Maneno kuntu aliyoyatoa Mh.Freeman mbowe hapo jana

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,589
20,898
Sisi kama vyama vya Upinzani tunaona hamna haki yoyote inayopatikana katika uchaguzi huu, hiyo 9% ilikuwa mpaka jana, wameendelea kupunguza watu na mpaka napozungumza labda wamebaki 6% au 7%, tuna uhakika hawatozidi 3%. Na uhakika hali ndiyo hii hii kwa vyama vyote Upinzani, kila Chama kwa nafasi yake na hakika wote wameendelea kutoa matamko kuhusiana na hali halisi ya uchaguzi huu.

Katika misingi hii ndugu Watanzania, tulilazimika Viongozi wa Chama hiki, Waheshimiwa wabunge wetu tukae tubadilishane mawazo tuendelee na uchaguzi huu au tujitoe kwenye uchaguzi huu.
Baada ya vikao ambavyo vilifanyika kwa siku nzima ya leo, ilionekana ni busara kwa Taifa na ni busara kwa Chama chetu kutobariki uchaguzi wa sampuli hizi, na sisi kuendelea, kushiriki kwa njia yoyote katika uchaguzi huu ni kuhalalisha ubatili ambao umefanywa na Rais, ubatili umefanywa na Serikali yake, ubatili uliofanywa na Chama cha Mapinduzi, ubakaji wa Demokrasia katika Taifa.

Kwa hiyo sisi kama kama Chama tumeamua hatutashiriki zaidi zoezi hili, nanatoa kama Mwenyekiti wa Chama, maelekezo kwa Viongozi na wagombea wetu wote nchi nzima, wasitishe kushiriki zoezi hili waachane na kuweka mapingamizi, hatupo tayari kubariki ubatili huu. Ujenzi wa Demokrasia ni process ni mchakato hatutajitoa katika mchakato wa ujenzi wa Demokrasia kwa kujitoa katika uchaguzi wa kuhuni kama huu.

Tunataka kumwambia Rais Magufuli, maana kauli zake mara kwa mara maelekezo yake kwa viongozi wake mara kwa mara ndiyo yanavuruga amani ya nchi yetu. Wananchi wanahasira, na wanahasira sana na wana haki ya kuwa na hasira na sisi tunawataka waendelee kuwa na hasira. Ambacho kinafanywa na Serikali ya Magufuli, sio aibu kwake yeye mwenyewe ni fedheha kwa Taifa letu, Mataifa mengine yanatuona majuha, kama tunaweza kuendesha uchaguzi wa kihuni, kijinga, kitoto kama uchaguzi unaofanyika sasa hivi.

Na bado viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali yao na wabunge wao wanaodai audacity ya kusimama na kujidai kwamba wao hakuna hata mmoja aliyeenguliwa nchi nzima wakati tunajua kuna viongozi chungumzima wa Chama cha Mapinduzi hata sifa ya kusoma na kuandika huko chini hawana. Jiji la Dar es Salaam tuna mitaa 570, tuliweka wagombea katika mitaa yote 570, jiji la Dar es salaam tumebakiziwa mitaa 24, upumbavu gani huu, Tukashiriki mitaa 24 kati ya 570 katika jiji la Dar es salaam?

Hali kama hiyo hiyo katika jiji la Mwanza, Mbeya, Arusha kwenye majiji ya Makao Makuu yote, tunaachiwa wagombea 3% tu, Chama Kikuu Cha Upinzani tunawanachama kwa mamilioni, na tunaomba hili Rais alisikie, Serikali isikie, tunawanachama kwa mamilioni ambao tunaweza kuwafikia. Kuharibu hoja na haki ya wananchi mamilioni kwa mamilioni ni kulinajisi Taifa, hili Taifa sio mali ya Chama cha Mapinduzi , hili Taifa ni mali ya Watanzania wote, wenye vyama vya siasa na wasio na vyama vya siasa.

Hawa watu wanakwenda kusimamia maisha ya watoto wetu, wanakwenda kusimamia maisha ya mama zetu, baba zetu, mijini na vijijini, legitimacy ya uongozi wao ambao wamepata kwa kubumbabumba bila kuchaguliwa na wananchi wanapata wapi legitimacy ya uongozi? Chama kinaendelea kufikiria kwa njia mbalimbali kichukue hatua gani zinazofuata. Lakini maelezo mahsusi ambayo tunawaeleza wanachama wetu, hatushiriki chaguzi hizi, wote wajitoe na wasiwatambue viongozi wowote watakaopatikana katika Serikali za vijiji, Serikali za vitongoji na Serikali za mitaa, na hiyo ni hatua ya kwanza, tusilaumiane, hatutatambua Kiongozi yoyote aliyepatikana kwa ubatili huu, hatutatoa ushirikiano wowote, na Serikali ya mtaa wowote, Serikali ya Kijiji chochote au kitongoji kwa Viongozi waliopatikana kwa unajisi huu.

Lakini Jafo, jambo serious anatoka anasema ndiyo mchezo wa kisiasa, mchezo gani wa kisiasa huu? Anasema watu wakakate rufaa, unakata rufaa kwa nani yupi mwenye nia njema? Kama uhuni na utaratibu wote wa uchaguzi huu umefanywa na wakuu wa wilaya, DSO ambao wamepelekewa appeal.

Hakuna Kiongozi yoyote wa Chama chochote cha Upinzani ambaye ana uwakilishi katika chombo chochote cha maamuzi katika mchakato mzima huu, tulilalamika tangu mwanzoni, lakini tukasema embu tuwape wenzetu benefit of doubt lakini sasa tume-prove beyond doubt, kwamba Magufuli anaogopa Demokrasia.
Tume-prove beyond doubt kwamba Chama cha Mapinduzi sasa kimekosa uhalali hakithubutu tena kuingia kwenye uchaguzi.

Kwa hiyo njia pekee iliyobakia lazima waengue watu wetu, umenunua ndege, umetamba kujenga reli, umetamba kujenga madaraja, unaogopa uchaguzi? Hii hii aibu wanaiona lakini? Wanaogopa uchaguzi na vyama ambavyo umevifunga miguu na mikono kwa miaka minne? Tunasema hatuamini tena taasisi yoyote ya kiserikali itaweza kusimamia chaguzi zilizo huru katika nchi yetu.

Wako wengine walikuwa na mawazo pengine tutake uchaguzi uanze upya, lakini huu mchakato wa uchaguzi hata ukianza upya unasimamiwa na nani? Tunasema njia pekee iliyobakia ya kujenga utengemano ni chaguzi zilizo za haki katika nchi hii, na lazima pawepo na chombo huru, kwa maana tume huru ya uchaguzi ambayo itaratibu na kusimamia uchaguzi huu. Lakini ujenzi wa Demokrasia ndani ya chama chetu utaendelea na kufanya kazi za siasa kwa nguvu kwa taratibu gani tutaelezana siku zinavyokwenda.

Ujumbe wetu kwa sasa, Chama Kikuu Cha Upinzani kimejitoa kwenye uchaguzi huu kwa 100% katika mchakato wowote unaoendelea, Viongozi wetu hawana sababu ya kuendelea na mapingamizi au rufaa,

Asanteni.
 
Attachments

  • 75285789_1366738000199937_1532059802790789120_n.jpg
    75285789_1366738000199937_1532059802790789120_n.jpg
    13.4 KB · Views: 1
What the hell? Kumbe walituacha only na kata 24 kati ya 570? Na hizo 24 wameacha wakijua tena watatubana kwenye matokeo!!!
Tamko la kujitoa lilikuwa best decision tusije tukaumizwa bure kwa Chaguzi za Mitaa
 
Mbowe aanze yeye kuonyesha demokrasia kwa kuachia kiti katika chama
 
Umenunua ndege, umetamba kujenga reli, umetamba kujenga madaraja, unaogopa uchaguzi? Hii hii aibu wanaiona lakini? Wanaogopa uchaguzi na vyama ambavyo umevifunga miguu na mikono kwa miaka minne? ..
 
Kwahyo mnasusia then?

ukija uchaguzi mwingne mnatangaza kushiriki
Mbowe ni muda muafaka kujiuzulu uenyekiti mbinu yako ya kujitoa na kususia haijawah kufanikiwa tangu enzi za Jakaya
 
Wewe unaumwa nanini na ccm yako?
 
Ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka. Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji. Tanzania imekuwa ikisifika kwa amani miaka mingi, lakini amekuja mharibifu wa amani yetu hii. Miaka minne tu madarakani kutwa nzima kubomoa misingi yote ya demokrasia. Kusiko na amani, mambo yalianza kwa uhuni kama huu huu wa kubaka demokrasia. Uamuzi wa Chadema ni wa busara sana
 
Back
Top Bottom