Sijui ni kwa nini Arsenal hawakuchukuwa point 3 toka kwa hawa losers? There is always next season.
 
umemaliza kila kitu hakuna cha kuongeza hapo ingawaje baadhi ya watu wanamtetea kwamba eti apewe muda nunue wachezaji wake wakiborongo ndo alaumiwe kama mechi ya leo alikuwa na kagawa akashindwa kumtumia kumuanzisha na hata sub alipoingia akaend kumchezesha pembeni 11,young akarudi saba hivi kweli unategemea kwa asilimia 100 akisajili wachezaji ataweza kuwatumia??? Mimi nahisi uwezo wa kocha ni mdogo anapokuwa na timu ya wachezaji wengi kufanya selection ya first eleven timu imepotea toka dk ya kwanza ya mchezo nilitegemea anagefanya mabadiliko half time ila nilikuwa disapointed na suprised kuona kwamba hakufanya changes yoyote.... Sasa sijui alitegemea miujiza gani??


Wanaometetea Moyes wanapingana na ukweli ambao itabidi waukubali tu baadae. Mimi mwenyewe nakiri kuwa nilikuwa mmoja wa walioamini kwa kiasi kikubwa kwamba Moyes ndo anafaa kumrithi SAF hata kabla ya babu kustaafu. Na kama Moyes atakuja kupata mafanikio na United baadae nitakuwa wa kwanza kukubali kwamba nilikosea kusema kwamba hafai. Kuna mabo mengi yanayosababisha mimi kufikia kusema kwamba Moyes afukuzwe.


  1. Moyes hajanonyesha muelekeo anaotaka timu ielekee. Kwa wale wanosema kwamba hajapata nafasi ya kunua wachezaji anaotaka yeye na hivyo apewe muda kujenga timu yake mwenyewe wana mantiki ya kusema hivyo lakini hata bila hao wachezaji anaowataka bado sijaona mfumo wowote anaojaribu kuintroduce ambao tunaweza kusema kwamba mfumo tunao bado wachezaji tu.Tukumbuke kwamba wachezaji tulionao sio wachovu wa kihivyo kiasi kwamba ndo iwe kisingizio cha matokeo kuwa mabaya. These are proffesional players I'm sure under the right coaching and direction they are more than capable of adapting to new ways and new systems at least to a point we can say that the team is working towards something different and we just need a few new players, but we don't even have a clear direction as to what Moyes is trying to do. We don't know if he is trying to implement an attack mindset or if he is trying to instill a more discpline unit or whatever. Bottom line is Moyes amerithi wachezaji wazuri zaidi ya wale aliowaacha Everton kwahiyo matokeo au style ya kucheza yanatakiwa yawe angalau mazuri kuliko Everton kitu ambacho hatuwezi kusema kwa sasa.
  2. Sifa kubwa anayopewa SAF ni uwezo wake aliokuwa nao wa kuadapt kutokana na muelekeo wa mechi au mchezo wa soka kwa ujumla. SAF asingekuwa mtu wa kubadilika kutokana na nyakati asingepata mafanikio aliyoyapata katika career yake. Tukija kwa Moyes hilo pia hana. Mechi kuenda kushoto kupo ila kinachomata ni jinsi kocha anavyoweza kusoma nyakati na kufanya maamuzi kujaribu kurudisha muelekeo. Nikisema mabadiliko simaanishi mabadiliko ilimradi tu bali mabadiliko yenye malengo kuendana na situation. Mara ngapi msimu huu tumeona Moyes akifanya mabadiliko na kuvuruga rhythm nzima ya timu? Kwa mfano mechi ya leo Kocha mwenye uwezo angegundua kuwa United walishindwa kudictate mchezo kwahiyo basi angejaribu kurudisha stability by changing the midfield. Cleverley ni mchezaji anaefaa kwenye mechi ambazo United wanamiliki mpira, mechi ya leo ilihitaji mchezaji kama Flethcer ambaye angempa Carrick defensive support and in return allow Carrick to do what he does best (dictate the tempo of the game). Kwa maoni yangu mabadiliko haya alitakiwa ayafanye wakati wa mapumziko. Pia angeona kwamba Smalling was not playing well so maybe take him out have Valencia play at RB and bring on someone like Januzaj or even the youngster Jesse Lingard who would probaly have offered more offesinvely than Valencia managed to do. Swala lingine kuhusu kuadapt ni kwamba 4-4-2 si formation inayofaa kwa mpira wa kisasa haswa kwenye Champions League. 4-4-2 inafaa kama una "spine" nzuri na winga zilizotulia kwenye kikosi. Nikisema spine namaanisha viungo na mabeki wa kati. United hawana spine nzuri kabisa na ma-winga wanasuasua kitu mtu yoyote anayeangalia mpira anaweza kukwambia kwahiyo kuona kocha anang'ang'ania hiyo fomation ya 4-4-2 inaonyesha kuwa kocha haoni au labda ni mgumu wa kubadilika.
  3. Moyes pia anaonyesha kuthamini wachezaji wanaojituma zaidi kuliko "skill" players, kitu ambacho sio kibaya sana lakini anatakiwa kuangalia balance ya timu pia. Kumpanga Young na Valencia ni kwamba utapata winga wachapa kazi lakini mashambulizi yatakuwa limited au one-dimensional. Ukiangalia kiungo kama Cleverly sio mtu wa kutengeneza kwahiyo Moyes alitakiwa aangalie kuwa utengenezaji wa mashambulizi ungetoka wapi? Au kama malengo yake hayakuwa kushinda mechi na alikuwa anatafuta droo basi asingepanga washambuliaji wawili. Wachezaji wachapa kazi ni muhimu lakini wasiwe sababu ya timu kuwa pungufu kwenye ushambuliaji.
  4. Kwa kawaida binadamu tulivyo ni kwamba tunaamini zaidi mifano na uhakika kwamba mtu flani ameshafanya kitu flani na kwahiyo akisema fanya hivyi na hivyi tunakuwa wepesi zaidi kufuata maelekezo yao kwasababu tuna uhakika kuwa wanajua wanachokifanya. Hata kama mtu hajaonyesha kuwa anajua anachokifanya akikuelekeza kitu ukakifanya ukapata mafanikio au ukaona muelekoe wa mafanikio basi utaendelea kumwaamini. Nahisi kinacho endelea Man United sasa hivi ni kwamba wachezaji walimkubali Moyes mwanzoni maana SAF alimchagua na walikuwa tayari kukubali mabadiliko yoyote aliyokuja nayo. Lakini baada ya muda wote huu na hakuna hata muelekeo wa mambo kubadilika lazima wachezaji watakuwa wameanza kupoteza imani kwa Moyes. Wakiangalia CV ya Moyes hamna accomplshment yoyote kubwa wanayoweza kusema 'we can trust this guy to lead us because of this'. Moyes hakuwa mchezaji mzuri enzi zake wala katika kipindi chake cha ukocha hajaonyesha uwezo mkubwa, lakini wengi tulikuwa tayari kumkubali maana wapo wengine kama Mourinho ambao hawakuwa wachezaji wazuri lakani wameonyesha uwezo wa kuadapt na kuproduce mafaniko, hivyo tukadhani kwamba Moyes akipewa wachezaji wazuri zaidi na hela nyingi basi ataweza. Ukweli ni kwamba hawezi! Ona jinsi Martinez alivyo ibadili Everton na mfumo wao wa kucheza katika kipindi hicho hicho. Sawa Moyes hajanunua wachezaji aliowataka maana alichelewa kuanza kazi United, mbona Martinez alianza kazi Everton wakati sawa na Moyes? Mbona yeye aliona wachezaji aliowahitaji na akasajili ndani ya muda huo huo mdogo? Kwangu mimi nahisi ndio sababu Wachezaji kama Vidic, Nani na Anderson wameamua kuangalia maslahi yao sehemu nyinginge. Ukiongezea upendeleo wa wazi ambao Moyes ameonyesha kwa wachezaji wa kawaida kama Young, Welbeck, na Valencia wakati Chicharito, Kagawa, Nani wameshawahi kuonyesha uwezo zaidi lakini hawapewi nafasi lazima timu itakuwa imegawanyika kwa kiasi fulani. Na timu ikianza kugawanyika basi ujue pia hata matokeo uwanjani yataathirika.
Hayo ni mawazo yangu tu kuhusu kinacho endelea sasa hivi na kwanini basi ni muhimu United kumuondoa Moyes. Moyes akibaki basi ujue timu ya msimu uajo itabalidika kwa kiasi kikubwa, kitu ambacho si kibaya maana hii timu inahitaji mabadiliko, lakini mabadiliko makubwa kwa wakati mmoja yatasababisha United kukosa Champions League kwa misimu michache ijayo. Kinacho hitajika sasa ni kocha ambaye atawarudishia wachezaji waliopo kujiamini kwao because these players might not be good enough to win the Premier League but I believe they are good enough to qualify for the Champions League and that should be the most important target for the next season.
 
Hahahahahahahahhahahahahhahahahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahhahahahahaha:baby:Cc: mwallu
 
Last edited by a moderator:
Bado chelsick nao kugongwa 2 kwa 0 ili tunywe maji yakapita!
Poleni ndugu,usicheke mamba kabla hujavuka mto,nimekula ela yangu kwa muhindi safi kbs
 
Bado chelsick nao kugongwa 2 kwa 0 ili tunywe maji yakapita!
Poleni ndugu,usicheke mamba kabla hujavuka mto,nimekula ela yangu kwa muhindi safi kbs

Hahaha, we will see about that but the Blues are the saviors of english football, the only in England now to scare Barca and Bayern
 
Hahaha, we will see about that but the Blues are the saviors of english football, the only in England now to scare Barca and Bayern

hawa manure nao walisema hivyohvyo!
Tusubiri bado masaa nanyi tutawafuata hukohuko kwenu kuwapa chai
 
Sikupata kuushuhudia mtanange huu but nasikia combination inayochukua almost 500,000 pound per week ilikuwa na combination ya 0 shots on target.
BTW hii inamaanisha nini kwamba EPL haina tena strong team za kucompete in in europe? Maana mpaka sasa timu 3 za England zimekula kichapo kinachofanana cha 2 kwa nunge.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Bado chelsick nao kugongwa 2 kwa 0 ili tunywe maji yakapita!
Poleni ndugu,usicheke mamba kabla hujavuka mto,nimekula ela yangu kwa muhindi safi kbs


Chelsea mtawasikia hivyo hivyo! Kwani mmesahau mlivyopigwa na Man Shit?
 
Ni afadhali Manchester United itolewe mapema tukibahatika kuvuka raund hii tukakumbana na Bayern au Real watatufanyia mauaji ya kutisha.Manchester ilistahili kufungwa kwasababu zifuatazo.

1. Timu imekosa vipaji binafsi,hakuna mchezaji anayeweza kuibeba timu inapozidiwa ni kisema kipaji binafsi namzungumzia mchezaji kama Ronaldo,Messi......Aina ya wachezaji hii inakosekana katika kikosi cha Man.Mchezaji kama Robin body language inaonyesha ameathirika kisaikologia.Timu imekosa malengo,timu haina speed pass.

2. Mfumo wa kulazimisha kupanga washambuliaji wawili Robin na Rooney katika mechi moja umesababisha Man kuwa predictable.Mfumo wa 4 4 2 umeshindwa kufanyakazi hata katika mechi nyingi za EPL sioni sababu zinazomfanya Moyes kulazimisha mfumo huu kwaajili ya kuwafurahisha Robin na Rooney.Timu nyingi zinacheza na mshambuliaji mmoja Man washambuliaji wawili kunasababisha kupwaya kiungo hasa sehemu ya kati kati.

3. Mimi ni mpenzi wa Man lakini sijawahi kumwamini T Cleverly hata siku moja nilipomwona kati list ya wachezaji watakao anza nikajua tumeumia.Ukweli ni kwmba Tom ni mchezaji wa kiwango cha chini sana hastahili hata kukalia bechi la Man ningekuwa na mamlaka angekuwa mchezaji wa kwanza kuuzwa hawazi kupigachenga,hawezi kukaba vizuri,hawezi kufunga......Ni mchezaji ambaye kamwe asingeweza kucheza kama angekuwa Chelsea,Arsenal au Man City lakini Man United anapangwa katika mechi kubwa siajabu hata kidogo tunashikilia nafasi ya sita.

4. Moyes anachelewa kufanya substute mfano mechi ya jana Cleverly alichemka mwanzo mwisho badala ya kumbadili dk za mwanzo aliachwa mpaka timu inafungwa magoli mawili ndio anastuka.Valencia alikuwa mchezaji mzuri sana lakini baada ya kuumia vibaya mpaka leo ameshindwa kurudisha kiwango chake cha zamani cross zake nyingi zinazuiwa mapema kabla hazijatua kwenye box kuna siku nilikuwa naangalia mechi ya Man Valencia alipiga cross 8 kati ya hizo cross 6 hazikufuka kwenye box zilizuiliwa mwanzoni kabla ya kuleta madhara.
 
Watani zangu wa ulaya mnanisononesha sana.Huyu babu mnampendea nini?au bado mnampa muda?mtampa muda mpaka timu ifike daraja la kwanza?jamani Man U inahitaji kocha wa kufanana nayo!mie nataka mrudi kwenye kiwango ili siku moja tukutane CL nirudishe zile goli za Giggs 1999.Mlinionea sana miaka ya 90's nawatafuta kweli tena mkiwa fit!hebu pona haraka mgonjwa Man U jamani hii sio Man U niijuayo kabisa!timua hili zee!
 
Back
Top Bottom