Mandela Road, Dar: Service Road yageuka parking. Watembea kwa miguu tunapata shida

Mlundilwa Jr

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
2,886
4,283
Service Road imekuwa parking ya malori ktk barabara ya Mandela road mpakani mwa Tabata Matumbi Hadi Buguruni ktk kiwanda Cha Murzah, wananchi watembea kwa miguu na waendesha baiskeli tunapata shida Sana.

Ingawa Kuna vijana wanajiingizia kipato kwa kulinda hayo malori lakini kwa namna nyingine inatupa tabu sisi wananchi watembea kwa miguu na waendesha bodaboda na baiskeli, hivi huu utaratibu kwenye nchi za wenzetu upo kweli hivi Hawa wamiliki wa haya malori hawana sehemu yakupaki haya malori ukiachilia mbali kwenye hizi barabara za watembea kwa miguu.

Nawaomba TANROAD walifanyie kazi hili ikiwa pale maeneo ya garage wameweka Bango la tahadhari ambapo ni makao yao basi na hapa Buguruni wafanye hivyo. Tumechoka na kelo hii kwani inawalazimu waendesha baiskeli kuingia barabara kubwa ili waweze kutokea upande wa pili napo wanapishana na magari yaendayo kasi hamuoni hii ni hatari.

IMG_20210822_091641.jpg
IMG_20210822_091718.jpg
IMG_20210822_091647.jpg
IMG_20210822_091721.jpg
IMG_20210822_091927.jpg
IMG_20210822_091718.jpg
 
Sijawahi kuelewa kabisa hawa ma engineer wetu wana tatizo gani, labda mnieleweshe nielewe : Hivi ni kwa nini hizo side drains (mifereji ya maji) inaachwa wazi hivyo?

Kwanza ni hatari gari na pikipiki kudumbukia humo, pili watu wanaigeuza madampo ya takataka. Kama ingefunikwa kwa slabs za zege tayari faida ingepatikana kwa watembea kwa miguu na baiskeli na pia kupishana..
 
Sijawahi kuelewa kabisa hawa ma engineer wetu wana tatizo gani, labda mnieleweshe nielewe : Hivi ni kwa nini hizo side drains (mifereji ya maji) inaachwa wazi hivyo?

Kwanza ni hatari gari na pikipiki kudumbukia humo, pili watu wanaigeuza madampo ya takataka. Kama ingefunikwa kwa slabs za zege tayari faida ingepatikana kwa watembea kwa miguu na baiskeli na pia kupishana..
Huu ulikuwa ni ujenzi wa zamani Sana mkuu pia hii barabara ilijengwa kwa mda mlefu Sana nahisi hawakuwa na huo ubunifu wakuziba side drains kama tunavyoona hivi sasa
 
Mara nyingi hayo malorry huwa nayakuta hapo nikipita, ila nilichogundua ni kwamba yapo kwenye foleni ya kuingia kwenye magodown ili kupakia/ kushusha mzigo, sio kwamba yamepaki tu, ni kama meli zinavyosubiri baharini miezi miwili ili tu ziingie bandarini kushusha / kupakia mizigo.
I don't agree with your point
Wengi wao hawana oda yoyote kutoka kiwandani Bali wanaamua tuu kupaki hapo na kwenda guest na mademu zao huku mlinzi wamamuachia Albino mmoja.
 
Back
Top Bottom