Mandela Miaka 27 Jela: Mizuri kwake na kwa Afrika Kusini


Mshombsy

Mshombsy

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Messages
372
Likes
8
Points
0
Mshombsy

Mshombsy

JF-Expert Member
Joined Mar 15, 2013
372 8 0
Wakati tunaendelea kuomboleza kifo cha mpambanaji na muungwana wa kweli Ndg Nelson Mandela naomba nitoe mtizamo wangu juu kifungo chake jela miaka 27.

Mandela alikamatwa 5/8/1962 na toka wakati huo alikuwa gerezani mpaka mwaka 1990. Miaka ya 1960 ni ndicho kipindi ambacho nchi nyingi za Afrika zilipata huru na kuanza kujitawala kisiasa na kiuchumia.

Mandela alipotoka gerezani 1990 alitembelea nchi nyingi za Afrika, Amerika na Ulaya kutoa shukrani zake kwa waliopigania yeye kuachiwa na kuendelea kukisaidia chama chake ANC wakati yeye akiwa gerezani.

Miaka yote hiyo 27 gerezani huku Makaburu wakiitawala Afrika kusini kiuchumi na kisiasa walifanikiwa kwenye nyanja za kiuchumi ingawa uchumi ulikuwa chini ya wachache lakini serikali iliweza kukusanya kodi kubwa za kuweza kuendesha shughuli za kijamii.

Miaka hiyohiyo ambayo Mandela alikuwa gerezani na makaburi wakiitengeneza Afrika kusini kiuchumi, nchi nyingi huru za kiafrika zilikumbwa na utawala mbovu wa kimabavu, sera mbovu za kiuchumi na utawala mbovu.

Nchi nyingi ziliangukia kwenye migogoro ya kisiasa kwa kugombania madaraka na udikteta uliopelekea watawala kujiona miungu watu. Ndoto za weusi kujitegemea kisiasa na kiuchuma ikaendelea kubaki ni ndoto.

Hivyo ziara ya Mandela baada ya kutoka jela mbali na lengo la kutoa shukrani ilimpa nafasi ya kujifunza juu ya mifumo ya kiuchumi inayofaa, umuhimu wa demokrasia.

Miaka 27 jela na ziara ilikuwa ikimwandaa kuyakabili majadiliano ya Afrika kusini mpya: kisiasa na kiuchumi. Majadiliano yaliyofikiwa yalikuwa ni kufuata mfumo wa uchumi wa kibepari huku serikali ikiweka mipango ya kijamii kusaidia masikini.

Majadiliano yaliweka mfumo wa utawala nchi wa kimajimbo unaohakikisha hata makundi madogo yanakuwa na uwakilishi kwenye vyombo vya uwakilishi (electoral college) kwani bila kufanya hivyo bunge la afrika kusini lingekuwa na jamii ya weusi 99% lakini kwa mfumo wa sasa ni kama 60%.

Hivyo kwa yeye kuonyesha moyo wa kutolipa visasi na majadiliano yaliyofikiwa na yeye kuachia madaraka mapema likiwa funzo baada ya kukaa gerezani na kutoka kukuta Afrika aliyoifikiria haiko hivyo liweika historia yake kuwa ya kipekee.

Kwa Afrika kusini kutopewa uhuru mapema kama nchi nyingine kumesaidia kuwa na siasa na mfumo mzuri wa kiutawala vilevile uchumi ulioimara ukilinganisha na walioanza kujitawala wenyewe wakati Mandela anaingia gerezani.

Hakuna ubishi kwamba nchi nyingi za kiafrika huru watawala walionyesha unyama kuliko hata makaburu ndio maana Mandela alitaka taifa la rangi zote.

Sasa hivi Afrika kusini ndiyo kimbilio la nchi nyingine ikiwemo Tanzania viongozi wake kupata matibabu.

Makuburu wameijenga Afrika kusini kiuchumi, Mandela kaijenga kisiasa kwa kuanzisha taifa la kidemokrasia. Ni jukumu la weusi kusogeza mbele hayo yote isije kuwa kama nchi nyingine za kiafrika zinazosuasua toka miaka ya 1960.
 

Forum statistics

Threads 1,250,692
Members 481,461
Posts 29,741,928