Maneno Mbofumbofu Kuhusu Dangote Yanaandikwa Na Watu Wenye Matatizo Na Serikali

BungelaKatiba2014tz

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
1,233
1,500
Maneno mbofumbofu kuhusu Dangote Cement yanaandikwa na watu wenye matatizo na serikali.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini Tanzania, Bi Esther Baruti wakati akihojiwa na Radio Sauti ya Amerika.

Amefafanua kuwa kiwanda hakijafungwa, bali kimesimamisha uzalishaji kwa muda. Na kwamba hii si mara ya kwanza kwa kiwanda hicho kusimamisha uzalishaji.

Amesema kuwa Dangote alipewa kila kitu alichoomba. Alipewa ardhi bure, msamaha wa kodi kwa kila kitu alicholeta kwa ajili ya kiwanda; ana msamaha wa kodi kwa mafuta ya dizeli. Na amepewa vibali vya kutosha kuajiri wataalam wa kigeni.

Anasema pia Dangote Cement ina mwakilishi katika kamati ya kitaifa ya gesi na makaa ya mawe. Na kwamba kampuni hiyo imenunua tani milioni tano za makaa ya mawe ya Tanzania.

Amesema uzalishaji umesimama kutokana na matatizo ya kiufundi ambayo yanashughulikiwa. Na kwamba wanaosambaza maneno mabaya ni watu wa kati ambao wanataka kuizuia Dangote Cement gesi badala ya TPDC. C&P
 

mamseri

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
685
250
Haya sasa naona wamepigwa mkwara wakanushe maana haiji akilini mawaziri wawili wazungumze kuhusu kufungwa kiwanda halafu leo mtuambie ni marekebisho. Ina maana mawaziri walitudanganya?
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,194
2,000
Duuh...... Inawezekana ikawa Mr Hajaribiwi keshawapiga mkwara mzito hao Dangote na kuwaelekeza cha kuongea na waandishi wa habari!

Kwa kuwa haiingii akilini kuona wafanyakazi wa Dangote wapo mitaani wakiwa 'jobless' halafu huyo Mkurugenzi mkazi wa Dangote anaongea na waandishi wa Habari akikanusha kuwa Dangote haijafungwa!
 
  • Thanks
Reactions: 999

igp

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
839
500
Lakini hawatafanikiwa kumchonganisha Dangote na serikali ya jpm.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,676
2,000
Nachukua break kufuatilia sakata la Dangote kwa sasa manake haiwezekani; hivi sasa naambiwa 1+1=2, nusu saa baadae naambiwa 1+1=11...
 
Top Bottom