Maneno gani ya Kiingereza ulikuja kujua baadaye yanasomwaje?

Wanaosema hii lugha ilikuja na meli hawakukosea. Kuna maneno ya Kiingereza nilikuwa nayatamka vizivyo kwa kipindi kireeefu. Nimekuja gundua baadaye nikajiona kilaza sana. Haya baadhi ya maneno ambayo nilifahamu baadae matamshi yake sahihi:

1. Tier - nilikuwa nafananisha matamshi na Tyre

2. Sandals

3. Apprentice

4. Agent - nilikuwa nafananisha matamshi na Urgent

Kama kuna maneno na wewe yanakusumbua, njol tutoane ujinga
dah mimi inaonekana kiingereza nimekijua mapema hata maneno ya hivyo nimeyasahau
 
Muda mfupi uliopita (saa 1 asubuhi ya leo hii) nimemsikia mtangazaji mmoja wa Radio One akitamka neno "Windsor" ndivyo sivyo.

Kwamba:
"Mume wa Malkia Elizabeth II, Philip, jana (Jumamosi) amepigiwa mizinga.... toka katika manowari zote za kijeshi za Uingereza kufuatia kifo chake siku ya Ijumaa katika makazi yake kule "Windso".

Windsor : inatamkwa " Winzah"
 
Nawakilisha Saint Kayumba hapa, hamna neno hata moja linalonisumbua, ninachofahamu mimi ni kuwa kila eneo katika dunia hii lina namna yake ya matamshi ya maneno ya Kiingereza
 
Id yangu watu wanaita “George” wakati haliitwi hivyo kuna utofauti hilo jina sio English

Jorge- inatamkwa “Hor-heh” kwa accent
 
Back
Top Bottom