Mandela hastahili heshima ya juu hivi kupita makubwa yaliyofanywa na akina Nyerere

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
images (2).jpg Julus Nyerere VS Nelson Mandela images (1).jpg

Sijaridhika bado na uzito wa Nelson Mandela ukilinganisha na baadhi ya viongozi wengine wambao wamefanya makubwa katika ukombozi wa bara la Afrika na baadhi ya mambo muhimu ulimwenguni. Jambo la pekee kwa Mandela ni kufungwa kwa miaka 26, na baada ya kufunguliwa makubaliano ya ANC ni kumpa nafasi ya kuongoza nchi ambapo alidumu kwa awamu moja na kuamua kuachia ngazi pengine sababu ya matatizo ya kiafya ndio alitaka upweke asibughudhiwe. Zaidi ya kupigania haki za Waafrika huku kusini hakuna tofauti na wapigania uhuru wengine katika bara hili.

Kwa kulinganisha na mmoja ambaye amekuwa katika vichwa vya waafrika wengi
Julius Nyerere naona kwa mtazamo wangu Nyerere yuko juu zaidi kwa juhudi kubwa alizofanya kupigania ukombozi wa bara la Afrika, kwani alijitolea bila hofu na hata umoja wa Afrika kuweka makao makuu ya ukombozi nchini Tanzania. Hata vyama vya wapigania ukombozi makao yao yalikuwa Tanzania, hali kadhalika ANC maskani yao yalikuwa Tanzania, karibu na mji kasoro bahari (Morogoro) ambako sasa ni chuo kikuu cha kilimo (Sokoine University).

Naweza kutafsiri kama mataifa ya magharibi yamefanya jitihada kubwa kumkuza zaidi kwa kile kinachoonekana kujaribu kufunika yale yaliyofanywa nao kipindi cha ubaguzi kwa vile walikuwa ni wazungu wenzao. Lakini kupima kwa vigezo halisi binafsi naona Nyerere yuko juu zaidi ya Mandela, na tena kuna wengine wengi tu wenye kustahili heshima zaidi yake hapa Afrika kuliko yeye. Mataifa ya magharibi yametuteka nasi tumefuata wayatakayo.

Kuna uwezekano mkubwa mpango wa msamaha kwa makaburu kuratibiwa na Askofu Mkuu Desmon Tutu kutokana na itikadi za kidini: "Wasameheni maaduni zenu, 7 x70, waombeeni wanaowaudhi, na usilotaka kutendewa usimtendee mwingine"jambo ambalo ni itikati katika imani ya Desmon Tutu. Dhahiri anayebeba heshima hiyo ni Mandela kwa kuwa aliridhia falsafa na teolojia hiyo.

wpfd728139_05.jpg
Katika picha hii licha ya huyo mhindi
yupo pia mzungu ambaye alikuwa
Waziri wa fedha kwa miaka mingi nchini Tanzania

The multi-racial first cabinet of newly independent Tanganyika. While this sort of thing was seen as strange in other newly independent African countries, for Nyerere this was a matter of course. People were appointed on merit, based on their ability and commitment to the cause. The issue of skin colour did not feature. Amir Jamal (far right, seated), the first of many Tanzanians of Asian origin to serve in Nyerere's cabinet was a long-serving member, for many years holding the powerful portfolio of Finance Minister. He continued to hold high office beyond Nyerere's own retirement, including a five year stint as Tanzania's ambassador to the United Nations in Geneva from 1988 to 1993. His close working relationship with retired President Nyerere continued as he became his personal representative when Mwalimu Nyerere was Chairman of the South Commission and then on the South Centre, and the Dag Hammarskjold Foundation of Uppsala, Sweden. Amir Jamal was continually re-elected to Parliament by his Morogoro constituency with ever greater margins. This is despite the fact that members of his racial group comprised less than 1% of the population, testament to Mwalimu's success in making his country a truly non-racial society. Mr Jamal died in March 1995 aged 74.

[h=1]Update
Rais Kikwete afichua siri kuhusu Mandela
[/h]Rais Jakaya Kikwete jana aliyateka mazishi ya Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, alipotoa salamu mbele ya maelfu ya waombolezaji na wageni wa kimataifa walioshiriki katika mazishi hayo. Rais Kikwete aliweka bayana jinsi Tanzania ilivyoshiriki katika vita ya ukombozi si kwa Afrika Kusini pekee bali kwa nchi nyingi za Kusini mwa Afrika zikiwamo Angola, Msumbiji, Zimbabwe na Namibia.

Kadhalika alizungumzia jinsi wapigania uhuru wa ANC walivyoweka kambi zao na kufungua ofisi za chama hicho nchini Tanzania ambako walipewa makazi na vifaa, maelezo ambayo yalishangiliwa na umati wa watu uliohudhuria. "Kwa hakika ANC walipata makazi mapya Tanzania ambayo waliyatumia kuendesha mambo yao, kujipanga na kuendeleza vita ya ukombozi. Kutoka Tanzania ANC waliweza kuwafikia makada wake na wanachama waliobaki Afrika Kusini kwa kutumia mawasiliano ya siri," alisema Kikwete na kuongeza: "Kimsingi Serikali ya Tanzania ililazimika kuanzisha redio maalumu kwa ajili ya vita ya ukombozi ambayo ANC waliitumia kupaza sauti ambazo walikuwa wamenyimwa na utawala wa ubaguzi wa rangi."

Rais Kikwete aliyekuwa na kazi ya kumwelezea Mandela kama mpigania uhuru, alieleza jinsi Mandela alivyofika Tanzania Januari 1962 bila kuwa na hati ya kusafiria na kwamba katika mazungumzo yake na Hayati Mwalimu Nyerere alieleza mpango wa kudai uhuru kwa njia ya mapambano. "Mwalimu Nyerere alikuwa na maoni tofauti kuhusu mpango wa kuendesha mapambano kwa kutumia silaha, lakini baadaye walikubaliana na Tanzania ilikubali kuanzishwa kwa kundi hilo na mwalimu (Nyerere) aliwapa sehemu ya kuendeshea shughuli zao na vifaa," alisema Kikwete na kuongeza: "Kwa hiyo, kwa wale walioshiriki katika vita vya ukombozi na askari wa MK (Jeshi la ANC), majina kama Kongwa, Mgagao, Mazimbu na Dakawa hayawezi kuwa mageni na pengine mtakumbuka enzi zile maisha yalivyokuwa."

Kikwete alisema wakati akiwa Tanzania, Mandela alikuwa akiishi kwa aliyekuwa Kada wa TANU, Marehemu Nsilo Swai na kwamba baada ya kusaidiwa kupata nyaraka za kusafiria kwenda Nigeria, Morocco na Ethiopia, aliacha buti zake nyumbani kwa mzee huyo. "Familia hii iliendelea kutunza buti hizo wakitaraji kwamba Mandela atarudi, lakini wakati anatoka katika safari yake hakupita tena Tanzania na kwa bahati mbaya alipofika Afrika Kusini alikamatwa na kufungwa," alisema Kikwete katika hotuba iliyorushwa na vituo vyote vya televisheni vya kimataifa.

Aliongeza: "1995 ikiwa mwaka mmoja tangu Mzee Mandela aingie madarakani, viatu vile vililetwa na mjane wa marehemu Swai, Vicky Nsilo Swai ambaye nimekuja naye leo ili ashirikiane nanyi katika msiba huu ninyi mlio ndugu zake." Alisema vita ya ukombozi haikuwa rahisi kwani wakati mwingine Tanzania mbali na kuwasaidia wapigania uhuru hati za kusafiria, ililazimika pia kuwapa majina ya bandia ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri.

Alimtania Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki akimuuliza iwapo alirejesha hati yake ya kusafiria na kusababisha waombolezaji kuangua kicheko. "Sifahamu kama Thabo amerejesha ya kwake," alisema. Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, uhusiano baina ya Tanzani na Afrika Kusini si wa bahati mbaya kwani umejengwa katika mizizi ambayo ilistawishwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Mzee Mandela. "Huzuni yenu, ni huzuni yetu na majonzi yenu ni majonzi yetu pia maana kama alivyo kwenu Mandela kwetu alikuwa kiongozi, baba na mfano wa kuigwa," alisema Rais Kikwete huku akimtambulisha Mama Maria Nyerere katika ibada hiyo.
Alisema baada ya kutoka gerezani, Mandela alifika Tanzania ambako alipokewa na umati mkubwa wa watu katika rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa na ujio wa kiongozi mwingine yoyote. Katika hatua nyingine, Rais mstaafu wa Zambia, Kenneth Kaunda jana aliuchekesha umati wa waombolezaji pale alipokwenda kwa kukimbia wakati alipoitwa jukwaani kwa ajili ya kutoa shukrani.

Kaunda pia alisababisha watu kuangua kicheko pale alipomwita Kikwete kuwa "bwana mdogo" wakati alipokuwa akianza mazungumzo yake. "Waheshimiwa marais, akiwamo huyo bwana mdogo kutoka Tanzania……," alisema Kaunda.

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Hapo nadhani ndio maana itakuwa vigumu kwako kuridhika na uzito wa Nelson Mandela!

Akian Nyerere, Jombo Kenyata na wengine wengi tu walifungwa enzi za kupigania ukombozi, hili la Mandela kufungwa si geni, kama ni kufungwa tu ndio kulikompa uzito huo wakati kuna wengine wengi tu walifungwa na walipokuwa huru waliendelea kupigania haki hadi nchi zinapata uhuru. Hapa kwa kufungwa tu kwangu hoja haijatosheleza kupata uzito huo.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
South africa inajulikana kuliko africa mkuu, ukitembea nje ya Africa utaona jinsi ambavyo wazungu wanaona Sa ni kama jimbo lao ila tu liko Africa

Ukweli huo haupingiki kwa vile walishaweka mizizi yao baada ya kugundua njia ya kufika India kwa urahisi kupata viungo kwa kuzungukia Cap of Goood hope, na waholanzi wakazamia kulima vyakula vya kulisha mabaharia wanapotia nanga SA. Ndio maana nimesema wazungu wametuteka nasi tumeingia kichwakichwa kwa vile huko ni himaya yao hata kama watawala wa sasa ni waafrika.
 
Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
13,953
2,000

Na wazungu ukiangalia vyema utagundua ndio wenye dunia, so hatujakosea kubebwa mzoba mzoba kwenye hilo. Wanajitukuza na ndio mana the son of Africa Robert Gabriel mugabe hakupewa nafasi ya kuongea..angewasema vby outrightly

Nimeshangaa kuona magazeti ya huku Australia yanaweka headline za Mandela, nusu mlingoti..wakati watu weusi wa huku (abo) hawawataki na wanawachukia sana kwa jinsi walivyowaua babu zao bu the time wazungu wanakuja na kukuta abo wana maisha yao.

Eti hata Tonny Abbot nae kaja Africa?? Loh hawa wazungu ni shenzi sana
 
Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,601
2,000
Akian Nyerere, Jombo Kenyata na wengine wengi tu walifungwa enzi za kupigania ukombozi, hili la Mandela kufungwa si geni, kama ni kufungwa tu ndio kulikompa uzito huo wakati kuna wengine wengi tu walifungwa na walipokuwa huru waliendelea kupigania haki hadi nchi zinapata uhuru. Hapa kwa kufungwa tu kwangu hoja haijatosheleza kupata uzito huo.
Tusitake kurahisisha historia kiasi hicho. Kama ulikuwepo kabla na baada ya uhuru na kufuatilia harakati za ukombozi wa bara la Afrika tangia enzi hizo sidhani kama itakuwa sahihi kwako kufikia hitimisho jepesi kama hili.
 
Swts

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
3,063
2,000
We sweet changia hoja, usikimbilie kwenye mapenzi
teh mkuu candid unalike kwa mbali...hahahah...me apo la kuchangia hmmm naona Mandela amefungua watu weusi duniani pote kuhusu suala zima la ubaguzi wa rangi.... Nyerere ana yake ila Mandela anastyle heshma yake!
ivi nae alikuwa na kifimbo cha kichawi kama grandpa wetu..teh
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Na wazungu ukiangalia vyema utagundua ndio wenye dunia, so hatujakosea kubebwa mzoba mzoba kwenye hilo. Wanajitukuza na ndio mana the son of Africa Robert Gabriel mugabe hakupewa nafasi ya kuongea..angewasema vby outrightly

Nimeshangaa kuona magazeti ya huku Australia yanaweka headline za Mandela, nusu mlingoti..wakati watu weusi wa huku (abo) hawawataki na wanawachukia sana kwa jinsi walivyowaua babu zao bu the time wazungu wanakuja na kukuta abo wana maisha yao.

Eti hata Tonny Abbot nae kaja Africa?? Loh hawa wazungu ni shenzi sana

Ukiangalia Nyerere hakuwa na chuki na wazungu, alipochaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wazungu waliokuwa na mapenzi mema kwa nchi za kiafrika hakuwaacha nje ya utawala wake, maana aliweza kuwapa nafasi kadhaa katika serikali hali kadhalika wahindi.

Waziri wa fedha tangu tupate huru hadi miaka ya 70 alikuwa mzungu nadhani alikuwa anaitwa Jennings kama sijachanganya jina lake ambaye sasa ni marehemu, alikuwa Mwingereza. Pia miaka ya nyuma kipindi cha Nyerere aliweza kumpokea mkimbizi mmarekani ambaye alikuwa na itikadi za kijamaa akawa anaishi Arusha. Mji wa Morogoro kwa miaka kadhaa katika awamu ya kwanza walikuwa na mbunge mwanamke mhindi.
 
Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
13,953
2,000
teh mkuu candid unalike kwa mbali...hahahah...me apo la kuchangia hmmm naona Mandela amefungua watu weusi duniani pote kuhusu suala zima la ubaguzi wa rangi.... Nyerere ana yake ila Mandela anastyle heshma yake!
ivi nae alikuwa na kifimbo cha kichawi kama grandpa wetu..teh

Umaarufu wa NM umekuzwa na wazungu ndio mana dunia nzima imezizima kwa kifo chake. Nyerere hakupata promo ya kimataifa
 
Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
14,929
2,000
Mwinyi wakati anaingia madarakani Mishahara ya
wafanyakazi alikosa akaomba kwa MUGABE........Nyerere was corrupt Leader in Africa, ukubali ukatae
 
Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
13,953
2,000
Ukiangalia Nyerere hakuwa na chuki na wazungu, alipochaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wazungu waliokuwa na mapenzi mema kwa nchi za kiafrika hakuwaacha nje ya utawala wake, maana aliweza kuwapa nafasi kadhaa katika serikali hali kadhalika wahindi.

Waziri wa fedha tangu tupate huru hadi miaka ya 70 alikuwa mzungu nadhani alikuwa anaitwa Jennings kama sijachanganya jina lake ambaye sasa ni marehemu, alikuwa Mwingereza. Pia miaka ya nyuma kipindi cha Nyerere aliweza kumpokea mkimbizi mmarekani ambaye alikuwa na itikadi za kijamaa akawa anaishi Arusha. Mji wa Morogoro kwa miaka kadhaa katika awamu ya kwanza walikuwa na mbunge mwanamke mhindi.

Mlinzi wa mzee Botha(the most arrogant president of ZA) aliwahi mfuta vumbi NM baada ya kutoka sero! Unaweza jiuliza ni kwa nini?
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Tusitake kurahisisha historia kiasi hicho. Kama ulikuwepo kabla na baada ya uhuru na kufuatilia harakati za ukombozi wa bara la Afrika tangia enzi hizo sidhani kama itakuwa sahihi kwako kufikia hitimisho jepesi kama hili.
images (2).jpg images (1).jpg
Ninachotaka kujua hoja za pekee zinazomfanya Mandela awe juu kwa kiwango hiki, maana sifa ambazo ninazifahamu kwa sasa ni kupigania haki za waafrika walio wengi nchini mwake kama walivyofanya akina hayati Walter Sizulu na wenzake, kufungwa miaka 26 jela, kisha kufunguliwa akachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo. Labda kwa sababu aliwasamehe watesaji wake? Hilo linaendana na umri aliokuwa nao, laiti angekuwa bado na umri kama wa mtomoto yangekuwa mengine ile kitu inaitwa "retaliation." Kumbuka hayati Mandela alikuwa Mwanamasumbwi.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Mwinyi wakati anaingia madarakani Mishahara ya
wafanyakazi alikosa akaomba kwa MUGABE........Nyerere was corrupt Leader in Africa, ukubali ukatae

We are human being, hakuna aliye mkamilifu, hata Kikwete amegeukia upande wa marehemu Matonya kuzunguka huku na kule na hakuna bara asilolikanyaja kupitisha bakuli wakati rasilimali zipo, hana jinsi maana uwezo wake umeishia kupitisha bakuli badala ya kutumia utajiri uliomo nchini.

Kumbuka kuwa Nyerere rasilimali za nchi hii alizitumia kwa ajili ya ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo Afrika Kusini.
 
Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,601
2,000
...laiti angekuwa bado na umri kama wa akina Mwigulu Mchemba, Zitto Kabwe, Nape Mnauye, Mwigamba, Le Mutuz yangekuwa mengine ile kitu inaitwa "retaliation." Kumbuka hayati Mandela alikuwa Mwanamasumbwi.
Sasa huo ni utani ambao siko tayari kuuendeleza. Suala hapa ni zaidi ya hao wanasiasa unaowataja. Achana na ufuasi wa siasa za majanga kwanza, kabla hatujaweza kuendelea na huu mjadala.
 
Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
13,953
2,000
Sasa huo ni utani ambao siko tayari kuuendeleza. Suala hapa ni zaidi ya hao wanasiasa unaowataja. Achana na ufuasi wa siasa za majanga kwanza, kabla hatujaweza kuendelea na huu mjadala.

Candid scope una maanisha jamaa alikuwa "mwili ni dhaifu ila roho i radhi"?

U are very wrong bloke
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Sasa huo ni utani ambao siko tayari kuuendeleza. Suala hapa ni zaidi ya hao wanasiasa unaowataja. Achana na ufuasi wa siasa za majanga kwanza, kabla hatujaweza kuendelea na huu mjadala.

Sorry, haja yangu hapa nataka kuonyesha kuwa umri aliokuwa nao Mandea wakati anatoka kifungoni alishakuwa mzee, hakuwa na nguvu zaidi za kujenga utetezi na pengine hakufikiria kama atatoka kifungoni. Hali halisi ya wazee na vijana tofauti ndio maana hapo nimeleta tu kama utani si kitu kamaili kwa kuchanganya vijana wanasiasa machachari, nadhani kuna jambo la kujua tofauti ya ujana, utu uzima na uzee. Ujana ni motomoto, utu uzima ni kupima kwenye mizani athari lipi halileta madhara zaidi, na uzeeni ni kutaka amani zaidi. Ni mambo ya kisaikolijia tu haya. Kwa hili la kusamehe kwangu naona tu kisaikolojia Mandela umri wake ulidai hivyo.

Askari Kanzu, angalia post # 15, unafikiri katika umri ule alipokuwa mwanamasumbwi kijana machachari angeweza kuwa laini kama alivyotoka kifungoni? Jibu unalo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom