Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimesoma kwa makini taarifa juu ya hukumu ya jaji Rumanyika kuhusu Mbowe na matiko kuachiwa kwa dhamana. Zaidi ya kutengua uamumuzi wa mahakama ya Kisutu, jaji Rumanyika ametamka wazi kwamba
Hukumu ya jaji Rumanyika, kwa mtu yeyote mwenye akili, inaonyesha kwamba kuna jambo haliko sawa kuhusu hizi mahakama za mwanzo ambazo mara nyingi ndio husikiliza kesi za kisiasa kama ya kina Mbowe. Haingii akilini kwamba hakimu aliyetoa hukumu pale Kisutu juu ya suala la kina Mbowe ni mwepesi kiasi hiki katika kuelewa sheria, hadi "akamstaajabisha" jaji Rumanyika kwa kiwango alichosema.
Nimeshasema humu JF kwamba katika awamu ya tano kumekuwa na kila ishara kwamba serikali huwa inawafungulia mashitaka wanasiasa wa upinzani, na kutumia vipengele vya kisheria (legal technicalities) kwa namna ambayo katika hali ya kibinadamu inapita mipaka. Ofisi ya mwendesha mashitaka na wanasheria wa serikali kufanya kazi kwa amri toka juu hilo liko wazi, wala sio siri tena. Ni wazi lengo ni kuwakomoa wanasiasa wa upinzani kwa kuwaweka rumande muda mrefu inavyowezekana kwa visingizio vya kisheria. Sintashangaa basi, ili kufanikisha hili, kwamba serikali inashirikiana pia na baadhi ya mahakimu, aidha kwa kuwa baadhi ya mahakimu wana ushabiki wa kisiasa au kwa huwa wanakuwa wamepewa maagizo toka juu. Hii ni hatari sana kwa nchi yetu. Mahakimu jitambueni, kutumika kisiasa huwa kuna mwisho wake, na mara nyingi si mwisho mzuri.