Maneno haya yanayoelezea wakati yananichanganya

Nancheto

Member
Mar 4, 2011
25
4
Ndugu waswahili wenzangu maneno haya yanayohusu wakati nashindwa kuyatumia ipasavyo na mwenye uelewa wa kutosha naomba anielimishe;
alfajiri,asubuhi,mchana,adhuhuri,jioni,alasiri na usiku.kwa mfano nawezaje kutofautisha kati ya alfajiri na asubuhi au mchana na adhuhuri n.k.
 
Alfajiri ni kuanzia saa 9 alfajiri hadi saa 11 alfajiri na asubuhi ni kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 5.59 asubuhi. Mengine wenzangu watakusaidia
 
Adhuhur ni sehemu ndogo ya mchana ambayo ni mida kati ya saa saba na nane, na mchana ni kuanzia saa sita mcha hadi saa kumi,

Alaasiri ni mwanzo wa jioni yani saa kumi hadi kumi namoja,na maghrib ni mwanzo wa usiku,pale jua linapo zama,mida ya kumi na mbili hadi saa moja.
 
alfajiri ni kuanzia saa 9 usiku hadi 11, na kuanzia 12 ni asbh, kuanzia 6 kamili ni mchana AMBAO huendelea hadi 10.ADHUHURI IMO NDANI YA MCHANA, SAA 7 NI ADHUHURI,NA ALAASIRI NI MWISHO WA MCHANA YAANI SAA 10, Na kuanzia 11 ni jioni na magharibi inaanza kuzama kwa jua hadi saa 1 usiku.
 
Back
Top Bottom