'Mandumilakuwili' CHUKUENI HATUA, Tanzania Kumekucha!!!

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187


'MANDUMILAKUWILI' TAMBUENI TANZANIA KUMEKUCHA!!!

Kweli nakubali, huu ni uchambuzi MAKINI SANA na wenye kuchokoza zaidi FIKRA za kiundani zaidi za kila mmoja wetu.

Na hata kwa MANDUMILAKUWILI wa miaka ya jana, leo, huko tuendako nao pia WANAPEWA UJUMBE MZITO MNO humu ndani. Ujumbe kuu hapa ni kwamba tangu RATIBA KUKAMILIKA ya uchaguzi mkuu 2010, japo bila mafanikio kwa wananchi, ni kwamba RAMANI YA Tanzania haipo kama ilivyokua huko nyuma tena.

Hakika ninakubaliana na huyu mwandishi kkwamba imefika mahala wananchi namna tunavyofikiri (mtu mmoja mmoja au kwa vikundi vyetu mbalimbali) imebadilika kabisa na haitokaa iwe kama huko nyuma tena!!

Imani imeanguka kupita kiasi kwa viongozi mbalimbali wa serikali na hata taasisi binafsi tuliopata kuwaamini sana sana lakini mwisho wa siku WAKATUGEUKA tena bila aibu!!

Imani kwa taasisi zetu mbalimbali iko chini kabisa sakafuni na wala hawawezi kupewa tena USHIRIKIANO STAHIKI mpaka TAnzania tukafanye MABADILIKO MAKUBWA SANA KITAASISI (Sweeping Cross-Sectional National Institutional Reforms to fully embrace the NEW political landscape - political pluralism). Hii kazi itabidi ifuatie baada ya kukamilisha kuandika KATIBA MPYA.

Nilivyo muelewa mwandishi Mwana-JF huyu ni kwamba MANDUMILAKUWILI ni sharti wasome maandishi ubaoni. Wasije wakaumbuka na hata KUDHURIKA kutokana na UKINZANO na MATAKWA YA NGUVU YA UMMA!!.

Huyu ndugu anaongeza kwamba kuna uwezekano mkubwa MANDUMILAKUWILI ni walewale, wakimtumikia bwana yule yule na kwa kutumia ulaghai na mbinu zile zile tunazofahamu sana tu (lakini kuzinyamazia katika miaka ya huko nyuma na kutufanya kumpa MDHALIMU mtaji wa kunyanyasia zaidi) LAKINI KATIKA TANZANIA MPYA iliyozaliwa upya baada ya kupitishwa kwenye TANURI KALI LA UFISADI, UDINI NA UDHALILISHAJI WAKUTUPWA kwa wananchi.

Hivyo basi, MANDUMILAKUWILI amkeni na mjue kwamba KUNA TANZANIA MPYA inayotafuta mitazamomi, miongozo mipya na NIDHAMU mpya wa mtu mmoja mmoja kati yetu.

MANDUMILAKUWILI hawanabudi kufurahia zaidi na zaidi HAKI ZAO KIDEMOKWASIA ndani ya vikundi walimojiunga PASIPO KUKALIA kwa makusudi au KUATHIRI NAZO HAKI ZA KITAASISI ambazo vikundi vyao hivyo vinavyotambulika KIKATIBA wanastahili kupewa.

Hebu changamkieni haya mawazo ya BUSARA ili mpate kuwa na UHAKIKA WA KUWA SALAMA mbele ya macho ya NGUVU YA UMMA iliozinduka usingizini leo hii nchini mwetu!!

SWALI KWA MODERATORS:

Mimi nilitamanitu kumshukuru huyu ndugu mtoa hoja hapo juu bila kuongezea neno kwa kuwa ameniridhisha mno na mawazo yake kama alivyokua akifanya Mzee Mwanakijiji kabla ya kuzaliwa kwake upya na yeye kiaina.

Sasa, inakua vipi kwenye baadha ya THREAD MNAONDOA (KU-MUTE) FURSA za kusema 'THANKS' katika baadhi ya hoja au watoa hoja fulani tu???????


---------------------------------------------------------------------

quote_icon.png
Originally Posted by Candid Scope
Baada ya uchaguzi wa mwaka huu Chama Cha Chadema kimetokea kuwa chama mashuhuri kati ya vyama vya upinzani dhidi ya CCM. Si ajabu kuona kuna mikakati ya kukisambaratisha.

Tunahitaji chama kimoja chenye nguvu cha upinzani ili kuleta changamoto katika mabadiliko yenye kuleta ndoto za maendeleo tunazotafakari kila kukicha katika taifa, vinginevyo tutaendelea na kinogaubaga. Bila ushindani wa kisiasa hakuna maendeleo ya kasi. Kwani wapenda maendeleo hawashabikii mradi kuwa na vyama vya siasa ila maendeleo ya vyama vyenye kuleta nguvu za kimapinduzi katika kuhamasisha maendeleo ya taifa kiushindani. Kumbuka huwezi kuwa mchezaji maarufu na mfungaji mzuri wa magoli bila kuwa na ushindani wa wanaogombania nafasi hiyo, na lazima upitie kipindi kigumu na hata cha kukata tamaa kwani ugumu wo wote ndio ngazi ya kufikia malengo. Wapiga kinanda wanafunzi huanza kiulani tu lakini unapofikia kiwango cha kila mkono kwenda kila upande peke yake hapo wanaanza toka jasho, kumbe ndio kipindi cha kuvuka na kuwa mpiga kinanda mzuri na mahiri.

USHAURI NASAHA: Chadema wawe makini na ye yote ambaye hata kama amekuwa wa kuaminika kwa muda mrefu iwapo mwenendo wake ni hatari kwa kukiimarisha Chama. Kuwa waangalifu na chachu mbaya inayoweza kumega chama, kwani mwenye mapenzi mema atayazungumza yanayohusu chama ndani ya chama, lakini kutoka nje ya chama ni hatari sana na haieleweki, na kabisa kuweka makundi ndani ya chama ni ufa wenye kulinganishwa na donda ndugu. Cha msingi kuwa makini na ndumilakuwili, isijetokea kulaumiana baadaye wakati nyoka anayekusudia kukuuma unaona movement zake nafasi ya kukwepa inakuruhusu. Leo amevuta mmoja, kisho utaona kikundi hapo mwenye macho huambiwi tazama. Uroho wa madaraka hupumbaza akili timamu.

BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA: Kuna mengi ya kujifunza toka CCM kwani humaliza mambo yao kwenye vikao, na huoni mwenye kuongelea mambo ya chama nje ya vikao, hapo huo ndio umoja unaotakiwa. Na kama umekosea unatakiwa kumalizana na wenzako vikaoni. Hilo la lugha za utata za nani sijui ana udini au utawala wa imla ni sumu mbaya sana. Rais Kikwete asingekuwa mnyenyekevu na msikivu leo asingekuwa Rais wa Tanzania, lakini baada ya kupata mwanguko wa mende kule Dodoma na Mkapa kutoka kifua mbele, alinyenyekea na kuvuta subira leo huyo kaukwaa Urais. Wapo wengi wa kutolea mizani lakini mwenye kuelewa anaelewa. Ulizeni CUF wamefanyeje kwani imeshindikana kuwasambaratisha kwa nini isiwezekane CHADEMA?


Wapenda mabadililiko tunasoma ishara za nyakati na wahusika wanatakiwa kuchukulia hatua zinazofaa vinginevyo itabaki historia kama ilivyotokea kwa Chama cha NCCR Mageuzi. Na ukiona mmoja hatetereki katika msimamo wake na wakati wengi wanaona yuko nje ya upeno wa nyumba tunayojenga wote ujue kuna anakopata ubavu, na bila kuwa na jicho makini ataendelea eneza sumu, isha kesho utaona wengine wanakuja na jingine hapo ujue mambo ndo yanaanza iva. Kuwa makini na mwendo wa kinyonga wa kubadilikabadilika rangi bila kukusudia mradi amepitia kuliko na rangi anaakisi rangi sawia.

Tamaa ilimshinda Sungura kupata mbivu kwa wanaokumbuka hekaya za Abunuwasi. Na hata katika siasa tunakumbuka wenye majina kama akina Masumbuko Lamwai, Kaburu na hawasikiki kabisa, na sijui kama wana ubavu wa kurudia hadhi waliyokuwa nayo hapo awali katika ulingo wa siasa.

Wana JF mnaweza kutia kapuni maoni yangu lakini ndio ishara za nyakati na kuna siku mtakumbuka ninayoyaongea leo. Ukimdaka nyani anakumalizia mahindi shambani ukiamua kumpiga anakuangalia kwa huruma sana na utamwacha, utajuta kesho ukirudi shambani utakuta mabua tu, kwani njaa ndiyo nyani anaona kitu muhimu kwake kuliko haki ya jasho lako.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom