Maneno katika methali/misemo

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,616
7,863
Haya maneno yana maana gani kwa jinsi yalivyotumika kwenye hizi methali?

1. Kisokula, sera, nale => (Kisokula mlimwengu,sera nale)
2. Konzo => (Konzo ya maji haifumbatiki)
3. Lila, fila => (Lila na fila hazitangamani)
4. Mchama, ago, hanyeli, akauya => (Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo)
5. Mgaagaa, upwa => (Mgaagaa na upwa hali wali mkavu)
6. Shibiri, pima => (Ukipewa shibiri usichukue pima)
7. Tonga => (Tonga si tuwi)
8. Ukambaa => (Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa)
9. Mbachao, msala => (Usiache mbachao kwa msala upitao)

Nakumbuka tulikuwa tunafundishwa shuleni lakini sijui kwa nini tulikuwa hatudodosi maana ya haya maneno achilia mbali maana ya kijumla ya methali yenyewe.

Karibuni tufunzane.
 
==Mchama ni mtu aliyechuchumaa ama kujikunyata mfano mtu aliyejikuntata chini ya mti ama pango kujihifadhi na mvua inayonyesha
== ago ni pango ama uvungu wa mti uliopinda na kuinama kuacha nafasi ya kiumbe kama mnyama ama mtu kukaa chini ake
==hanyeli maana yake hanyei (rejea msemo maarufu wa JKT wa kunyea kambi)
==akauya (sahihi ni akawia) maana yake akarejea, ama akarudi tena
>> maana ya jumla ya methali hii ni kuwa mtu aliyapata hifadhi chini ya pango ama mti wakati wa shida hajisaidii (kunya) hapo kwani huenda siku moja akapata shida kama ileile na kulazimika kukimbilia tena pale kwa hifadhi

== mgaagaani mtu anayetangatanga amab kujigalagaza mfano wa watu wanaojigalagaza mchangani wakiwa ufukweni mwa bahari kwa mapumziko
==upwa (rejea kpwa na kujaa kwa maji) ni hali ya maji ya bahari yanapoondoka na kuacha ufukwe ukiwa na mchanga pekee bila maji
>> maana ya jumla ni kwamba mtu anayetangatanga ufukweni baada ya maji (bahari) kupwa hata siku moja hakosi kitoweo (hali wali mkavu) kwani kuna samaki wadogowadogo wngi huokotwa mchangani baada ya kushindwa kurudi baharini maji yanapokupwa. Hawa wagaagaa na upwa ni wengi sana pwani ya ocean road na wanaonekana kirahisi

==ukambaa ni kamba iliyotokana na gome la mti inaytumka katika shughulkama kufungia kuni. Si kamaba halisi bali ni ganda tu la mti. Baadhi ya miti ina mikambaa mizuri sana na mirefu, mfano mikomakoma. lakini bado si imara kama kamba halisi
>>maana ya jumla ya methali hii ni kwamba, hata kamba ikiwa umechakaa namna gani bado haiwezi kulinganishwa uimara wake na ukamaa

== mbacha ni mkeka ama kilago hasa kinachotumika kuswalia (kwa waislam) hivyo mbachao ni mbacha yako ama mbachayo
== msala ni mkeka ulio mzuri zaidi ukilinganisha na mbacha. Nao hutumika kwa swala kwa waislam
>>maana ya jumla ya methali hii ni kuwa usipuuze ama usiache kilago (mbacha) chako mwenyewe hata ukakipoteza kwa kuhadaika na msala mzuri usio wako (mfano usiharibu l\kilago chako kwa sababu umepata mkeka mzuri wa kuazima)

Ni hayo tu niliyoweza, yaliyobaki wajuzi zaidi watujuzu…………… nawasiliha………..
 
Asante sana AK kwa maelezo yako murua. Kwa kweli unapofahamu maana ya maneno, methali inakuwa na maana zaidi.

Kwa jinsi ulivyoyaeleza haya naamini na hayo mengine tutapanza wajuzi tu humu JF.
 
Asante mkuu kwa maelezo yako mazuri,
Ngoja tusubiri wataalam tupate majibu yaliyobaki,ingawa imechukua muda.
 
Haya maneno yana maana gani kwa jinsi yalivyotumika kwenye hizi methali?

1. Kisokula, sera, nale => (Kisokula mlimwengu,sera nale)
2. Konzo => (Konzo ya maji haifumbatiki)
3. Lila, fila => (Lila na fila hazitangamani)
4. Mchama, ago, hanyeli, akauya => (Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo)
5. Mgaagaa, upwa => (Mgaagaa na upwa hali wali mkavu)
6. Shibiri, pima => (Ukipewa shibiri usichukue pima)
7. Tonga => (Tonga si tuwi)
8. Ukambaa => (Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa)
9. Mbachao, msala => (Usiache mbachao kwa msala upitao)

Nakumbuka tulikuwa tunafundishwa shuleni lakini sijui kwa nini tulikuwa hatudodosi maana ya haya maneno achilia mbali maana ya kijumla ya methali yenyewe.

Karibuni tufunzane.

Kuna baadhi najua tafsiri zake Ila maneno mengine yananipa taabu (sikukaa Sana na babu mie uswahilini )

1: kisoliwa na Mtu , shetani atakila
2: konzo (kobwe ?, kukinga/kuchukua kitu kwenye vitanga /viganja viwili vya mkono hali ya kuwa viganja hivyo vimekuyanishwa/vimegusanishwa) la maji halifumbatiki , huwezi kuyafumbata /kuyakunyata maji kwenye viganja.
3: lila na fila ( kizuri na kibaya haviambatani/ haviendi pamoja).

6: hivi ni vipimo vya asili vya kiswahili. Nyanda, dhiraa, shibiri na Pima.
Kama nakumbuka vyema ni hivi,
Nyanda /Wanda ni kipimo cha urefu kipatiknacho kwa kutumia kidole gumba na kidole cha shahada.
Dhiraa ni urefu kutoka kiwiko (kipepsi) cha mkono hadi ncha ya kidole cha mkono huo.
Pima ni kipimo cha urefu kutoka ncha ya kidole cha mkono wa kulia hadi ncha ya kidole cha mkono wa kushoto (unanyoosha mikono yako pembeni Sio mbele ).

Shibiri/Shubiri ni urefu wa kutoka kidole gumba hadi kidole kidogo cha mwisho.
MSEMO HUO MAANA YAKE NI , ukipewa kidogo basi usichukue kikubwa /kingi.
 
Asante kwa ufafanuzi murua. Nafikiri mambo haya hayafundishwi vizuri/ipasavyo mashuleni (angalau kwa kutizama uzoefu wangu mwenyewe). Tunaishia kukariri tu.

Hapo kwenye Lila na fila. Lila ni nini hasa?/Na fila? mtu kitu
 
Sisi siku hizi hatumjui nani kasoma, na wala asosoma , mathalan ; maradhi ya R - L, Z na DH , GA mwisho wa neno yamekuwa makubwa Sana, kuchanganya na kingereza kingi, Mtu hawezi kutunga sentensi hata 5 za kiswahili au kingereza.
Walimu , waandishi wa habari , wengi wao nao wanaharibu hii lugha.
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Similar Discussions

Back
Top Bottom