa milele.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,597
2,000
kama viongozi wa sasa watashindwa kurejesha imani kwa wananchi na kuleta mabadiliko yanayotakiwa, wataondolewa madarakani
 

MZALENDOWAKWELIKWELI

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
324
250
Hata Obama ni mnafiki vilevile coz yuko after maslahi ya wamarekani kuliko utu....alidiriki kuvamia Libya na kufadhili magenge ya wahuni kumuondoa Gadafi aliyekuwa anawapa wananchi wake huduma zoote na kumuacha Bagbo ambaye kwa wakati uleule alikuwa akiua watu wengi Ivory Coast simply tu coz hawana rasilimali yeyote ya kuvuna....Waafrica tuamke!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom