Maneno Mbofu Mbofu kutoka kwa viongozi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno Mbofu Mbofu kutoka kwa viongozi wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chapakazi, Jul 26, 2009.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ninapendekeza kuanzisha hii thread itakayoweka rekodi ya maneno 'ovyo ovyo' yaliyotamkwa na viongozi wetu...
  Jamani feel free kujazia humu, ikiwezekana tuweke hata date.

  “Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyie wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu Alifoka Mkuchika.


   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  "Wote wanajisumbua, rais atayemfuata JK atatokea ZANZIBAR, na kwa jina anaitwa Dr.HUSSEIN ALI HASSAN MWINYI. Habari ndio hiyo, uipende, usiipende shauri yako!" - Alwatan :)
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  "Pamoja na matatizo makubwa aliyoanza nayo Mh Kikwete aliposhika ofisi kama vile ukame, upungufu wa chakula, uhaba wa umeme, kupanda kwa bei ya nishati ya petroli, kuyumba kwa uchumi wa dunia, lakini amekuwa very steady na issues za wananchi, ukweli ni kwamba ni kiongozi imara na mzuri.
  Wakati wote amejikita katika kuhakikisha kuwa matatizo ya wananchi yanatafutiwa ufumbuzi, ni kiongozi anayeangalia mbali." -Pundamila07
   
 4. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  huyo punda naye kiongozi? au kumbukizi tu
   
 5. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe - Mhe. CD Msuya.

  Kama daladala zimekoma kutoa huduma, basi pandeni maroli au tembeeni kwa miguu kuja kazini - Mhe. BP Mramba.
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Ni bora Watanzania wale nyasi ili ndege ya Rais inunuliwe- Mhe. Basil Pesambili Mramba
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  "Dola millioni moja nayo ni hela? hivyo ni vijisenti tu ......." -Mhe Andrew Chenge.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ndio, ni kiongozi anayekaa jamii forums kuitetea serikali ya mafisadi:D
   
 9. M

  MathewMssw Member

  #9
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliwaambia wagogo watunze pumba ili wakati wa njaa waleeeeeeee! wakati ni waziri mkuu wa TZ
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna hii niliipenda sana. Hapa ni mwishoni wa vita vya Iddi Amini, baada ya kumn'goa nduli.
  Amin was toppled by a combined military force of Uganda exiles and Tanzanian troops on April 11, 1979. On December 10, 1980, Ugandans held a general election, the first one since Independence in 1962, and the Democratic Party won by a majority of 75 seats out of 108 seats. Paul Kawanga Semwogerere who was the leader of DP at that time, went to Paul Muwanga, accompanied by Mzee Evaristo Nyanzi, to make arrangements for Paul Semwogerere to be sworn in as the new President. Paul Muwanga who was the Chairman of the ruling military Commission at that time, told them he would check with President Nyerere in Dar es Salaam and advise them the following day.
  "Paul Muwanga telephoned Nyerere that very day and said: “Mr President, the Democratic Party has won the elections and Paul Semwogerere has just been here, he wants me to hand over to him. What should I do now?” Nyerere replied and said: “Paul Muwanga, you have got my army there – change all the results”. Muwanga changed all the results and gave victory to UPC/Obote. (The Commonwealth Observer Team declared the elections free and fair- Editor)"

  Inakumbusha katika kampeni za 1995, Mrema alivyokuwa popular sana Kilimanjaro. Nyerere alikuja kumpigia Mkapa kampeni, nadhani Uwanja wa Mashujaa, lakini watu walimzomea. Mzee akawaambia wananchi, mnayemtaka hamtampata. Sijui alihakikisha wanacheza mchezo huo huo walioufanya Uganda!!!
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  "Watanzania mna wivu wa kike" - B W Mkapa
   
 12. Lengeri

  Lengeri Senior Member

  #12
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "ukitaka kula lazima ukubaliwe na wewe uliwe hapo kidogo..." JAKAYA M KIKWETE alipolihutubia bunge khs azma ya serikali kulipia matangazo CNN
   
 13. S

  Simoni Member

  #13
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Alikuwa Msekwa aliyewaambia wale waliokuwa wanahoji uenyekiti wake wa vodacom huku akiwa spika. Akawaambia "waache wivu wa kike" UWT wakaja juu lakini hawakufika juu sana kwa sababu Mweyekiti taifa wao alikuwa mkewe Msekwa. Hahaha
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi Mchonga alijua kuwa mbaada ya kufanya hivyo alisababisha mauaji ya maelefu ya watu wasio na hatia nchini Uganda during Obote's 2nd term hadi 1987? Nasikia Obote alikuwa drunkard wa kutupa during his second term.

  Mchonga pia alifanya vivyo hivyo kwa uchaguzi wa zanzibar mwaka 1995 -- aliamuru ushindi ubadilishwe kwa kumpora maalim Seif na na kumpa dr salmini. tangu wakati huo zanzibar imekuwa hovyo hovyo kisiasa, pamoja na mauaji ya 2001.

  Mwal alikuwa kila kitu isipokuwa mwanademokrasia halisi.
   
 15. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuwa mwanademokrasia halisi tu, bali na ujuzi wa uchumi mbovu. Uzuri wake hakuwa fisadi, lakini aliweka system ya kuneemesha mafisadi.
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mtoto naona unaamini kilichoandikwa humo. Naomba chanzo cha taarifa hiyo tafadhali. Ilinganishe na hii kutoka TIME Magazine la 22 Disemba 1980:

  What one member of the British Commonwealth observer group called "the sheer sweep of maladministration" forced interminable queues of voters to wait for more than twelve hours at many polling booths. As a result, there was a second, unscheduled day of balloting. Even as the votes were counted, the ruling military commission headed by Paulo Muwanga first imposed, and then reversed, a highhanded decision to withhold the election results and even nullify them. Finally, after conflicting victory claims by the rival parties, the first official results showed that the apparent winner was the broadly based United People's Congress (U.P.C.), headed by Milton Obote, 56, the shrewd, sometimes ruthless former President who was deposed by Amin in 1971.

  Obote was openly backed by Muwanga as well as by Uganda's watchful patron, President Julius Nyerere of neighboring Tanzania. The U.P.C. appeared to have captured at least 66 seats in the 126-seat Parliament, compared with 44 for the Catholic-oriented Democratic Party (D.P.) of Paul Ssemogerere, 48, a U.S.-educated, longtime Obote adversary. The outcome was immediately contested by the D.P., with accusations that Obote had been steamrolled to victory. In reply, the Ugandan Army unleashed a two-hour barrage of gunfire in Kampala to intimidate Ssemogerere's angry supporters.

  Pia linganisha na hii kutoka Wikipedia:

  The period following the ousting of Amin proved to be a time of intense competition and fighting for power among different groups made up of political and ethnic rivals. Yusuf Lule had been installed as president by Tanzania. In June 1979, following a dispute over the extent of presidential powers, the National Consultative Commission (NCC), which was then the supreme governing body of the UNLF, replaced Lule with Godfrey Binaisa. Binaisa was himself removed on 12 May 1980 by the Military Commission, a powerful organ of the UNLF headed by the Paulo Muwanga, and whose deputy was Yoweri Museveni (then leader of Uganda Patriotic Movement). The country was then led by the Presidential Commission of Uganda with among others Paulo Muwanga, Yoweri Museveni, Oyite Ojok and Tito Okello. The Presidential Commission ruled Uganda until the December 1980 general elections which were won by Milton Obote's Uganda Peoples Congress. The elections were bitterly disputed. Yoweri Museveni alleged electoral fraud and declared an armed rebellion against the government of Obote, plunging the country into the civil war which came to be known as the bush war.
   
 17. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  .......Nyie vunjeni Muungano muone...........!!!!???
   
 18. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mh. kwenye hizo report ulizoweka hapo, unavyoona zinapinga hizi claims nilizoweka mimi? Kusema naamini au siamini mkuu hilo ni swala lingine. Ninachooamini ni kuwa anything is possible. Kwanza kabisa hii repoti nimetoa kutoka thread nyingine ilitoko humu - https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/31815-st-nyerere-s-18-political-miracles.html. Naona ni thread iliyoanzishwa na Maxence Melo aka JF Founder. Na inavyoonekana, ameitoa katika source kama ya gazeti hivi.

  Anyway... nimekuwekea maandishi mekundu sehemu ambapo hizi repoti zako zinaweza kuwa zinakubaliana na hii ya 'kwangu' au Maxence.

  1. Kilichomfanya Musseven kuingia katika bush war, sio baada ya kuona mchezo mbaya uliochezwa na wajanja?
  2. Je, Hiyo Military Commission iliyokuwa headed na Paulo Muwanga isingeweza kumwomba Nyerere ushauri?


  Kwanza kabisa naona hii ripoti ulizoleta zina-support uwezekano wa huu mchezo kuchezwa, zaidi ya kupiga kutokuwepo kwake.
   
 19. M

  MC JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  .."Meremeta ni Siri ya Jeshi, sitaizungumzia hata mkinisulubisha"..-- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pinda

  ...Ukihisi mtu ameuwa Albino, ukamfuatilia na kupata angalau uhakika flani wa swala hilo mmalize/muuwe/mchinje papo hapo.. Pinda

  .. Mama Migiro anaweza kutembea KIFUA WAZI na sisi wabunge tuko Nyuma yake tunashangilia.... Chiligati
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tusubiri ripoti ya MJJK tuone akisulubishwa kama mwenzake sasa. Ni ile ukiona mwenzako ananyolewa nywele, anza kuweka za kwako maji.

  hii ni mwisho. Huu ndo utawala wa sheria Pinda style.

  hii ilitolewa kwenye context gani mh? Maana ki-upesi upesi inatisha!!
   
Loading...