Maneno haya ni ya Kiswahili?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Maneno haya ni ya Kiswahili?
Wakuu, maneno yafuatayo hutumika sana katika mazungumzo ya kiswahili.
Je matumizi ya maneno haya na maana zake humaanisha kuwa maneno haya ni ya kiswahili?
Mdosi,
Ngangari,
Vigogo,
Mkenge,
Changudoa,
Dingi,
Ng'atuka,
Kipute,
Ndinga,
Kobis,
Kibosile,
 
Maneno haya ni ya Kiswahili?
Wakuu, maneno yafuatayo hutumika sana katika mazungumzo ya kiswahili.
Je matumizi ya maneno haya na maana zake humaanisha kuwa maneno haya ni ya kiswahili?
Mdosi,
Ngangari,
Vigogo,
Mkenge,
Changudoa,
Dingi,
Ng'atuka,
Kipute,
Ndinga,
Kobis,
Kibosile,
kwani yanatumika katika lugha gani? na je yanapotumika huleta maana?
 
Lakini unayaelewa yamaanisha nini??

Maneno mengine huwa yanaanzia uswahili au mitaani bila kwenda kwenye baraza la kiswahili. Hata kama yanatumika katika lugha ya kiswahili haimaanishi ni maneno ya kiswahili, Pia maneno mengine ni ya kiswahili lakini yanatumika kwa maana zingine tofauti. kwa mfano,mzuka

Siyaoni kwenye kamusi ya kiswahili ya mwaka 1973 mkuu,
Katika kamusi ya mwaka huo hayapo lakini yamesanifiwa hivi karibuni na kutumika katika lugha ya kiswahili kama vile:
Kasheshe, ngangari, ngunguri, n.k.
 
Maneno mengine huwa yanaanzia uswahili au mitaani bila kwenda kwenye baraza la kiswahili. Hata kama yanatumika katika lugha ya kiswahili haimaanishi ni maneno ya kiswahili, Pia maneno mengine ni ya kiswahili lakini yanatumika kwa maana zingine tofauti. kwa mfano,mzuka


Katika kamusi ya mwaka huo hayapo lakini yamesanifiwa hivi karibuni na kutumika katika lugha ya kiswahili kama vile:
Kasheshe, ngangari, ngunguri, n.k.
GM7,
Maelezo yako ni makini sana.
Baadaye nitauliza swali dogo tu.
 
Nafikiri kuwa lugha inakuwa kutokana na jinsi inavyotumika katika jamii husika kwa kuzaa maneno mengi ambayo yanakuwa yanaeleweka kwa wenye lugha wenyewe
 
Maneno haya ni ya Kiswahili?
Wakuu, maneno yafuatayo hutumika sana katika mazungumzo ya kiswahili.
Je matumizi ya maneno haya na maana zake humaanisha kuwa maneno haya ni ya kiswahili?
Mdosi,
Ngangari,
Vigogo,
Mkenge,
Changudoa,
Dingi,
Ng'atuka,
Kipute,
Ndinga,
Kobis,
Kibosile,

Jibu lake ni ndio, hayo ni maneno ya Kiswahili kisicho rasmi.

Mdosi = Watu wenye asili ya Asia (Wahindi) na maana nyingine neno ili linamaana ya mteja au mwenye fedha ambaye unataka kufaya naye bishara.

Ngangari = Ngangari ni neno linalo tumika kwenye siasa (CUF) lina asili ya neno la Kindengereko, na maana yake haswa ni kuwa na msimamo.

Vigogo = Ni mtu mwenye fedha na madaraka

Mkenge = Kukosea jambo wakati wa kujitia unajuwa na watu wakakudanganya au kutarajia kupata jambo fulani na ukapata sivyo ulivyo tegeme.

Changudoa = Ni aina ya samaki wadogo wadogo wenye madoa ubavuni, pia mwanzoni lilitumika kama watoto wa mitaani wenye mazoea ya kwenda feri kupaa samaki, na baadhi yao (watoto wa kike) walipopata umri wa barehe wakaingia mitaa ya Ohio kufanya ukahaba ndipo neno changudoa lilopobeba maana ya umalaya.

Dingi = Linatokana na neno la kiingereza dinghy au life boat, Waswahili wakalipa maana nyingine yaani Baba, lakini kwa maana ya baba mwenye kufuata mambo ya kizamani bila kupima... (dinghy au life boat zinabebwa kwenye meli bila kujuwa wapi meli inaelekea) baadaye sana likazoeleka na kupata maana ya Baba tu bila maana mbaya.

Ng'atuka = Linatokana na neno la Kizanaki, yani kuachia madaraka au kuondoka
Kipute = Kucheza mpira... na haswa ule wa chandimu au mpira wa makaratasi, neno ili linatumia haswa na watoto mitaani.

Ndinga = Neno ili linatokana na neno Karandinga, gari la kubebea wafungwa magerezani.

Kobis = Neno haswa ni kula Kobis yaani kukaa kimya bila kuongea... Kuuchuna.

Kibosile = huyu ni Boss mdogo

Hope wapo watakao changia na kurekebisha nilipo kosea Insha'Allah.
 
Dingi = Linatokana na neno la kiingereza dinghy au life boat, Waswahili wakalipa maana nyingine yaani Baba, lakini kwa maana ya baba mwenye kufuata mambo ya kizamani bila kupima... (dinghy au life boat zinabebwa kwenye meli bila kujuwa wapi meli inaelekea) baadaye sana likazoeleka na kupata maana ya Baba tu bila maana mbaya.
Ndo maana sipendi kukosekana Jamvini, asante mkuu, sikuwahi kujua jambo hilo kama linatokana na DINGHY, wewe nakuheshimu.

kwa mawazo yangu katika muktadha huo wa Lugha hii maridhawa ya kiswahili , ni kua ukuaji wa lugha zote duniani iwe kipogoro,kingoni , kigogo ama kinyakyusa hutegemea na matukio ya maisha ya watu kiuchumi na kijamii , pia muingiliano wa watu wa tamaduni na historia mbalimbali. hivyo jamii ikiyakubali maneno hayo moja kwa moja huingizwa kwenye kamusi na matumizi yake huanza kua rasmi.
 
Sijui mkuu ameishi wapi, lakini kila lunga ina slang zake....hizo ni za kiswahili....
 
Naongezea neno SOLEMBA.
Ili neno lishawahi kuelezewa maana yake.

Lilitokana na nyimbo ya marehemu Nico Zengekala.

Ni sawa na mtu kuambiwa "Kaachwa kwenye mataa"

Kupewe ahadi kisha yule uliye mtegemea kuwepo kwenye ahadi hakutokea.

Kupewa ahadi ya uwongo
 
matawi ya juu
ATM
kujiachia
usipime
adabu tupu
Kubambia
mwana
Majita
mwake
michosho
mkwanja
kichaa wangu
kumchomolea
kumpa sound
Unanitega unanitaka
manjemanje
kupiga mkeka
kutia timu
manjemanje
kumdakisha
Nyomi
Shalo tina tina
aminia
Mdosho
Kama kawa
full chaja
serengeti girls/boy
kicheche Haya kama kuna mtu anaweza kunitafsiria haya maneno mimi siyajuwi kwa kiswahili maana yake asanteni
 
matawi ya juu: mtu wa kipato cha juu au kuwa na cheo

ATM: Hili neno ni kifupi cha Automated Teller Machine; Mashine inayo toa fedha na mara nyingi ukaa nje ya baadhi ya benki au Super market kwa ajili ya kutolea fedha na utumia kadi. Vile vile kwa lugha ya mtaani linatumika haswa kwa wanawake kuwaita wanaume wenye kuwaonga. Pia neno lingine ni (Buzi au kuchuna buzi)

kujiachia: Kwa kiswahili fasaha ni kuwa mzembe, kukaa bila ya kufanyakazi;

usipime: Kwa kiswahili cha mtaani ili neno lina maana ya usijaribu

adabu tupu: Kuwa na nidhamu

Kubambia: ......

mwana: Mtoto wa..., kwa lugha ya mitaani linatumika kwa watu ambao ni maswahiba (marafiki) tena wenye umri unao fanana.

Majita: Kabila linalopatikana Musoma (Jita... Mjita au Wajita). Kwa lugha ya mtaani ni Askari police au askari jeshi.

mwake: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni kitu kizuri au kupatia jambo.

michosho: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni mtu mwenye maneno ya kuchosha, mtu asiye makini

mkwanja: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni kuwa na uwezo wa kifedha, Pesa

kichaa wangu: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni rafiki yangu.

kumchomolea: kumkatalia.

kumpa sound: kumwongelesha mtu kwa ajili ya kupata kitu. lakini kwa njia ya uwongo.

Unanitega unanitaka: Haya ni maneno mawili tofauti, na mara nyingi yanaandikwa hivi; Unanitega au unanitaka, na utumiwa na wanawake kuwauliza wanaume pale wanapotongozwa. Wakimaanisha kuwa 'unanitaka kwa ukweli au unaniongopea'

manjemanje:
Sina uhakika na hili neno, lakini kama una maanisha Manjee, kwa kiswahili chamtaani maana yake ni chakula

kupiga mkeka: Ni neno lenye kutumikwa kwa wanao kwenda Kusali msikitini, maana nyngine utumika mpirani wakimaanisha kusakata kabumbu kwa kutoleana pasi maridhawa.

kutia timu: maana yake ni kufuatilia jambo, kuingia sehemu bila kutegemewa au kualikwa.

manjemanje: Angalia hapo juu.

kumdakisha: Kumpa mtu kitu, kama vile pesa.

Nyomi: Kujaa na mara nyingi ili neno linatumika kwenye mabasi ya abiria. Au kwenye viwanja vya michezo (Mpira n.k)

Shalo tina tina: ....

aminia: Maana yake ni ...ndio ivyo ivyo... na mara nyingi utawasikia wakisema ...aminia babake.

Mdosho: Mwanamke mrembo au msichana, ili neno limefupishwa kutoka neno Kidosho.

Kama kawa:
Kama kawaida.

full chaja: ....

serengeti girls/boy:
Wavulana/Wasichana wenye kutembe na wanaume/wanawake wenye umri mkubwa.

kicheche
: Mtu mwenye kupenda ngono na haswa linatumika kwa wavulana na wasichana wenye umri mdogo

Kama kutakuwa na makosa wapo wataalam watasahihisha.
 
Back
Top Bottom