Maneno haya Jenerali kuhusu katiba nimeyapenda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno haya Jenerali kuhusu katiba nimeyapenda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIM KARDASH, May 4, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mwanazuoni Jenerali Ulimwengu anawaasa wanasiasa anasema hivi...  Yapo mambo yanayowasumbua wanasiasa, ndani ya chama tawala na ndani ya vyama vya upinzani. Haya ni yale ya kiutawala zaidi ambayo ni tume huru ya uchaguzi; utaratibu wa uchaguzi; viwango vya asilimia katika uchaguzi; utaratibu wa uchaguzi; madaraka ya Rais; madaraka ya Bunge; kuwapo kwa waziri mkuu au la, na madaraka yake; uwakilishi wa uwiano (PR); ukomo wa mihula ya uongozi, na mambo mengine madogo madogo kama hayo.

  Haya yote ni muhimu lakini hayana uzito kama ule ninaouona katika maeneo mengine mfano Kuwapo kwa Muungano na mgawanyo wa mamlaka na rasilimali baina ya Tanganyika na Zanzibar; mamlaka juu ya rasilimali za nchi kwa ujumla (ardhi, madini, maji, misitu); ugatuzi na mamlaka ya serikali za mitaa na mgawanyo wa madaraka baina ya serikali hizi na serikali kuu; mgawanyo wa rasilimali baina ya wakulima na wafugaji; utamaduni na lugha za asili mkabala na Kiswahili na Kiingereza; mfumo wa elimu utakaojenga Utanzania, na kadhalika.


  "Narudia kusema kwamba tusifanye mambo kwa haraka kwani hatuna tunakoenda. Tupo hapa, na tunataraji kuwa hapa kwa miaka milioni ijayo, kama si zaidi. Kwa nini tunafanya mambo kama vile tuko transit tukienda mahali pengine?"- Jenerali Ulimwengu
   
 2. k

  kubane Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  general z r8 nd muungano plus hw we share th national cake ar sensitive matters 2 4rm part of th constitution.
   
 3. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jenerali ulimwengu kichwa halafu si mnafiki,ni bonge la hazina lakini serikali haitaki kumtumia,akifa tutajutia.anajua mambo mengi sana huyu mtu
   
Loading...