Maneno kugeuzwa maaana je kiswahili ni lugha maskini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno kugeuzwa maaana je kiswahili ni lugha maskini?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mpasuajipu, May 15, 2011.

 1. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kiswahili kweli ni lugha masikini, maneno mengi yanatumika kwa maana tofauti na hivyo huweza kuwachanganya watumiaji:

  Mfano:
  1. Kufika= kuwasili sehemu fulani, kufikia hamu katika tendo la ndoa,
  mf. Amekaribia kufika nyumbani.
  au Mmmh leo nataka kufika kileleni.

  2. Kutafuna= kusaga kitu kwa meno,hasa chakula
  siku hizi neno hili pia linatumika km vile kutafuna pesa za umma.
  kutafuna (ktk mapenzi) = kutembea na mwanamke. utasikia aah, yule nilisha mtafuna.

  3. Kutia= kuweka kitu au kuingiza kitu ndani ya kingine.
  neno hili pia hutumika kwa ilee, pale jogoo anapoparamia mtungi.

  na yapo maneno mengi yanayogeuzwa maana na kutumika tofauti na yalivyokusudiwa.

  je ndio kusema kwamba kiswahili hakina misamiati ya kutosha ?.
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  maneno yako mengine ni ya mtaani wewe....nenda nchi zingine tena tajiri za maneno hayo hayo unayoyasema kwa kiswahili pia yanamaanisha vile vile, ukipm ntakwambia other languages....achana na Kingoswe pia ni maskini wa maneno...
   
 3. S

  Senior Bachelor Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo ni jambo la kawaida katika lugha. Ndio maana unatakiwa ujue rejesta i.e lugha fulani kwa matumizi fulani. Hiyo ni misimu au maneno ya mtaani (slangs) ambayo yanaweza baada ya muda yakapata mashiko yakaingizwa katika lugha. Na pia sio ajabu neno moja kubeba dhana zaidi ya moja. Mf Kufika kileleni ni sahihi tu. hayo mengine ni misimu tu ambayo wanaelewa watu wa rika fulani tu.
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  we nawe mchoyo! Hadi upiemiwe, si useme hapa hapa jamani.
   
 5. K

  KASIGAZI Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo la huyu jamaa maneno yote yanayomtatiza yana uhusiano na ngono. Ana dalili za ugonjwa wa hyper-ngono-emia! Lakini kuna maneno ambayo hayatosherezi. Kuna wakati nilikuwa nafanya ukarimani, mwingereza akafululiza maneno haya "Shame, reproach, disgrase", ungekuwa wewe ungesemaje?
   
 6. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kiswahili ni lugha mbichi, viraka kibao, haiwezi kutumika kitaalamu, au viraka vinajazwa na maneno ya kiarabu, inakera sana, si japo wajaze kwa maneno ya kibantu?
   
Loading...