#COVID19 Maneno ya Askofu Gwajima yamepata nguvu, kitaa wanaamini wakubwa wamehongwa

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Jun 12, 2021
1,061
2,475
The come back of Rashid Gwajima siyo ya kitoto we mchukulie kama chizi au serious(mimi huwa namuona mwehu )ila nipo Tabata hapa ka grocery fulani tunabishana suala la chanjo reference ya hawa jamaa ni video ile ya Gwajima najaribu kuwaelewesha nimeshindwa,anyway nime stick kula beer tu huku nacheka.

Nimependa part alipopiga kunako kwamba kuna watu wamechukua FUNGU ili watupe hofu ya Corona akauliza mbona wakati wa Magufuli haya hayakuwepo?

Hivi Shehe Ponda au Mnyika angeongea speech ile leo angekuwa uraiani kweli?
 
Afadhari wewe watu wa bar ndiyo hawaelewi.

Mimo nipo staff moja na walimu wote wana degree na masters lakini Gwajima ni reference yao,yaani wamesababisha nimepewa onyo leo kwa kelele.

Ujinga bado ni mkubwa hapa nchini.
 
Hili suala la CORONA limekuwa kizungumkuti kwa sasa kwenye jamii yetu.

Nguvu kubwa inayotumika kuwashawishi watu wapatiwe chanjo pia nguvu kubwa inayotumika dhidi ya watu wanaotoa maoni yao dhidi ya chanzo vinazidi kuzua maswali na hofu kuu kwa wananchi.

Nadhani huu ndio muda muafaka kwa wataalamu kulitolea ufafanuzi wa kitaalamu hizi chanjo na sio kuwazodoa watu wanaopingana na chanjo.

Hayo malumbano ndio yanazidi kuwaweka wananchi njia panda na kuwajaza hofu.

Kama kupata chanjo ni khiyari ya mtu basi ibakie tu hivyo hivyo na kama kunatokea mtu anatoa maneno yanayoonekana kupotosha basi jukumu la wataalamu ni kutoa ufafanuzi kwa wananchi ili washawishike na sio vitisho na maneno ya kejeli.

Kupanic baada ya kutoa maelezo kunaleta tafsiri ya kuwa hao wanaopanic huenda wana maslahi na hii chanjo kwa namna moja au nyingine.

Mungu ibariki Tanzania
 
Kitu gani kinakuhakikishia usalama wako baada ya hii chanjo hali ya kuwa tunaambiwa hata ukipata chanjo uwezekano wa kupata maambukizi uko pale pale?
 
Toka enzi za JK yaliiuwepo aliambiwa kahongwa suti, JK alijua tu kushughulika navyo alisema ni ka upepo katapita.

Hivyo Gwajima hoja yake Kama Haina mashiko itapita Kama upepo tu,ila Kama Kuna hoja itaendelea kuvuma.
Gwajima ameongea mambo yanayoonekana ya kipuuzi lakini yamezusha taflani kwa sababu yanagusa moja kwa moja uhai na mustakabali wa afya za watu wengi sana kwa wakati huu wa Corona.

Hata kama Gwajima ameongea hoja za kipuuzi lakini zinahitaji ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika kulingana na hali ya taharuki mitaani.

Kuendelea kumtusi na kumdhihaki Gwajima ni kuendeleza sintofahamu kwenye jamii na kuzidi kuaminika kwa Gwajima.
 
Kweli kabisa wataalamu watokee wamjibu au nao hawana uhakika Kama Gwajima.
 
Hili suala la CORONA limekuwa kizungumkuti kwa sasa kwenye jamii yetu.

Nguvu kubwa inayotumika kuwashawishi watu wapatiwe chanjo pia nguvu kubwa inayotumika dhidi ya watu wanaotoa maoni yao dhidi ya chanzo vinazidi kuzua maswali na hofu kuu kwa wananchi.

Nadhani huu ndio muda muafaka kwa wataalamu kulitolea ufafanuzi wa kitaalamu hizi chanjo na sio kuwazodoa watu wanaopingana na chanjo.

Hayo malumbano ndio yanazidi kuwaweka wananchi njia panda na kuwajaza hofu.

Kama kupata chanjo ni khiyari ya mtu basi ibakie tu hivyo hivyo na kama kunatokea mtu anatoa maneno yanayoonekana kupotosha basi jukumu la wataalamu ni kutoa ufafanuzi kwa wananchi ili washawishike na sio vitisho na maneno ya kejeli.

Kupanic baada ya kutoa maelezo kunaleta tafsiri ya kuwa hao wanaopanic huenda wana maslahi na hii chanjo kwa namna moja au nyingine.

Mungu ibariki Tanzania
Viongozi wajitokeze wapangue kuanzia hoja za Magufuli maana ndo walimwamini zaidi,na alidai chanjo Zina madhara.
Halafu wajibu za Gwajima kuliko kurukia conclusion tu eti anapotosha.
 
Gwajima Ana hoja mm pia nimejaribu na Niko karibu kbsa na doctar bigwa apa KCMC na ni mtalamu haswa naish na mdgo ake wenyewe wanasema hawna imani na chanjo ya korona hataki na Wala czani kma atachanjwa, huyo ni doctor sas mm Ni Nani kuchanjwa au nimpinge gwaji boy.
 
The come back of Rashid Gwajima siyo ya kitoto we mchukulie kama chizi au serious(mimi huwa namuona mwehu )ila nipo Tabata hapa ka grocery fulani tunabishana suala la chanjo reference ya hawa jamaa ni video ile ya Gwajima najaribu kuwaelewesha nimeshindwa,anyway nime stick kula beer tu huku nacheka

Nimependa part alipopiga kunako kwamba kuna watu wamechukua FUNGU ili watupe hofu ya Corona akauliza mbona wakati wa Magufuli haya hayakuwepo?

Hivi Shehe Ponda au Mnyika angeongea speech ile leo angekuwa uraiani kweli?
na aliwataja majina😅😅
 
Gwajima Ana hoja mm pia nimejaribu na Niko karibu kbsa na doctar bigwa apa kcmc na Ni mtalamu haswa naish na mdgo ake wenyewe wanasema hawna imani na chanjo ya korona hataki na Wala czani kma atachanjwa ..huyo ni doctor sas mm Ni Nani kuchanjwa au nimpinge gwaji boy....
piga nyungu
 
The come back of Rashid Gwajima siyo ya kitoto we mchukulie kama chizi au serious(mimi huwa namuona mwehu )ila nipo Tabata hapa ka grocery fulani tunabishana suala la chanjo reference ya hawa jamaa ni video ile ya Gwajima najaribu kuwaelewesha nimeshindwa,anyway nime stick kula beer tu huku nacheka

Nimependa part alipopiga kunako kwamba kuna watu wamechukua FUNGU ili watupe hofu ya Corona akauliza mbona wakati wa Magufuli haya hayakuwepo?

Hivi Shehe Ponda au Mnyika angeongea speech ile leo angekuwa uraiani kweli?
Wewe unayejiona mjanja, ndo zwazwa......hahahaha
 
Back
Top Bottom