Rodwell mTZ
JF-Expert Member
- Nov 16, 2012
- 1,308
- 1,423
Wabongo bana,hapa kazi tu,ilikuwa ni slogan ya JPM kwenye kampeni zake wakati wa kujinadi kuelekea uchaguzi mkuu,ikawaje wakaandija slogan hiyo mpaka kwenye ndege?
Serikali ifute maneno ya "hapa kazi tu" kwenye ndege zetu na badala yake ziandikwe jumbe za kutangaza nchi yetu.
Ndege yetu ikitua nje hakuna anaejua maana ya hiyo mineno. Hata kama ni safari za ndani ziwekwe jumbe nzuri na zenye kutangaza taifa letu.
Hayo ni mawazo yangu.
'Hapa kazi tu 'ataelewa nani kama ndege ipo china ?
Wenzetu wanaweka slogans zinaeleweka dunia nzima ndege inapokwenda
Quantas the spirit of Australia
Youre the reason we fly
Slogans zinatakiwa zieleweke na kila anayezosoma
Tukianza kufundishana grammar tutaelewana kweli ??Youre the reason we fly ni lugha gani! ‘Youre’ hata sielewi ni neno gani maana hata hilo tangazo kwenye hiyo ndege sijui nani angeelewa!
Tukianza kufundishana grammar tutaelewana kweli ??
You're the reason we fly, nilitaka kumaanisha hivyo bahati mbaya autospell haikuwa upande nilioutaka
Unaelewa hata hiyo ni slogan ya nchi gani? Niandike kiswahili wakati wenyewe wameandika hivyo?Wewe andika kiswahili tu, sasa hapo umeeleweka kitu gani? Kiingereza cha shule za kata ni shida bwana mdogo!
Kwa kifupi ni kwamba maneno hayo hayana kabisa maana yoyote ile katika ulimwengu wa kujitangaza biashara. Ni kama vile misemo ile iliyopo kwenye khanga ama nyimbo za taarabu, yenye kurusha vijembe kwa watu wengine kwa nia ya kuwananga.Serikali ifute maneno ya "hapa kazi tu" kwenye ndege zetu na badala yake ziandikwe jumbe za kutangaza nchi yetu.
Ndege yetu ikitua nje hakuna anaejua maana ya hiyo mineno. Hata kama ni safari za ndani ziwekwe jumbe nzuri na zenye kutangaza taifa letu.
Hayo ni mawazo yangu.
Kwahiyo hapo umekaa unahisi ni zako peke yako na Sabaya tu?Leo hii zimekuwa ndege zenu? Si mlikuwa mnasema tutashitakiwa MIGA na mkawa mnashangilia zikikamatwa?