Maneno gani ya dharua uliambiwa yakakuumiza sana

Karma is a bitch
Kulikuwa na shida ya maji mkoa mzima.so maji yakiwa ya kununua dumu mia tano hapo zamani.visima vikiwa adimu
My sister alikua sekondari sasa akirudi inabidi akatafute maji japo ndoo kubwa moja kwa kufulia uniform na anabakisha ndoo ndogo moja ya kuosha asubuhi .siku hiyo akakosa hata maji ya kisima.kuna ndugu mmoja alinunua maji sababu alikua na ajira.alipopata maji ya kuoga akataka kuyamwaga yaliyobaki.Dada akamuwahi "kaka flani usimwage hayo maji kama huyataki nayaomba"

Yule kaka akamwangalia kwa dharau akamjibu "haya maji si bora niyamwage au nimpe mbwa kuliko wewe"
Halafu Ilikua mbele ya member wengine wa familia mchanganyiko..


Sasa hivi huyo aliejibu kwa dharau anapuyanga huko vijijini mlevi hafai.huyo mdada yuko mjini na maisha yake kayapata.
 
kuna mzee mmoja alikua hataki nisitembee na binti yake.Sasa cku moja alinifata kijiweni mbele ya washkaji ngoja ni mnukuu "ctaki ufala wako kwangu unataka mwanangu aje azae mtoto ana mashavu kama mtungi" nilijickia vibaya sana kwa kudhalilishwa kule mbele ya watu nikajiondokea kwenda gheto kujiangalia kwenye kioo hayo mashavu kama mtungi lakin cku yaona.

Ila mapenz ndo kama aliyachochea binti alidata kupita maelezo.
 
Mimi aliniomba 100K aongeze kwenye kodi wakati me mwenyewe kodi jau enzi za chuo hizo nikamwambia asubiri nipate boom. Akasema mwanaume wa kutegemea boom nae mwanaume sasa

Kitu gani cha dharau alichowahi kukwambia babe wako alipokuomba hela ukasema huna?
Nyambafuuuuu na mlipe mikopo yenu....baada boom iwasaidie msome vizuri mnaaza kutafta vischana na kuongaa,mkiaza kudaiwa mnalia liaaa
 
"mwanaume mzima unaishia kwenu ,unazidiwa na mdogo wangu wa shue ya msingi amepanga ":nilifungasha vilago siku hyo hyo siku ya kwanza nililala nje siku ya 6 nikachukua getho la buku 5 saiv getho nalipia 150k per month ila ile kauli inaniuma kila kukicha
 
Nakumbuka mwaka 2014 mwanzoni nilienda kufanya interview pale ukonga. Interview ilikua ni ya Jeshi la Zimamoto. Sasa sisi tulikua wengi sana hivyo ili zoezi liende kasi ilibidi wao mainterviewer wajigawe kwenye magroup matatu mule bwaloni.
Ilipofika zamu yangu niliingia na nikaangukia kwenye meza moja yenye wasaili watatu akiwepo mmama mmoja hivi mtu mzima na miwani yake.
Akaniambia nikae. Baada ya kuka akaamza kuniuliza jin langu nani, naishi wapi na shughuli yangu kwa wakati ule ilikua ni nini. Baada ya kumjibu hivyo, ilionekana kama namdanganya (nahisi alinifananisha na mtu mwingine) , na nilipojitetea zaidi akanambia kwa ukali, "shika vyeti vyako uondoke kwanza mdomo wako unanuka"
Kwakweli iliniuma sana hasa ukizingatia nilitokea mwanza kwa ajili ya hiyo interview.

Nilichojifunza baada ya miezi kadhaa ni kutolalamika sana kwani kila kitu kina sababu na Mungu mwenyewe ndie ajuae. Nadhani nilipo hapa ni pazuri zaidi kuliko nafasi niliyokua naitafuta Zimamoto.
Kuna jemba zingine midomo Kama dampo, unatamani umwambiye, hivyo huyo mama alifikisha ujumbe kwako, kunuka mdomo ni balaa hata kama unakula waweza tapika.piga mswaki tumia Listerine
 
Kuna jemba zingine midomo Kama dampo, unatamani umwambiye, hivyo huyo mama alifikisha ujumbe kwako, kunuka mdomo ni balaa hata kama unakula waweza tapika.piga mswaki tumia Listerine
Kweli mkuu. Mi sijui kama wangu unanuka na sijawahi kuambiwa na yeyote mwingine zaidi ya huyo mama. Lakini ntajitahidi kufuata ushauri wako inawezekana watu wananivumilia tu
 
Back
Top Bottom