Maneno katika methali/misemo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno katika methali/misemo

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by SMU, Feb 25, 2010.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,112
  Likes Received: 2,411
  Trophy Points: 280
  Haya maneno yana maana gani kwa jinsi yalivyotumika kwenye hizi methali?

  1. Kisokula, sera, nale => (Kisokula mlimwengu,sera nale)
  2. Konzo => (Konzo ya maji haifumbatiki)
  3. Lila, fila => (Lila na fila hazitangamani)
  4. Mchama, ago, hanyeli, akauya => (Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo)
  5. Mgaagaa, upwa => (Mgaagaa na upwa hali wali mkavu)
  6. Shibiri, pima => (Ukipewa shibiri usichukue pima)
  7. Tonga => (Tonga si tuwi)
  8. Ukambaa => (Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa)
  9. Mbachao, msala => (Usiache mbachao kwa msala upitao)

  Nakumbuka tulikuwa tunafundishwa shuleni lakini sijui kwa nini tulikuwa hatudodosi maana ya haya maneno achilia mbali maana ya kijumla ya methali yenyewe.

  Karibuni tufunzane.
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  4. Mchama, ago, hanyeli, akauya => (Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo)
  ==Mchama ni mtu aliyechuchumaa ama kujikunyata mfano mtu aliyejikuntata chini ya mti ama pango kujihifadhi na mvua inayonyesha
  == ago ni pango ama uvungu wa mti uliopinda na kuinama kuacha nafasi ya kiumbe kama mnyama ama mtu kukaa chini ake
  ==hanyeli maana yake hanyei (rejea msemo maarufu wa JKT wa kunyea kambi)
  ==akauya (sahihi ni akawia) maana yake akarejea, ama akarudi tena
  >> maana ya jumla ya methali hii ni kuwa mtu aliyapata hifadhi chini ya pango ama mti wakati wa shida hajisaidii (kunya) hapo kwani huenda siku moja akapata shida kama ileile na kulazimika kukimbilia tena pale kwa hifadhi

  5. Mgaagaa, upwa => (Mgaagaa na upwa hali wali mkavu)
  == mgaagaani mtu anayetangatanga amab kujigalagaza mfano wa watu wanaojigalagaza mchangani wakiwa ufukweni mwa bahari kwa mapumziko
  ==upwa (rejea kpwa na kujaa kwa maji) ni hali ya maji ya bahari yanapoondoka na kuacha ufukwe ukiwa na mchanga pekee bila maji
  >> maana ya jumla ni kwamba mtu anayetangatanga ufukweni baada ya maji (bahari) kupwa hata siku moja hakosi kitoweo (hali wali mkavu) kwani kuna samaki wadogowadogo wngi huokotwa mchangani baada ya kushindwa kurudi baharini maji yanapokupwa. Hawa wagaagaa na upwa ni wengi sana pwani ya ocean road na wanaonekana kirahisi

  8. Ukambaa => (Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa)
  ==ukambaa ni kamba iliyotokana na gome la mti inaytumka katika shughulkama kufungia kuni. Si kamaba halisi bali ni ganda tu la mti. Baadhi ya miti ina mikambaa mizuri sana na mirefu, mfano mikomakoma. lakini bado si imara kama kamba halisi
  >>maana ya jumla ya methali hii ni kwamba, hata kamba ikiwa umechakaa namna gani bado haiwezi kulinganishwa uimara wake na ukamaa

  9. Mbachao, msala => (Usiache mbachao kwa msala upitao)
  == mbacha ni mkeka ama kilago hasa kinachotumika kuswalia (kwa waislam) hivyo mbachao ni mbacha yako ama mbachayo
  == msala ni mkeka ulio mzuri zaidi ukilinganisha na mbacha. Nao hutumika kwa swala kwa waislam
  >>maana ya jumla ya methali hii ni kuwa usipuuze ama usiache kilago (mbacha) chako mwenyewe hata ukakipoteza kwa kuhadaika na msala mzuri usio wako (mfano usiharibu l\kilago chako kwa sababu umepata mkeka mzuri wa kuazima)

  Ni hayo tu niliyoweza, yaliyobaki wajuzi zaidi watujuzu…………… nawasiliha………..
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,112
  Likes Received: 2,411
  Trophy Points: 280
  Asante sana AK kwa maelezo yako murua. Kwa kweli unapofahamu maana ya maneno, methali inakuwa na maana zaidi.

  Kwa jinsi ulivyoyaeleza haya naamini na hayo mengine tutapanza wajuzi tu humu JF.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...