Maneno haya yalinigusa mno japo yalikuwa hayanilengi mimi!

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Yamkini yalikuwa kwa ajiri yako wewe, unayesoma ujumbe huu.

Au kama siyo wewe basi rafiki yako, na kama siyo rafiki yako basi ni ndugu yako.

Na kama hao wote hayawahusu ila kuna kitu utajifunza.

Ili ukawafunze wengine.

UJUMBE HUU NI KWA AJIRI YA WANAWAKE

Ila kwa kuwa hakuna mwanamke bila mwanaume, basi hata mwanaume unamhusu pia.

Kwanza kabisa fahamu msemo huu.

"Ukikuta pesa njiani, iokote, hata kama huihitaji, yamkini mbeleni ukakutana na omba omba, ukampatia akasema ubarikiwe, na mwisho ukajikuta na wewe unapata unachotaka kutokana na asante uliyopata kwa yule uliyemsaidia"

Basi na mimi niliyachukua haya kama yalivyo.

Huyo mtu mwenye hekima na busara nyingi Alisema kwamba wanawake walioko FORM 6 na wale walioko VYUO.

Hususani wale wa miaka 20-27

Huwa wanafanya makosa makubwa sana.

Nilipomuuliza ni makosa gani, alinitazama usoni na kuniambia

Wanapoteza FURSA kwa watu waliokuwa SERIOUS kujenga nao malengo ya kimaisha, kwa ajiri ya baadae.

Na wanakuja kuijutia nafasi hiyo baada ya kufikia umri wa miaka 28-30.

Aliniambia, wanawake wengi wenye miaka 20-27, huwa WANAMTAZAMA MWANAUME hali aliyonayo kwa sasa.

Wakishaona hana pesa, hana kazi ya uhakika, hana maisha.

Alisema kwamba SIWATUKANI wanawake, ila ukweli ni kwamba, vijana wengi wa kike HAWANA VISION-(maono)

Ndio maana wanashindwa kuwatambua WANAUME WENYE MAONO.
.
Ndio maana wanapoteza NAFASI kwa wanaume WENYE VISION na kuwakimbilia wale wenye TELEVISION

Kwa sababu mtu mwenye maono ni rahisi kumtambua mwenye MAONO mwenzake.

Lakini asiye na MAONO ni ngumu kumtambua mwenye MAONO (the law of attraction).

Hii ndiyo sababu, wengi wanapoteza wanaume wa MAANA kwa sababu ya wanaume wenye MALI.
.
Wanampotezea hata kama ALIDHAMIRIA KWELI KUWEKA NAYE MALENGO

Na kwa kuwa wanawake ni wengi, basi, mwanaume huyo hata kama alimpenda kwa dhati, huamua kuupa TAABU moyo kwa kwenda kutafuta mwingine.

Kwa sababu wahenga walisema mwenye mbili havai moja Basi hivyo ndivyo wanavyofanya.

Kimbembe kinakuja pale mwanamke huyo ALIYECHEZEA NAFASI Miaka kadhaa iliyopita

Anapofikia miaka ya 28-30+ anaanza kupata stress.

Alinisisitizia kwamba katika miaka 20-27 hakuna mwanamke YEYOTE asiyetokewa na mtu ambaye yuko serious kujenga naye malengo, maana hicho kipindi ni kipindi cha kustawi na kunawili, ni lazima ua likichanua wadudu wanavutiwa

Ila bahati mbaya, kipindi hicho, wanawake wengi HUANGALIA wale wenye PESA TU ambao hata hawana malengo nao.

Kipindi cha 20-27, wanawake wengi wanaharibu FUTURE zao kwa kutembea na MATAJIRI, MABOSS na VIJANA WENYE HELA kwa ajiri ya starehe tu.

Mwisho wa siku wengi huishia kutoa mimba, na kutumikishwa na wenye hela wasio na UCHUNGU na UTU wao.

Alipofikia hapo, nilinyamanza kimya nikawa namsikiliza.

Akaniuliza swali, unajua ni kwanini mwanamke anapata tabu miaka ya 20-30+?

Nilimjibu Sijui (ili aendelee)

Basi, akaniambia ni kwa sababu anayeweza kumwoa mwanamke wa miaka 28-30 anamhitaji mwanaume mwenye miaka kuanzia 33,35, au zaidi

Na bahati mbaya wanaume wengi katika miaka hiyo ya 30+ wanakuwa tayari wana familia zao, yaani wameshaoa.

Akaniambia unajua Wanachokifanya inapotokea hali hiyo?

Wengi huamua kuendelea kudate na waume za watu

Na wengine huamua kuzalia nyumbani, ili kumaliza ubishi

Na wengine huamua kujikunyata tu na kuwa wanyonge wakisubiri MUUJIZA kutoka kwa Mungu.

Na wengine huamua kuwa wahuni TOTALLY.

Nilipoyatafakari hayo nikawa sina cha kuongezea.

Sijui kwa upande wako unayaonaje hayo, je yana ukweli ndani yake?

"LIVE A GREAT LIFE"
 
Kuna mmoja anaishi na jamaa yake, wana mtoto mmoja sasa wa mwaka mmoja Kama sikosei. Jamaa alikuwa vizuri lakini Mambo yakaanza kubadilika, basi demu (anajisemea, siwezi kuolewa Mimi na Huyu jamaa wala siji kusex naye tena!).

Jamaa anatuambia kijiweni, baada ya kupata na kuthibitisha taarifa hizi anatarajia kutafuta binti mwingine mbichi kabisa afunge naye ndoa mchezo uishe. Huyu anayeishi naye Yuko around 26/27 years. Yuko busy kuwasiliana ex wake ambaye tayari ni mume wa mtu!

Uliyosema yote ni kweli tupu. Huwa wanadhani wataendelea kuwa wabichi daima!
 
Ingefanyika x-change....mwanaume mwenye Mali aoe mwanamwali hohehahe na mwanaume mgonga urimbo aoe mlibwende mwenye nazo.
Vilio vyote tunavyoviona visingetokea...kila familia ingeishi maisha classic.
Hiyo ni nzuri sema kutegemeana ndo kingekuwa kipengele kingine yaani nani aingie shamba na nani ofisini.
Wacha tu tutegemeane.
 
Kipindi cha 20-27, wanawake wengi wanaharibu FUTURE zao kwa kutembea na MATAJIRI, MABOSS na VIJANA WENYE HELA kwa ajiri ya starehe tu.

Mwisho wa siku wengi huishia kutoa mimba, na kutumikishwa na wenye hela wasio na UCHUNGU na UTU wao.

Akaniuliza swali, unajua ni kwanini mwanamke anapata tabu miaka ya 20-30+?
Kweli kabisa. Nikiwa UDSM kulikuwan na msichana nilimpenda sana. Alikuwa mzuri n bonge ya figure, na from a well off family. Tatizo tulikuwa mwaka mmoja na sikuwa natoka familia tajiri. Sasa yeye alikuwa anapenda company ya wasichana wenzake ambao walikuwa ni watoto wa matajiri kama yeye, na hivyo kuwa na uhusiano na vijana walio na fedha pale chuoni, tukiwaita ma-Hillsider.

Walikuwa wanatuita watu kama sisi infantria, yaani "infantryman" au askari wa miguu, kwa kuwa hatukuwa hata na magari. Hillsiders walitanua na magari ya baba au ndugu zao mara nyingine, na weekend lazima kwenda disco na kutanua.

Hawa wasichana walikuwa na mentality kwamba utaolewaje na mtu ambae mtaanza kununua pamoja vikombe vya chai?

Nilikutana tena na msichana huyo ten years later baada ya kumaliza chuo, mie sijaoa na yeye bado hajaolewa, ila ameanza kuisha. Akaanza kunikumbusha nilivyompenda eti ananiuliza do you still love me? Nikamwambia yes I do, but now as my big sister from UDSM!

Alikuja akaolewa olewa na wanaume walioacha wake zao na bado yakamshinda mara mbili, na hadi leo yupo single, a very frustrated mother (Frumo)
 
Ndo maisha yalivyo yaani wao hawatazami future yao wao wanao walipo ndio wataendelea kuwa.
 
Ha ha ha ha ha ha we jamaa unakipackage cha skills and words. Eti Frumo
 
Kuna mmoja hapa namwangalia kisha nabaki kucheka, katoka UDSM mwaka jana anasema yeye kuolewa mpaka awe na gari. Yupo mtaa hata kazi hana, bado anaishi katika zile ndoto za kishuleshule. Nimempa muda mpaka December akiendelea na upuuzi wake huo namuachia Mungu.
 
Back
Top Bottom