Mandela ALAMA YA SIASA ZA KUUNGANISHA WATU!

Nape Nnauye

MP Mtama
Dec 26, 2012
99
408
Katika hali ya kawaida chuki kati ya weupe na weusi Afrika Kusini,chuki iliyojengwa kwasababu ya ubaguzi wa kutisha uliotendwa na serikali ya makaburu, haikua rahisi kudhani kwamba lingekua ni jambo rahisi kuwafanya watu wasahau na kusameheana na leo waishi kama Afrika Kusini moja! Nelson Mandela(Madiba) kaliweza hili. Ndio maana ninaamini Madiba ni mfano bora wa viongozi waliondesha siasa zao kwa kuunganisha watu, badala ya kuwagawa.

ALITUMIA DAWA YA UPENDO KWENYE JAMII ILIYOKUWA IMEJAA CHUKI NA AKAFANIKIWA KULINGANISHA TAIFA LAKE! R. I. P baba
Madiba, pumzika kwa amani baba Afrika!
 
Hii ni nzuri sana na ni ya kuungwa mkono

Lakini nakuja kwako wewe pamoja na chama chako
Ni kwanini mankuwa wagumu sana kujifunza kutokana na makosa ya wengine?

Mmeiongoza nchi kwa miaka 50 na bado ni masikini wa kutupa,ni upendo gani unaouona hapo kwa wananchi mnaowapa kupitia chama chenu?

Ni upendo gani unaouhubiri hapa ambao wewe mwenyewe na chama chako mmeshindwa kuufanya kwa nchi yenu?
Hakuna chuki mbaya kama kuwafukarisha wananchi
Hakuna unafiki mkubwa kama kuhubiri kitu ambacho wewe mwenyewe hauko tayari kukifanya!
 
Katika hali ya kawaida chuki kati ya weupe na weusi Afrika Kusini,chuki iliyojengwa kwasababu ya ubaguzi wa kutisha uliotendwa na serikali ya makaburu, haikua rahisi kudhani kwamba lingekua ni jambo rahisi kuwafanya watu wasahau na kusameheana na leo waishi kama Afrika Kusini moja! Nelson Mandela(Madiba) kaliweza hili. Ndio maana ninaamini Madiba ni mfano bora wa viongozi waliondesha siasa zao kwa kuunganisha watu, badala ya kuwagawa.

ALITUMIA DAWA YA UPENDO KWENYE JAMII ILIYOKUWA IMEJAA CHUKI NA AKAFANIKIWA KULINGANISHA TAIFA LAKE! R. I. P baba
Madiba, pumzika kwa amani baba Afrika!
Nape nakusifu kwa kauli hii ya busara. Lakini usiishie hapa JF tu. Nenda uitendee kazi hii kauli yako. Washauri wana CCM wenzako waige mfano huo wa Mandela wa kuwaunganisha wananchi. Waache mara moja kuwa kama makaburu kwa kufanya propaganda chafu za ukabila udini na ukanda ili kuwagawa watanzania.
 
Pole Nape. Kauli yako ni ya kinafiki kwa vile chama chako ndicho kimegeuka kuwa makaburu kwa kung'oa watu kucha, kuua kwa mabomu na kuendekeza propaganda za chuki. Mfikishie Mwigulu huu ujumbe.
 
^^
Naomba nikuulize, Ile tuhuma ya CCM "A" na CCM "B"
imeunganishwa kwa wema au kwa kutunza visasi mpaka uchaguzi ufike?
^^
 
Nape Mnafiki tu, anaongea asichotaka kukitenda. Nyerere alisema kaburu wa leo ni mtu mweusi ambaye ndiyo CCM na mafisadi inayowashikilia.
 
Katika hali ya kawaida chuki kati ya weupe na weusi Afrika Kusini,chuki iliyojengwa kwasababu ya ubaguzi wa kutisha uliotendwa na serikali ya makaburu, haikua rahisi kudhani kwamba lingekua ni jambo rahisi kuwafanya watu wasahau na kusameheana na leo waishi kama Afrika Kusini moja! Nelson Mandela(Madiba) kaliweza hili. Ndio maana ninaamini Madiba ni mfano bora wa viongozi waliondesha siasa zao kwa kuunganisha watu, badala ya kuwagawa.

ALITUMIA DAWA YA UPENDO KWENYE JAMII ILIYOKUWA IMEJAA CHUKI NA AKAFANIKIWA KULINGANISHA TAIFA LAKE! R. I. P baba
Madiba, pumzika kwa amani baba Afrika!
Kaka yangu Nape hivi kweli unacho kiandika unamaanisha au ni katika kuhakikisha ume post thread humu jf? wewe ukiwa kama kiongozi wa ngazi ya juu katika chama chako kwanini unashiliki katika kuhakikisha mnatugawa watanzania kwa misingi ya udini, ukanda na ukabila ilihali unajua ni hatari kwa ustawi wa taifa? CCM ya leo imegeuka kuwa zaidi ya makaburu ya Afrika kusini na wewe umekuwa ukihubili sana udini, ukabila na ukanda hii zambi itawatafuna ccm wote na vizazi vyenu nakuambia ili ujue unacho kifanyya wewe na chama chako hakitufurahishi watanzania wengi.
 
Nape ni mmoja wa waasisi wa siasa za kubagua wachagga. Amekuwa anawaongelea wachaga kama watu ambao hawana haki nchi hii na hawastahili kuwepo nchini.

Wanasiasa wanafiki sana. Nape anapata wapi ujasiri wa kuandika kuhuburi haya anayohubiti hapa? Siasa za kuunganisha watu kazijua lini wakati anabagua watu kwa misingi ya ukabila?
 
Unafiki mtupu ambao umeugemeza kwenye kifo cha Simba wa Afrika Tata Nelson Madiba Mandela...

Hata tusiende mbali, ninyi CCM mmeshindwa kuendeleza kile alichokiacha Kambarage leo hii unaleta hili faraguo...

Sio ninyi ambao siasa zenu zimejiegemeza kimakundi ndani ya Chama chako?

Sio ninyi ambao mmewafanya Watanzania waonekane watumwa ndani ya nchi yao?

Mmeuza rasilimali za nchi hii kwa bei chee, mmeuza utu wenu kwa ngozi nyeupe kwa gharama ya kura za Watanzania...

CCM hakika ninyi ni tambara bovu msoweza kuchuja mawe wala mchanga, hakika hamfai maana ni Wazandiki wakubwa...
 
Ni kweli aliwaunganisha watu aliruhusu mahakama ya kadhi kuendelea kuwepo Afrika kusini.Mungu amuweke mahali pema.
 
Sasa nimegundua kwa nini Nape Nnauye ulipata F ya Civics kidato cha nne...

Zilonga tofauti, Zitenda tofauti. Kila siku unahubiri ukabila na udini majukwaani na kuwabagua wachaga lakini leo unajifanya mfuasi wa kuunganisha watu. Shame on you Nape Nnauye
 
Mmepata pa kujifanya na nyie wazalendo, naona mmekimbilia huku na Mwigulu wako. Tena mtuwache kabisa na machungu yetu na nyie kaeni na meno yenu ya tembo.
 
!
!
hizi ni siasa tu....eti Afrika Kusini hakuna ubaguzi na wanaishi kama ndugu!?...........yaani ni noma sana na wala huhitaji darubini kujua hilo. Ubaguzi upo tena upo sana tu, hizi tamthilia za isidingo sijui mambo ya soka haya yanatupotosha tu
 
Unavyosemaga chadema ni chama ya wachaga na wakristo ndio siasa za kuunganisha watu. Maneno yako ipo siku yatakuhukumu.
 
Na kwa hakika kitu kimoja ambacho kinanifanya nimtpfautishe Mandela na viongozi wengine wala sio harakati zake za kupambana na ubaguzi na kuhakikisha SA huru bali ile hatua yake ya kuanzania Kamati ya Mapatano na Maridhiano.

Hakuna mwanadamu ambae angependa kutawaliwa na kudhalilishwa milele hivyo hata kama Mandela asingetokea bado wangetokea wengine wakapigana dhidi ya ubaguzi. Lakini linapokuja suala la mapatano na maridhiano, ni very exceptional issue.

Inawezekana kabisa kwamba kiongozi mwingine yeyote ambae angekuwa ni first Black President SA nae asingependa suala la visasi kutokea lakini sidhani kama angefanya kama alivyofanya Mandela; kwamba watu(tena wazito) wanajitokeza hadharani, mbele ya TV na kukiri makosa yao bila kujali kwamba wewe ni Kaburu au Mwafrika wa ANC; provided ulihusika kwa namna moja au nyingine, lazima uhojiwe.....haikuwa ni kamati dhidi ya Makaburu peke yao bali hata manguli wa ANC kwavile Mandela alifahamu kwamba wakati wanapinga ubaguzi hata wana-ANC nao walifanya mambo kadhaa yasiyo ya kibinadamu!!

Hakumuachwa hata mke wake anayeheshimika sana, Winnnie Mandela....wote wakahojiwa mbele ya tume huku mahojiano yakirushwa Live; very impressive! Mandela alifahamu wazi kwamba kama angewataka watu wasemeheane kwa kauli tu kutoka Ikulu, basi watu wasingesameheana; lazima visasi vingekuwepo!

Rest In Peace Madiba!
 
Maraisi wote wa dunia wametoa salamu zao za rambirambi usiku kwenye nhi zao, wakwetu ilikuwaje?
 
Maraisi wote wa dunia wametoa salamu zao za rambirambi usiku kwenye nhi zao, wakwetu ilikuwaje?
Wa kwetu anakwenda live kwa siku kadhaa anasubiri kukamilishiwa posho nono ya safari. Mzee wa masafa a.k.a fastjet
 
Tutasikia mengi kwenye huu msiba. Kama alivyo taamka madiba,kaburu mweusi ni mbaya zaidi ya kaburu mweupe. Tunayaona haya kwa viongozi wetu wa sasa. Mida mingine unawaza uhuru wetu una maana gani. Maana viongozi wamekuwa zaidi ya
wakoloni,viongozi wapo kwa ajili ya kudholotesha nchi, sio kustawisha nchi. Kiongozi akiingia madarakani yeye ndiyo anakuwa mastaplan wa jinsi gani ya kuiba.
 
Back
Top Bottom