Mandela na Lema wafanya uamuzi unaofanana - kwenda mahabusu kwa hiari

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Nimesoma kitabu cha Nelson Mandela cha ‘THE LONG WALK TO FREEDOM – Ni kitabu kikubwa kiasi. Tukio kubwa ktk kitabu hicho ni Mandela kukamatwa na polisi wa makaburu kwa tuhuma za kuongoza mapambano na maandamano ya kudai haki na usawa dhidi ya makaburu.

Mandela anasimulia, baada ya kukamatwa na kusweka mahabusu nilipewa chaguo rahisi sana, kati ya kukana na kusitisha harakati za kupinga serikali ya makaburu kisha niachwe huru au nigome kufanya hivyo nirudishwe mahabusu kisha jela kabisa. Akaelezwa hayo –na yeye alijua, jela kuna mawili, unaweza kufa kama wenzake (waliomtangulia wakafa) au ukateseka muda mrefu.

Mandela aliwajibu mahakamani bila woga, mkiniachia tu, nikishatoka nje ya kizingiti cha mlango wa mahakama hii, naanza harakati za kudai haki - alichagua chaguo la pili – Kurudi mahabusu bila kujali kama anaenda kufa kama wenzake au kuteseke muda mrefu. Kwake hilo lilikuwa chaguo rahisi sana. Mara ya pili na ya tatu msimamo wa mandela haukuyumba mahakamani. mwisho wakamsweka jela.

Mandela kama Lema hakutaka kuwadanganya makaburu wamwachie huru ili aendeleze harakati kwa siri au porini. Alijitoa mhanga hadharani na mahakamani kama Lema. Makaburu wakamsweka jela miaka 27. Aliwaambia,
kwangu mimi, heri kufa kuliko kuwa mtumwa wa makaburu ndani ya nchi yangu. Sina sababu ya kuishi kama waafrika wenzangu hawana uhuru, na Mateso haya yote yana mwisho, nisipoona mimi mwisho wake watoto au wajukuu zetu wataona. Mandela akaona matunda ya mapmbano yake miaka 27 baada ya kusota jela.


Lema kama Mandela anasema, na nukuu waraka wake

Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasa bila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.

Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ," JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU


Binafsi nimeumizwa sana na tukio la Lema kwenda mahabusu bila kosa, Lema analalamikia jeshi la polisi kutumika kisiasa. Amegomea dhamana ama alikosa kwangu mimi siyo hoja. Hoja ya maana ni uonevu wanaofanyiwa watu wa Arusha.

Komredi Lema anauliza, maandamano yake toka mahakamani yanatofautianaje na yale ya UVCCM Arusha? hakuna jibu, Anahoji yale maandamano ya Ole Sendeka toka mahakamani akisindikizwa na washabiki wake, yanatofautianaje na haya ya Lema? Jibu halipo.

Halafu na sisi wengine tujilize, watu zaidi ya 200 hadi 500 wanaondokaje wote mahakamani kwa pamoja baada ya kesi kuahirishwa halafu usiite hayo ni maandamano? Je, tuwalazimishe waondoke mmoja mmoja ili isionekane si maandamano? Kuna sheria ya namna hiyo? Kama ipo, ni kwa Chadema tu? Haiwahusu Ole Sendeka na UVCCM? Mazingira haya yanamfikisha Lema njia panda.

Mimi kama Lema najiuliza, utawekewa dhamana mpaka lini kwa kesi ambayo unajua haipo? Si afadhali uende huko ambako wanakutishia, kama alivyosema mwenyewe, ili wajue kuwa uvumilivu wako na uvumilivu wa wananchi wako umefika mwisho? Si inabidi wajue kwamba Jela haiogopwi mbele ya haki?

Hii tishio la kukamata na kuwatoa kwa dhamana viongozi wa Chadema inatofautianaje na tishio la Makaburu kwa Mandela na wenzake? Hivi Lema, Dr Slaa, Mbowe, Ndesamburo nk ambao wamesha lala mahabusu wanakosa gani kama siyo ukaburu wa ccm?
Nini mwisho wa yote haya?

Hata hivyo, pamoja na yote haya, Mimi kama Martin Luther King naona mwanga mbele ya Safari. Naona ccm ikifa kifo cha mende kama makaburu wa Mandela. Ninawaombea Lema, Dr Slaa, Mbowe, Ndesamburo nk ambao wamekwisha lala mahabusu bila kosa waone siku hiyo – wasikose kama Martin Luther king ambaye ndoto yake imetimia mpaka mweusi ( obama kuwa Rais) wakati yeye hayupo.

Aluta Continua.
 
You are not serious!

"Mandela kama Lema" na sio walau "Lema kama Mandela"??

Labda niamini ni ukosefu wa kutoelewa lugha ya Kiswahili vizuri
 
2mechoka kuonewa haki iko wapi tz? Namuombea lema kwa Mungu atoke salama na afanikishe adhma yake ya kutafuta haki
 
I have stupendous respect for Godbless Lema's boldness but I am not so sure if he's already in a position to be compared to Nelson Mandela's intrepidness. You have inordinately exaggerated the eclats and some may deem the remarks to be rather an insult to Mandela more than an accreditation to Lema.
 
You are not serious!

"Mandela kama Lema" na sio walau "Lema kama Mandela"??

Labda niamini ni ukosefu wa kutoelewa lugha ya Kiswahili vizuri
Hayo ni matumizi ya lugha tu ila nafikiri umeelewa, kwenye kiingereza kuna You and I hakuna I and You lakini kiswahili tuna vyote unaweza kusema wewe na mimi au mimi na wewe ni mfano tu, hata hivyo kwenye bandiko lake kuna sehemu ameandika...
Lema kama Mandela anasema, na nukuu waraka wake
 
Matukio hayafanani kati ya lema na mandela,mandela alikuwa anadai uhuru na haki za weusi kwa mikutano na migomo.maandamano ya lema yanadai nini?

Mandela alipewa ofa,afutiwe mashtaka na aache harakati lema hajapewa ofa hiyo kesi bado ipo. Kama mandela angapewa dhamana angetoka kosa lake lilikua halidhaminiki,lema linadhaminika.ni umbumbumbu wa lema na anaowahadaa
 
Nawashangaa mnaotaka kumfanya mandela kama nabii aliyeshushwa kutoka mbinguni, hivi na yeye si binadam aliyejitoa kwa ajili ya upendo kwa binadam wengine? Kuna ubaya gani kumlinganisha Lema na Mandela?

Ni wenye akili zilizoganda tu ndo mnaona hivyo, binafsi naamini lema ni shujaa kama mandela au awe zaidi ya mandela, mandela alipigania haki za weusi dhidi ya makabulu, Lema anapigania haki ya wanyonge dhidi ya dhulma za weusi wenzetu, si ajabu vizazi vijavyo vikamuona Lema ni bora kuliko mandela, mnaobeza sasa ni wivu dhidi ya Lema mkijua wazi kuwa woga unawafanya msithubutu kusogelea viatu anavyovaa mh. Lema.

"watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema
 
You are not serious!

"Mandela kama Lema" na sio walau "Lema kama Mandela"??

Labda niamini ni ukosefu wa kutoelewa lugha ya Kiswahili vizuri

mbona lugha haina utata. Tofauti zao ni zama. Mandela kipindi cha unyanyasaji wa kikaburu lkn lema ni kipindi cha ukoloni mamboleo, kwa kutumia mfumo kandamizi wa kisiasa kwa maslahi ya wachache.
 
matukio hayafanani kati ya lema na mandela,mandela alikuwa anadai uhuru na haki za weusi kwa mikutano na migomo.maandamano ya lema yanadai nini?
mandela alipewa ofa,afutiwe mashtaka na aache harakati lema hajapewa ofa hiyo kesi bado ipo.kama mandela angapewa dhamana angetoka kosa lake lilikua halidhaminiki,lema linadhaminika.ni umbumbumbu wa lema na anaowahadaa

Kwa hiyo, unakubaliana na mimi kuwa wote walipewa ofa, japo mmoja kwa kufutiwa kesi, mwingine kwa kupewa dhamana. Wote wakachagua kurudi mahabusu/jela.
 
Nafikiri mandela hakupewa dhamana...lema alipewa offer ya dhamana akakataa.mandela alihukumiwa kwa uhaini kifungo cha maisha..
 
Back
Top Bottom