Maneno 21 kutoka kwa Baba kwenda kwa mtoto wakiume aliye katika mahusiano.

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,929
2,000
1. Kijana wangu, kama unafanya matumizi kwa msichana ambaye hakuulizi kama umeweka akiba au umefungua mradi, na anaendelea kufurahia matumizi, usimuoe.

2. Kijana wangu, Mwanamke anaweza kuwa mke mzuri kwako, mwingine anaweza kuwa mama mzuri wa watoto wako ila kama utapata mwanamke anakuwa kama mama kwako, kwa watoto na familia yako, tafadhali usimwache aondoke

3. Kijana wangu, mke wako asiwe kazi yake ni jikoni tu, Wapi tumiambiwa kazi ya mke ni jikini tu. Katika miaka yetu tulikuwa na mashamba, ambayo tulikuwa tukilima kwa pamoja na ndio ilikuwa ofisi yetu.

4. Kijana wangu, Kama nikikuambia wewe ndiye kiongozi wa nyumba, simaanishi uangalie ukubwa wa mfuko wako, namaanisha uwe unaangalia sura ya mke wako kama anatabasabu

5. Kijana wangu, Kama unaitaji maisha marefu. Acha mke wako awe in-charge wa mshahara wako, itakuwa ngumu kwa yeye kufanya matumizi fika akitambua kuna mahitaji nyumbani na ya kulipa bills. Kama utayafanya wewe, atakuwa anakuuliza mara kwa mara na pengine mahitaji ambayo yatakuwa tayari yamefanyika

6. Kijana wangu, Usimpige mke wako, maumivu atakayo yapata katika mwili wake huwezi fananisha na jeraha atakalo kuwa nalo moyoni. Utakuwa kwenye tatizo kuishi na mwanamke aliye na majeraha moyoni.

7. Kijana wangu, sasa umeoa, kama utaishi maisha ya kibachela wakati una mke, tambua mda mfupi utakuwa single tena.

8. Kijana wangu, miaka yetu, tulikuwa na wake wengi na watoto wengi sababu tulikuwa na mashamba makubwa yenye mavuno mengi, mashamba ya kulima kipindi hichi mtu kuwa nayo makubwa nadra sana, kwa hiyo muweke mke wako karibu sana

9. Kijana wangu, chini ya mbuni ambao nilikutana na mama yako, kwa wakati wenu ni hoteli na migahawa, kumbuka, ule mficho tulio ufanya siku hiyo ni kila moja kumkumbatia mwenzake.

10. Kijana wangu, pindi ukianza kupata pesa nyingi, badala ya kufanya matumizi na mahawara ambao hawajui kwa ugumu upi ulizipata hizo pesa, tafadhali fanya matumizi na mwanamke ambaye anasimama na wewe miguu yote kila wakati

11. Kijana wangu, Pindi nikitupa kijiwe kidogo au kupiga kimluzi nyumbani kwa kina mama yako kipindi hicho, si kwa sababu ya sex, ni kwa sababu nilimkumbuka sana

12. Kijana wangu, pindi ukisema mke wako amabadilika, kuna uwezekano wa kitu fula unafanya, tafadhali acha haraka sana.

13. Kijana wangu, Mama yako alisukuma bicycle na mimi hapo zamani kabla sijamnunulia mgongo wa chura iliyopo njee pale, mwanamke yeyote ambaye hata kubaliana na wewe katika madogo muanzapo, hata enjoy utajiri wako.

14. Kijana wangu, Usimfananishe mke wako na mwanamke yeyote, na kuna njia ya wewe kujiweka na yeye hata kufananisha na mwanaume yeyote

15. Kijana wangu, Nilimkuta mama yako ni bikra na nilitoa mahari kubwa sana kwa wazazi wake, sikukatazi kama utamkuta mke wako siyo bikira kwa sababu wakati wenu na wetu ni tofauti.

16. Kijana wangu, Sikuwapeleka dada zako shule kwa sababu nilikuwa mjinga kwa kufikia kwamba mwanamke abebi jina la familia, tafadhali usifanye kosa hili, kwa aina ya wanawake wenye mafanikio nikiwaona siku hizi wamefanya jinsia ya kike kuwa juu sana.

17. Kijana wangu, Mama yako na Mimi hatufurahishwi na kila kinachotokea kwenye ndoa yako, jaribu kukabiliana nayo na sii kila mara unakuja kwetu.

18. Kijana wangu, Nilimnunulia mama yako cherehani, msaidie mke wako atimize ndoto zake kama wewe utimizapo

19. Kijana wangu, usiache kunijali mimi na mama yako, ni siri ya kuwa mzee na kuwa na watoto wa kukujali wewe pia.

20. Kijana wangu, Sali wewe na familia yako, kuna kesho ambayo uijuwi, ongea na Mungu ambaye anajua kila kitu, kila siku

21. Kijana wangu, Nimechukuwa muda mwingi kukuambia yote haya na ndoa yako haita koma kama ya mama yako na mimi, wewe utakuwa kidume.


Nimekopy kutoka Nailands
 

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
15,124
2,000
Sijasoma zote kind of boring kijana wangu kijana wangu kijana wangu...
Ila asisahau ile huduma hiyo ndo muhimu hata akiwa na bicycle bibie ataiona ni kama vogue
 

benteke

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
1,294
2,000
Sijasoma zote kind of boring kijana wangu kijana wangu kijana wangu...
Ila asisahau ile huduma hiyo ndo muhimu hata akiwa na bicycle bibie ataiona ni kama vogue

Hapo ndipo wazazi wengi wanasahaugi kuwaasa vijana wao. Mimi baba yangu nafikiri ataniambia tu......yule mzee anaweza niambia hata ....."Kijana wangu jaribu 0714, ya mkeo, utaimarisha ndoa".
 

cerengeti

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,884
2,000
kumekucha kitchen party adi kwa wanaume

Sijasoma zote kind of boring kijana wangu kijana wangu kijana wangu...
Ila asisahau ile huduma hiyo ndo muhimu hata akiwa na bicycle bibie ataiona ni kama vogue

Asisahau kumuasa mwanaye asiwape moyo wanawake, watauumiza halafu abaki akihaha JF kuomba msaada wa namna ya kumsahau mwanamke

Maawaidha mazuri kwa yule anayeoa hata aliye katika ndoa. Zungatie na mtaishi vizuri na hao wake zetu.
 

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,929
2,000
Sijasoma zote kind of boring kijana wangu kijana wangu kijana wangu...
Ila asisahau ile huduma hiyo ndo muhimu hata akiwa na bicycle bibie ataiona ni kama vogue

Si kila mahali lazima uweke utoto, yapaswa uweke hili kwenye mind set yako. Na sii lazima ukoment.
 

Janosi

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
220
0
Sijasoma zote kind of boring kijana wangu kijana wangu kijana wangu...
Ila asisahau ile huduma hiyo ndo muhimu hata akiwa na bicycle bibie ataiona ni kama vogue

Katka wajinga ww unaongoza maneno hujirudia kulingana na ktu knachozungumziwa hvyo kutosoma ujumbe wote kunakufanya ukose vtu vya maana na unaonekana u mvivu wa kusoma punguza kujickia
 

Janosi

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
220
0
Pole kwa kutosoma maneno yote. maneno mazuri sana

inaonekana kama jamaa ulisoma bas utakuwa ulifel ngaz ya mitihan ya taifa labda uwe ulifanya magumash kwan inaonekana u mvivu wa kusoma maneno meng ambapo ndan ya maneno meng ndo utam ulikojifcha jifunze kutokuwa mvivu na kutorahcsha mambo
 

Janosi

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
220
0
Pole kwa kutosoma maneno yote. maneno mazuri sana

mjinga hufanya mzaha mpaka cku ya mwsho unapewa ujumbe unauletea mzaha upewe nn kama ungewekewa picha ziczo na maadl tena nyng ungezptia zote kuwa jitume acha uvivu jenga tabia ya kufka mwsho wa ktu unachokfanya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom