Mandela hakuwa msaliti kama inavyodaiwa. Alisimamia vema sera za ANC

Jamiitrailer

Member
Oct 20, 2019
25
80
Kuna mdau waliweka uzi katika JF leo na katika mtindo wa maswali alijaribu kuonesha picha ya NELSON MANDELA kama msaliti wa jitihada za harakati za kudai haki na usawa nchini Afrika ya kusini.

Nitajaribu kutoa picha tofauti na mtazamo huo katika haya yafuatayo chini:

Historia ya mapambano ya kudai haki na usawa katika Afrika ya kusini ni ndefu na yenye kona nyingi. Ikumbukwe kuwa Afrika ya kusini ilishapata uhuru wake mapema mwaka 1910. Kwa hiyo mapambano yenyewe yalikuwa ni ya kudai haki na usawa katika jamii kwa vile mfumo wa sheria,uchumi na biashara uliwapendelea wazungu. Mathalan, mtu mweusi hakutakiwa kisheria kuchukua mkopo mkubwa katika bank. Na kutokana na hilo, fursa kubwa za kibiashara kama tenda za ujenzi wa majengo na miundombinu hawakutakiwa kufanya. Hali hiyo iliwafanya Weupe katika Afrika kusini kuzidi kuwa matajiri kwa kupendelewa fursa nyingi za kiuchumi.
NELSON MANDELA alijiunga na chama cha ANC wakati tayari hicho chama lilishaanza mapambano miaka mingi nyuma kabla hata Mandela hajazaliwa. Msingi mkuu wa ANC ulikuwa ni kudai haki hizo ili jamii ya Afrika ya kusini iishi katika usawa. ANC walisema hawakuwa na agenda ya ubaguzi; lengo lilikuwa ni kupigania haki kwa watu wote bila kujali rangi zao. Kutokana na agenda hiyo hata watu wasio weusi kama jamii ya wahindi ambao nao walikuwa wakibaguliwa nao wakajiunga na harakati za kudai haki kwa WAZI. Lakini kuna kitu ambacho hakisemwi sana ambacho kwa watu ambao hawajazama sana katika mwenendo wa historia ya Afrika ya kusini wanaweza kushangaa endapo wakiambiwa ukweli kwamba walikuwapo pia wanaharakati weupe waliounga harakati za weusi kwa SIRI. Mathalan, makampuni ya Anglo Gold na hasa kampuni tanzu yake ya Debeers yalikuwa yakiiwezesha ANC kifedha kwa siri ili kukwepa adhabu toka serikalini.

Sasa nirudi katika hoja ya uzi uliotolewa unaouliza kama Nelson Mandela alikuwa msaliti.
Kutokana na mtiririko wa matukio Nelson Mandela hakuwahi kuwa msaliti wa harakati za kudai usawa kabla hajaenda jela, akiwa jela na baada ya kutoka jela. Alipokamatwa na kushtakiwa na baadaye kuhukumiwa, Mandela alikuwa na msimamo uleule. Ikumbukwe kwamba kosa ambalo yeye na wanaharakati wenzie walishtakiwa nalo ni TREASON,..shtaka la kufanya njama za kuipundua serikali, kosa ambalo adhabu yake ni kifo. Lakini alipopewa nafasi ya kujitetea, yeye ndiyo kwanza akatoa ile hotuba fupi maarufu sana hapo mahakamani akielezea malengo na mtazamo wa harakati zao,..akahitimisha kwa kusema kuwa kama kudai haki na usawa ndilo hilo analoshtakiwa na kuhukimiwa nalo yuko tayari kufa,."..IF NEEDS BE I'M READY TO DIE ".

Mandela alikataa hongo ya kutolewa jela kwa sharti la kwenda kuishi nje ya Afrika ya kusini na kupewa huduma zote za kianasa na makaburu. Kwa hlo hakuwasaliti wananchi kwa vile kwa kubaki kwake jela kukamfanya yeye kuwa nembo ya watu kudai haki, na watu ndani na nje ya Afrika ya kusini kuzidisha mapambano na msukumo wa kudai haki kwa serikali ya kibaguzi.

Msukumo dhidi ya makaburu ulipozidi,kulikuwa hakuna namna kwa makaburu,ikabidi wakubali kubadili sera za ubaguzi na kwa mantiki hiyo kuwaachia pia wafungwa wote wa kisiasa waliofungwa wakidai haki na usawa.
Kwa kufanya mabadiliko ya sera katika Afrika ya kusini kungemaanisha kuwa hata vyama vya siasa vingekuwa huru kushiriki katika uchaguzi. Katika hali hiyo ilishajulikana kuwa endapo Mandela angeachiwa, na ANC kushiriki uchaguzi huku Mandela akiwa mgombea wake, ANC ingeshinda uchaguzi kwa kishindo.
Katika hiyo hali kuna masuala kadhaa ilibidi yajulikane mapema,na hasa kuhusu aina ya sera ya kiuchumi ambayo serikali itakayoongozwa na ANC ingeendesha. Kwamba ingeendesha SERA YA KIUCHUMI WA KIBEPARI au SERA YA UCHUMI WA KIJAMAA? Serikali ya makaburu pamoja ba sekta binafsi, sekta binafsi iliyohusisha wafanyabiashara wakubwa kama vile wamiliki wa migodi walitaka kujua hatma yao itakavyokuwa baada ya kuingia serikali ya ANC. Kama ANC ingependa kufanya sera za kijamaa ingemaanisha kwamba njia kuu za kiuchumi pamoja na migodi,mashamba na viwanda vingetaifishwa toka sekta binafsi na kuwa katika umiliki wa serikali. Kwa hiyo ilikuwa muhimu kwa wafanyabiara wale ambao kihistoria walikuwa weupe kujua hatma yao; ANC iongoze nchi kijamaa, ili wao waondoke mapema au ANC iongoze kibepari au uchumi huria ili wao wabaki.

Ili kujua hilo ilibidi lazima vikao vya makubaliano kati ya wadau wote vifanyike mara kadhaa. Washiriki wa vikao walikuwa watendaji wa serikali ya makaburu na wafanyabiashara kwa upande mmoja na wawakilishi wa ANC kwa upande wa pili. Muwakilishi mkuu wa ANC alikuwa Mandela, upande wa sekta binafsi wawakilishi walikuwa akina William na Harry Oppenheimer wa kampuni ya Anglo Gold. Serkali iliwakilishwa na watendaji wa juu wakiongozwa na PW Botha ambaye alikuwa kiongozi wa nchi na vikao vilifanyika nyumbani kwake.

Ikumbukwe tena jambo la msingi, sera ya ujamaa haikuwa muundo wa ANC toka awali kwa hiyo kufikia makubaliano ya aina gani ya mfumo wa kiuchumi watatumia haikuwa suala la mjadala. ANC waliamini katika uchumi huria, ambao ni ubepari.
Akina Oppenheimer ambao walikuwa wakiisaidia ANC kifedha kwa siri walimkumbusha Mandela juu ya jitihada zao hizo katika vikao. Na Mandela aliwakumbusha ANC ilichokipigania toka mwanzo, kwamba hawawachukii weupe lakini wanapinga sera zinazowabagua weusi na kuwapendelea weupe. Kwa hiyo serikali ya ANC ikiingia madarakani itasimamia uchumi wa kibepari kama ilivyoamini lakini ingesimamia haki na usawa kama ilivyopigania toka mwanzo.

Chama ambacho kilikuwa nacho ni cha ukombozi katika Afrika ya kusini lakini chenye mlengo wa kikomunisti ni SACP ambacho kiongozi wake miaka ya tisini alkikuwa ni Chris Hani. Hiyo ina maana kuwa kama chama cha SACP kingeshika madaraka baada ya uchaguzi mwaka 1994 ,serikali yake ingeendesha sera za utaifishaji wa njia zote kuu za kiuchumi.

Baada ya Nelson Mandela na ANC kuingia madarakani waliendesha nchi kwa mfumo wa uchumi huria/ubepari, mfumo ambao upo hadi leo na ni mfumo ambao upo katika kila nchi duniani kwa sasa isipokuwa Cuba pekee.
Katika hali ya kuleta usawa kwa fursa hasa kwa weusi ili kufidia lile pengo la umaskini uliotengenezwa na miaka mingi ya unyanyaswaji, serikali ikaanzisha sera maalum (BLACK EMPOWERMENT)ya kuwawezesha weusi ili nao kuweza kufanya biashara kubwa ambazo awali hawakuruhisiwa kuzifanya.

Katika sera hiyo, weusi waliwezeshwa na kupewa upendeleo maalum na serikali ili waweze kufanya zile biashara na tenda kubwa ambazo awali hawakuruhusiwa kufanya na serikali ya makaburu. Sera hiyo maalum ya upendeleo ndiyo ikawatengeneza wafanyabiashara mabilionea wa mwanzo wa Afrika ya kusini kama akina Tokyo Sexhwale na Cyril Ramaphosa, rais wa sasa.

Kwa hiyo kabla ya kusema kwamba Nelson Mandela aliwasaliti weusi inabidi huo ukweli niliouleza hapo juu ujulikane na kuingia kwenye akili za watu kwanza.

Kuna baadhi ya watu ndani na nje ya Afrika ya kusini wanaamini kwamba Mandela baada ya kuingia madarakani alitakiwa ataifishe mashamba,migodi na biashara zote za weupe ili aonekane kwamba ameleta usawa.
Hoja hiyo ni dhaifu kwani sera kiuchumi ya ya ANC haikuwa katika utaifishaji toka mwanzo na hata sasa; Na kama Mandela angesimamia utaifishaji ,basi angekuwa anakiuka mtazamo na sera za chama chake.
Kuna hoja nyingine dhaifu inayosema kwamba Mandela aliwasaliti weusi kwa vile hadi anaondoka madarakani watu weusi bado wengi walikuwa maskini.
Ijulikane wazi kwamba pamoja na ukweli kwamba serikali ya Mandela ilianzisha sera maalum ya kuwezesha weusi, lakini mabadiliko ya kimaendeleo kwa weusi yasingeweza kuja kwa haraka ndani ya miaka mitano, huku ikizingatiwa kuwa hata hao weupe pamoja na kupewa upendeleo iliwachukua zaidi ya miaka 70 kuwa katika hali ya kiuchumi waliyokuwa nayo.

Upotofu huo wa kufikia waliokuwa nao weusi Afrika kusini, ulikuwapo pia kwa waafrika wakati nchi zao zikipata uhuru toka. Wao walidhani kwamba wakishapata uhuru tu, basi kila kitu kitakuwa kinatolewa bure na serikali. Julius Nyerere ilibidi awaamshe watu kwa kuwaambia UHURU NA KAZI..,ili wafanye kazi.

Sent from Yahoo Mail on Android
 
Umeongea na kuchambua vizuri lakini kwa nini miaka mwishoni akiwa jela wengi walimchukia Mandela waluona amewabadilikia kwa kwenda kuongea na hao wazungu peke yake na kukubali baadhi vitu bila wenzake kujua !! Au kulitokea mini zaidi ??
 
Unganisha na suala la uraiswa Afrika Kusinina kifo cha Chris Hani ili mtiririko uwe vizuri chief.
 
Hakuna wa kumsafisha Yule mzee yuda, tena usiongee hayo alipo Julius Malema, utampa kesi ya jinai ya kujeruhi mtu.

Mtu alienda kupatana na wazungu, na akakubali kuwasamehe watesi wa wote Kama vile kaumia peke yake.

Na nini kilimkuta kuingiza jeshini wazungu wengi mwaka wa kwanza tu wa utawala wake?
 
Umeongea na kuchambua vizuri lakini kwa nini miaka mwishoni akiwa jela wengi walimchukia Mandela waluona amewabadilikia kwa kwenda kuongea na hao wazungu peke yake na kukubali baadhi vitu bila wenzake kujua !! Au kulitokea mini zaidi ??
Kwanza hakuchukiwa na wenzie. Pili isingewezekana watu wote waende kuwakilisha maana ingekuwa kitu cha ajabu watu wote wa ANC waende katika meza ya majadiliano,ukiachilia ukweli kwamba hata wawakilishi wa serikali na wale kutoka sekta ya wafanyabiashara walienda wawakilishi tu na siyo watu wote. Na wangemchukiaje wakati kile alichokiwakilisha ndo kilekile ambacho ANC ilikisimamia toka mwanzo? Nikukumbushe jambo moja, kama katika hayo majadiliano kulikuwa na waliopoteza (loosers),basi kati ya watu hao walikuwa ni PW Botha. Botha alilazimishwa kukubali hali halisi hiyo na idara ya usalama ya nchi yake baada ya tathmini iliyobaini kuwa kamwe wasingeweza kushikilia msimamo wa sera ya ubaguzi hadi mwisho na taifa lisimame, huku kibano cha wadai haki kikizidi na vikwazo vya kiuchumi toka nje vikinukia.
Wengi wanaosema aliwasaliti, kimsingi wenyewe ni wabaguzi japo weusi. Katika hao Winnie Mandela alikuwa mmoja wao, ambaye yeye alitamani TOTAL CONFISCATION ya mali zote za weupe,..kitendo ambacho ni cha kiubaguzi tu.
Mmoja wa watu kama hao wa miaka ya karibuni ni Julius Malema ambaye japo amezaliwa miaka ya karibuni lakini alikuwa akiwa kiongozi wa vijana wa ANC alimpiga vita Thabo Mbeki kwamba hafai kwa vile anatetea sera za kiuchumi zinazopendelea wazungu. Malema alikuwa kati ya watu waliofanya fitna Mbeki aondoke ili Jacob Zuma achukue nafasi kwa kuwa kichinichini Zuma alitamani pia migodi itaifishwe,..kioja ni kuwa walitamani itaifishwe lakini wapewe weusi. Baada ya Zuma kuingia madarakani, na Malema akiwa mwenyekiti wa vijana wa ANC,katika mkutano mmoja wa ANC Malema alimwambia Zuma hadharani kuwa amekuwa msaliti kwa kusita kutaifisha migodi na mashamba. Malema akihojiwa na mwandishi wa BBC ambaye ni mzungu ,aliyetaka kujua undani wa sera na madai yake,....Malema alimtukana na kumwambia.." ni washenzi weupe kama wewe ndiyo hamtakiwi hapa,..huu ni muda wetu"
Malema alikuwa dhahiri ni mbaguzi,.na alipozidisha ubaguzi wake akafukuzwa ANC. Walichoshauri wachumi wakati wa Zuma ni kwamba ni bora Afrika kusini iendeelee na sera ya kuwezesha weusi katika fursa za kiuchumi kuliko kutaifisha migodi na biashara mashamba kiasi cha kuanguasha uchumi kama ilivyokuwa kwa Zimbabwe. Ilishajulikana serikali ingekuwa ngumu kujihusisha na biashara na kufanikiwa katika uchumi wa kibepari, sasa wakishataifisha wanampa nani aendeshe migodi na mashamba? Makada wa ANC walitaka wapewe wao wagawane.
Sasa hao watu ambao hawakuwa na hata chembe ya uzoefu katika biashara hiyo wangeimudu? Lakini kitendo cha serikali kuwapora migodi raia weupe na kuwapa raia weusi wamiliki, siyo ubaguzi?

Kule Zimbabwe, siku ya uhuru mwaka 1980,Robert Mugabe aliwaahidi weupe ambao wangeamua kubaki katika Zimbabwe huru kwamba watakuwa na haki zote kama raia wengine na shughuli zao zitaendelea kama kawaida.
Suala la mgawanyo wa ardhi lilipokuja kukupamba moto miaka ya 2000,wakulima weupe walitoa wazo kwamba wao wangeitoa nusu ya ardhi wanayoirumia katika kilimoili igawiwe kwa weusi ili walime kilimo cha kawaida, lakini serikali ilikataa. Ikumbukwe kuwa hiyo nusu ya ardhi waliyotaka kuitoa hata robo ya hiyo wakulima weusi wasingemudu kulima. Wazo hilo lilikuwa suluhisho zuri kwani wakulima weusi wangepata ardhi na wakulima weupe wangebaki pia na ardhi ambayo wangelima ili uchumi wa Zimbabwe usianguke. Lakini serikali ikakataa tena ,na matokeo yake mashamba yote yakaporwa toka kwa weupe na kupewa makada wa ZANU PF ambao hawakuwahi hata kulima bustani kabla ya hapo,.. Sitaki nikuaambie nini kilitokea baada ya hapo kwa vile unajua ...
 
Nitarejea kusoma tena niweke rekodi zangu sawa .....
 
Back
Top Bottom