Mandela legacy in the eye of poor black south africans

Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Messages
977
Likes
249
Points
60
Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2010
977 249 60
Mandela, mtu aliyejizolea sifa yakuwa mtu bora sana yamkini kuliko wote duniana ktk minajiri ya amani, na hata kufika kuchua ka sehemu kwa uungu kwa baadhi ya watu. Na pia kuwa mtu aliyetokea kupendwa sana na makaburu yamkini kuliko alivyopendwa na wanaharakati(blacks) wenzake. Huyu ni mtu aliyetumikia kifungo cha zaidi ya miaka 27 jela,na baada ya kuachiwa akaamua kuwasamehe wahasimu wake. Maamuzi ya mandela aliyafanya kwa gharama ya kuwaacha wanaharakati ktk vifungo vya maisha kwahabari ya ufukara wa kupindukia na kuwapa neema ya maisha ya kula 'kuku kwa mrija' makaburu. Ifahamike kuwa, japokuwa mandela alifungwa jela 'physically', wananchi weusi na wapigania uhuru walikuwa na wamebakia ktk vifungo vya kudumu vya ufukara wa kutupwa,walikuwa wanapigania kutoka jela ya ukapuku/ufukara uliopelekewa na mfumo wamakaburu. Hivyo, maamuzi yake ya kuwasamehe makaburu ambao kimsingi hata hawakuomba huo msamaha kwa kuamini mfumo wao wa kibaguzi ulikuwa/na upo/ nautabakiwa kuwa sahihi, na pia kuwaachia kuendelea kumiliki uchumi walioupora kutoka kwa wananchi waliowengi, ilimaanaisha na itaendelea kumaanisha nikupoteza 'focus' kwa huyu mzee na yamkini kusahau matakwa ya aliokuwa anawaongoza. Baada ya kuwa rais, mzee Mandela had everything a human being would long for, but it wasn't the case for poor majority south african who could not even had a small piece of farm land in their own country. Kwa mandela kuwasamehe wahasimu wake in that state of affairs was selfishly too easy b'se he could not listen to what his people longed for. Nachofahamu mimi ni kuwa,alikosa ujasiri ktk kuwatendea haki ethinic black majority ambao walidhulumiwa kila kitu kwa zaidi ya karne 3 (300 years). Na akaamua kuwaachia makaburu kila kitu ambao mpaka sasa wanaendelea kuwabagua na kuwanyanyasa weusi waliowengi(zaidi ya 90% of ZAR pop.). Kwa wanamapinduzi, hiyo sio haki kabisa bali niusaliti kwa wanaharakati ambao hawana hope in years to come! Wazungu walio wengi wa south A. are the most barbaric human species in the history of human kind. I'm not sure what future holds for makaburu that the one who used to restrained blackmajority, who they fight a fierce battle to save his life, is no more. May God rest his soul, amen. Ubaguzi umejikita ndani sana ya mioyo ya makaburu, hata ukienda kwenye nyumba za ibada huwezi amini mpaka leo bado idiology ya kubagua weusi ipi hai! Majority southafrican are frustrated and sometimes they misdirect their frustration to foreigners. Makaburu ambao ndio waajiri huwa wanapenda kuwaajiri wakuja (ingawa policies za nnchi yao zinakataza) nabaadaye wanawachongea kwa weusi wazawa kuwa wanachukuliwa nafasi zao za kazi na hao wakuja. Lengo la huu uchonganishi ni kuwazubaisha hawa wazawa waliowengi na kupoteza muono wa picha kubwa badala yake wawaone adui zao ni wakujawakati kimsingi makaburu ndio maadui wabaya sana wa wazawa weusi waliowengi.
Funzo kwa wanasiasa:
Mwanasiasa aliyewekwa kwa ridhaa ya wananchi, anapoingiza matakwa yake na kusahau ya wale waliomtuma, hata matakwa yake yakiwa mazuri kiasi gani, kama yanapingana na ya kundi analoliongoza ni usaliti full stop!

Nawakirisha!
 
2013

2013

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Messages
8,660
Likes
2,080
Points
280
2013

2013

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2013
8,660 2,080 280
tunaheshimu mawazo huru, lakini sio kila mawazo yanajenga
 
2013

2013

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Messages
8,660
Likes
2,080
Points
280
2013

2013

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2013
8,660 2,080 280
haya siyo mawazo, ni ukweli usio na chenga usiopingika!
chenga na chuya nyingi sana mkuu. japo haijawa pumba.
wenye imani na mungu tunaamini hutakiwi kulipa ubaya kwa ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.hii ni roho ya mungu, hata yesu anatufundisha hivi ndicho alichokifanya mzee mandela baada ya kula kalenda zake 27 alipotoka akasamehe yote, ndicho alichokifanya nyerere baada ya Gadafi kuja kumshambulia Tanzania na baadae kumwomba nyerere awaachie huru wanajeshi wake kwa ahadi ya kumpa mafuta, nyerere hakutaka bali akawaachia wanajeshi wa walibya huru akisema thamani ya mtu hailinganishwi na mafuta. kimsingi hata kama angechukua mafuta kipindi kile yale mafuta yangekwisha na upendo wa Gadafi kwa nyerere ungekwisha pia.
hii ni miongoni mwa maneno aliyotamka mandela;
"I have fought against white domination, and I have fought against black domination. I have cherished the ideal of a democratic and free society in which all persons will live together in harmony with equal opportunities. It is an ideal which I hope to live for, and to see realised. But my Lord, if needs be, it is an ideal for which I am prepared to die."
Nelson Mandela, defence statement during the Rivonia Trial, 1964. Also repeated during the closing of his speech delivered in Cape Town on the day he was released from prison 27 years later, on 11 February 1990.

fahamu anayelipa ubaya kwa ubaya huyo ni shetani. huwezi kuwa na furaha na amani moyoni kwa vengeance.
ukweli ni kuwa hata uwe mzuri kiasi gani wapo wazungu wasiopenda weusi , yaani pamoja na Obama pamoja na kuwa rais mweusi lakini wapo wasiompenda kwa weusi wake. na hili liko mioyoni mwa watu, huwezi kuliondoa kwa muda mfupi.ndio maana marekani mpaka leo kuna black church na white church, pia kuna Mormon, na imani nyingine zenye ku-perpetrate ubaguzi, pia jambo hili lipo ulaya, bila kujali kuna rais mweusi anayetawala Taifa kubwa kama marekani. Mke wa obama baada ya kuwa mumewe kuwa Rais amewahi mara kadhaa kupokea lugha za kibaguzi kutoka kwa watu(wazungu) wa karibu na obama, lakini alizipuuza.
Mandela hakuwa Selfish bali alionyesha ujasiri wa hali ya juu, pale alipowasamehe waliombagua na kumfunga jela miaka 27. Hakutaka kuonyesha yeye ni dhaifu bali ni strong sana.
. na ndicho kinachofanya mpaka leo wazungu ulimwenguni kumfanya binadamu exceptional na popular na anayependwa hata na wazungu wenyewe wakiwemo waliokuwa maadui zake, na huku bado akipendwa na kuheshimika na waafrika wenzake pia.

Mandela alisema hakuja pale kupambana na wazungu... here are more details...

"We are not anti-white, we are against white supremacy … we have condemned racialism no matter by whom it is professed."
Nelson Mandela, defence statement during the Treason Trial, 1961.
 
Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Messages
977
Likes
249
Points
60
Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2010
977 249 60
Asante kwa maoni yako! Kimsingi sina tatizo na kusamehe... tatizo lipo ktk mazingira ya kusamehe...nachofahamu mimi, mtu anapaswa asamehewa akiomba msamaha. Hao makaburu hawajawahi omba msamaha, hawaoni kosa. Na kumsamehe adui yako asiyekiri kukosa ni dalili ya woga!!! Ofcourse kwa mandela alitoa msamaha kwa kumaanisha yaliyopita si ndwele, kwa msingi asingerudi kifungoni tena, maana ni wazi kifungo chake kilikuwa kimefikia kikomo...Je unaweza kusema hivyo kwa kundi kubwa alilokuwa akiliongoza? jibu ni rahisi tu, hapana, maana wao mazingira yao duni yalikaziwa hukumu. Badala hata kufikiliwa japo kuwa fidia wahanga hao wa ubaguzi, mzee akaamua kuwakumbatia makaburu. Msamaha bado ungeweza tolewa ndani ya utaifishwaji ili kuwapunguzia wahanga ukali ya ufukala na kujaribu kupunguza upana wa 'inequalities in opportunities' kwa makundi (hapo kwenye red). South africa aliioiacha Mandela haina hiyo "harmony wala equality" ambazo unazikariri ktk nukuu za mzee...watu hawana matumaini baada ya kutiwa changa la macho kwa kupewa uhuru wa kisiasa tu!

Sio kila kitu kinachoshabikiwa na kusifiwa na wazungu kina mashiko, hayo ni mawazo ya kitumwa! Kwa maoni yangu, mara nyingi wazungu wakikusifia sana inabidi uanze kujiwekea alama za kuuliza mwenyewe kwa sababu zilizowazi...! Ofcourse kwa wazungu Mandela aliwakuna penyewe maana baada ya kuchukua nchi tu aliwatosa wafuasi wake!
Nukuu za Mandela sina tatizo nazo lakini ufahamu 'talking is cheap'!
Mandela hakutumwa kupambana na wazungu, alitumwa kupambana na mfumo wa ubaguzi na kuyasawazisha matokeo ya mfumo huo! Ilikuwa kama vile alilewa ghafula mvinyo wa uhuru na kuwasahau kabisa wahanga. Shida ni pale alipowasaliti wahanga kwa kui'abandon ANC freedom charter'! Hii ndio imekuwa inarusha cheche kila kukicha kwa vijana kujaribu kuchimbua mambo yaliyofunikizwa na mzee M! Mifano ya nyerere uliyoitumiaa haina uhusiano ktk unyeti wa maamuzi aliyoyafanya mzee M!

Kuhusu upumba/uchenga kuhusu haya ninayowakilisha, haijarishi sana kwa kuwa inategemeana sana na upeo wako wa kufikilia, kama huwezi elewa leo, basi Mungu akikujalia uishi umri mrefu zaidi, utajakuja elewa namaanisha nini!

katika huu ulimwengu kuna watu wako juu yake, na hao ni wazungu wa magharibi, huwezi fanikisha jambo kirahisi ukionekana unataka kuwahujumu. kiufupi, sio kwamba botha na makaburu wengineo walishindwa kuendelea kumwacha Mandela aozee gerezani licha ya kuwepo waafrika weusi wanaompigania miaka nenda miaka rudi, lazima ujue mataifa haya makubwa ya Ulaya magharibi ikiwemo uingereza yaliweka pressure kwa serikali ya makaburu wa afrika kusini, ili imwachie huru mfungwa huyu, ndipo wakamwachia huru.
hivyo hata kuongoza kwake pale kwa muda mfupi inawezekana alitumia kujenga fikra chanya kwa wakubwa hawa wa ulaya pamoja na kwa waafrika wenzake. Alikuwa na haja ya kuuthibitishia ulimwengu kuwa alistahili kuachiwa huru kwakuwa yeye sio Gaidi bali mpenda Amani bila kubagua.

ukitazama afrika kusini utaona pia wazungu wanaoishi sio wageni bali ni raia halali wa taifa lile kubwa afrika. Wakiwa wanaendesha viwanda na biashara kubwa na kutoa ajira kwa raia wa afrika kusini. Hivyo kitendo cha Mandela kuwageuka sehemu ya raia wake kwa kigezo cha weupe wao kingepelekea maisha kuwa magumu sana kwake yeye binafsi na pengine kuuwawa na hata kungepelekea kuurudisha utawala uleule wa makaburu tena. Alipokea nchi akikuta wenye vyeo vya juu jeshini ni wazungu, mapolisi wazungu, wafanya biashara wazungu, serikalini wazungu, alichofanya ni kuondoa sheria kandamizi katika mfumo ili kuweza kutoa fursa kwa wote kupanda vyeo bila kujali rangi zao.hivyo hata weusi wanauwezo wa kupanda vyeo pia.
Hivyo isingekuwa rational kwa yeye kutumia maskini weusi wasiosoma kuendesha utaifishaji dhidi ya wazungu matajiri (mabepari) wenye viwanda na waliojuu ya mfumo mzima wa nchi na yeye akabakia salama bila kuuwawa. Na hapa mandela angechafua jina lake hata kwa wazungu waliompigania aachiwe huru. Fahamu pia kuna wazungu waliokuwa wakipinga ukandamizaji huu bila kujali uzungu wao.
Mandela alichagua njia sahihi zaidi kuliko vinginevyo.
nukuu

Bofya: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2013/12/131206_wanamichezo_mandela.shtml

Mwanamasumbwi Muhammad Ali alisema: "Maisha ya Mandela yalikuwa na maana kubwa kwa dunia nzima , kwake mwenyewe, kwa taifa lake na dunia nzima.
Alitufanya sisi kugundua kua ni muhimu kumjali mwenzake na kuwa sisi ni ndugu licha ya rangi zetu.''
Ali aliongeza kusema kua, atamkumbuka Mandela sana kwa kuwa mtu mwenye roho safi na alichukizwa sana na mambo ya ubaguzi wa rangi pamoja chuki na uhasama.Aliwatia moyo wengine kufikia mambo waliyoyaona kama yasiyowezekana.''Ali amesema kua Mandela alifunza watu umuhimu wa kuwasamehe wenzao, na leo ameweza kuwa huru.

Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Messages
977
Likes
249
Points
60
Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2010
977 249 60
nimefurahi kuona kuwa umefuatilia mtiririko uliopelekea mzee M kuamua kuwatosa wahanga na kuwakumbatia makaburu!
 
Baada ya uhuru mzee M aliamua kufuata njia rahisi (easy way) ili kusalimisha maisha yake, na ilikuwa rahisi sana kufanya hivyo kwani angepata uungwaji mkono na wazungu wote duniani na hivyo waafrica walio wengi pia wangefuata kwa mkumbo. Kitu ambacho watu hawataki kukiongelea ni kwamba hili kundi lililokuwa likitetewa la wahanga, liliachwa mkiwa likiwa ktk hali ya kuchanganyikiwa.
sisemi kuwa utaifishaji ungefanyika kwa ghafla, nachosema angalau ange'negociate' nao kama alivyofanya Mugabe ili kuruhusu 'smooth transition' wakati huo wakiwaanda na wahanga nao wawe tayari kushika fursa hizo, na siyo kuwatosa na kuruhusu hao wadhulumati wabaki na kila kitu walicho dhulumu. Huwezi ukawa na nchi yenye 'harmony' ktk mazingra ya hivyo. Uhalifu wa hali ya juu wa SA ni sehemu ya mkanganyiko aliowaachia wa SA kwa kuwa kuna vitu havikufanyika. Pamoja na kusoma hizo nukuu na historia, kama utapata nafasi nenda katembelee nchi hiyo ujionee mwenyewe. Wamekuwa wanyonge zaidi ktk nchi yao wenyewe.
(hapo kwenye red)Wazungu wamekuwa wakitaka kutuonyesha kuwa hatuwezi fanya mambo yetu wenyewe bila ya wao. Na kwa bahati mbaya sana waafrika wengi wenye mawazo ya kitumwa pia huwaza hivyo, matokeo yake nchi zetu zimekuwa 'abused' na mataifa hayo 'makubwa'. Ukweli ni kwamba siyo kweli kwamba nchi zetu haziwezi kuendelea bila mataifa ya magharibi(ukweli ni kwamba tunategemeana). Na kama sisi hatuwezi kuwapangia mambo yao, wao pia hawapaswi kutupangia au kuyaingilia ya kwetu. Shida kubwa ni kukosa kujiamini na uthubutu kwa viongozi wa kiafrica waliowengi kama mzee M alivyofanya. Alijiaminisha kuwa wangemuua kama angeendelea na ANC freedom charter ambayo ilitaka kutaifisha mali zote za nchi ili kuzigawanya sawa kwa wananchi wote. Kitu ambacho alisahau ni kwamba, alikuwa anaahirisha tu kifo maana muda ulipofika hata hao makaburu hawakuweza kuzuia asimrudie muumba!
Ile kitu aliyofanya mzee M iliwavunja sana moyo wapambanaji wahanga na kuwaacha ktk hali ya masononeko makubwa na hivyo kila mmoja alivyopata upenyo tu aliamua kuchukua hamsini zake na kuliacha kundi kubwa likiwa sasa halina pa kujiokoa!
Mzee M kama kiongozi kwa waafrica wengi aliokuwa anawaongoza, lengo la kupata uhuru halikuwa kuanza kujipendekeza kwa wazungu na mataifa ya magharibi ili kujisafisha kuwa hakuwa gaidi. Lengo la ANC kama chama cha ukombozi lilikuwa wazi kwa kila mtu hata hayo mataifa ya magharibi yalijua. Ndio maana kuyasaliti hayo kuliwashangaza sana hata hao wazungu!

(…kutoa fursa kwa wote kupanda vyeo bila kujali rangi zao), ndugu yangu hayo yapo kwenye makaratasi tu, ili mweusi apande cheo inabidi a'prove' kuwa ni mzuri mara 3 zaidi ya mzungu. Ni rahisi sana lumpeni tu wa kizungu kupata nafasi na kupanda vyeo na kuachwa kipanga mweusi akisota kwani mfumo bado unathibitiwa na wazungu, na kazi yao kuu ni kutaka kuwafanya weusi wajione kuwa hawafai kwa kuwaweka ktk mazinra duni ili wa'underperform')

Gaidi au sio ghaidi haijarishi, hizo ni propaganda za kizungu ktk kumkandamiza mweusi! Ugaidi wa mzee M ulikuwa wapi!katika huu ulimwengu kuna watu wako juu yake, na hao ni wazungu wa magharibi, huwezi fanikisha jambo kirahisi ukionekana unataka kuwahujumu. kiufupi, sio kwamba botha na makaburu wengineo walishindwa kuendelea kumwacha Mandela aozee gerezani licha ya kuwepo waafrika weusi wanaompigania miaka nenda miaka rudi, lazima ujue mataifa haya makubwa ya Ulaya magharibi ikiwemo uingereza yaliweka pressure kwa serikali ya makaburu wa afrika kusini, ili imwachie huru mfungwa huyu, ndipo wakamwachia huru.
hivyo hata kuongoza kwake pale kwa muda mfupi inawezekana alitumia kujenga fikra chanya kwa wakubwa hawa wa ulaya pamoja na kwa waafrika wenzake. Alikuwa na haja ya kuuthibitishia ulimwengu kuwa alistahili kuachiwa huru kwakuwa yeye sio Gaidi bali mpenda Amani bila kubagua.

ukitazama afrika kusini utaona pia wazungu wanaoishi sio wageni bali ni raia halali wa taifa lile kubwa afrika. Wakiwa wanaendesha viwanda na biashara kubwa na kutoa ajira kwa raia wa afrika kusini. Hivyo kitendo cha Mandela kuwageuka sehemu ya raia wake kwa kigezo cha weupe wao kingepelekea maisha kuwa magumu sana kwake yeye binafsi na pengine kuuwawa na hata kungepelekea kuurudisha utawala uleule wa makaburu tena. Alipokea nchi akikuta wenye vyeo vya juu jeshini ni wazungu, mapolisi wazungu, wafanya biashara wazungu, serikalini wazungu, alichofanya ni kuondoa sheria kandamizi katika mfumo ili kuweza kutoa fursa kwa wote kupanda vyeo bila kujali rangi zao.hivyo hata weusi wanauwezo wa kupanda vyeo pia.
Hivyo isingekuwa rational kwa yeye kutumia maskini weusi wasiosoma kuendesha utaifishaji dhidi ya wazungu matajiri (mabepari) wenye viwanda na waliojuu ya mfumo mzima wa nchi na yeye akabakia salama bila kuuwawa. Na hapa mandela angechafua jina lake hata kwa wazungu waliompigania aachiwe huru. Fahamu pia kuna wazungu waliokuwa wakipinga ukandamizaji huu bila kujali uzungu wao.
Mandela alichagua njia sahihi zaidi kuliko vinginevyo.
nukuu

Bofya: Wanamichezo wamkumbuka Mandela - BBC Swahili - Habari

Mwanamasumbwi Muhammad Ali alisema: "Maisha ya Mandela yalikuwa na maana kubwa kwa dunia nzima , kwake mwenyewe, kwa taifa lake na dunia nzima.
Alitufanya sisi kugundua kua ni muhimu kumjali mwenzake na kuwa sisi ni ndugu licha ya rangi zetu.''
Ali aliongeza kusema kua, atamkumbuka Mandela sana kwa kuwa mtu mwenye roho safi na alichukizwa sana na mambo ya ubaguzi wa rangi pamoja chuki na uhasama.Aliwatia moyo wengine kufikia mambo waliyoyaona kama yasiyowezekana.''Ali amesema kua Mandela alifunza watu umuhimu wa kuwasamehe wenzao, na leo ameweza kuwa huru.

View attachment 125558
 
B

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Messages
1,451
Likes
565
Points
280
Age
41
B

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined May 31, 2012
1,451 565 280
Ni kweli kuna uhuru wa mawazo na wewe Hero umeutumia vzr.

Lakini nadhani ni makosa makubwa kudhani Mandela alitakiwa kufanikiwa kurekebisha kila ktiu kwa utawala wa muda wa miaka 5 wakati nchi na jamii ya SA ilishaharibiwa kwa zaidi ya miaka 300!!!

Yeye amepigania usawa, demokrasia pamoja na maridhiano. Kazi hiyo ameifanya vzr kwa viwango vyovyote vile vya kitaifa na kimataifa. Kwa ukweli kazi aliyofanya ilipita matarajio ya kila mtu pengine hata yeye mwenyewe.

Ni wajibu wa WaSA kufanya yaliyosalia hatua kwa hatua bila kukurupuka.
 
Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Messages
977
Likes
249
Points
60
Hero

Hero

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2010
977 249 60
Baba Kiki… pia ni makosa makubwa sana kufikiri kuwa hivyo alivyanya mzee Mandela kuwa ilikua ndio njia pekee ya kupitia katika kuhitimisha matarajio ya wahanga wa SA. Naamini unafahamu fika kuwa simaanishi kuwa nilitegemea mzee M ayamalize matatizo yote ya wahanga hao! Shida ni kwamba maana na malengo ya mapambano hao yalibakwa mwishoni kwamaamuzi yaliyofanywa na mzee M. Ikumbukwe pia maamuzi yake yalikuwa na sura ya kubeba hatma ya wafungwa wa tabaka la chini, mafukara, kwamba waone angalau mwanga mbele au wahesabu maumivu! Kwake yeye mzee M binafsi alikuwa amefikia kilele cha matarajio yake binafsi kupata uhuru na madaraka makubwa kabisa ambayo mtu anaweza kuyaota, hivyo swala la kusamehe sio gumu kihivyo…lakini alikuwa na wajibu wa angalau kuweka msingi wa matarajio mema kwa wahanga ambao kwa sasa hawana matumaini ya kutoka katika dhuluma waliomo. Hiyo 'civil war' ambayo mzee aliiogopa sana na kuingia makubaliano ya woga na kibinafsi zaidi, inaweza tokea hata sasa kwani kwa hali ya SA, kipindi chote wamekuwa wamo kwenye vita hii ya wenyewe kwa wenyewe. Wakulima wa kizungu wamekuwa wakichinjwa na hata yale mauaji ya hivi karibuni ya wachimba migodi, Malema movements etc ni cheche tu ya moto unaofukuta juu ya uonevu wanaupata wahanga kwa sababu ya hayo makubaliano yaliyowanufaisha makaburu na kuwaacha wahanga wakilia na kusaga meno!
Makubaliano yaliyofanywa na Mugabe kipindi cha uhuru wa nchi yake yalikuwa na mtazamo wa kuweka tumaini kwa wahanga wa Zim ambao mazingira yao hayakutofautiana sana na ya waSA. Hayo makubaliano yalikuwa na lengo la kuwaacha wananchi kwenye 'war/struggle footing' yaana kwamba mapambano bado yanaendlea, kwamba baada ya kipindi flani basi natural resourse zitapaswa kugawiwa kwa usawa kwa raia wote… lakini sivyo kwa makubaliano yaliyoingiwa na mandela ambayo wazungu waliyashangilia na kuya 'publicize' kwa kila mtu ili hatima kutufanya tuamini yalikuwa na maana!Ni kweli kuna uhuru wa mawazo na wewe Hero umeutumia vzr.

Lakini nadhani ni makosa makubwa kudhani Mandela alitakiwa kufanikiwa kurekebisha kila ktiu kwa utawala wa muda wa miaka 5 wakati nchi na jamii ya SA ilishaharibiwa kwa zaidi ya miaka 300!!!

Yeye amepigania usawa, demokrasia pamoja na maridhiano. Kazi hiyo ameifanya vzr kwa viwango vyovyote vile vya kitaifa na kimataifa. Kwa ukweli kazi aliyofanya ilipita matarajio ya kila mtu pengine hata yeye mwenyewe.

Ni wajibu wa WaSA kufanya yaliyosalia hatua kwa hatua bila kukurupuka.
 
Forum statistics

Threads 1,238,302
Members 475,878
Posts 29,315,350