Gary Neville on Manchester United:
“I think you have to be a unit in and out of possession, and when you only deliver in moments, those moments won’t go for you in certain games. You need patterns of play, way of playing — I still see a group of individuals playing in moments.”
================

huyu kocha mbovu wa zamani wa valencia anapata wapi jeuri hii ya kumnanga baby face kutoka norway, alikuwa wapi kwa kipindi chote hicho mpaka ajitokeze leo hii kuzungumzia ishu ya structure, pattern of plays haliyakuwa sisi tuliokuwa huku uswahili na tusio na taaluma yeyote ya kimpira tumekuwa tukilizungumzia swala hili kwa miaka mitatu. si ndiye gary neville huyu aliyeuliza eneo gani lijengwe sanamu la ole baada ya kuwatoa PSG kwa kikosi dhaifu
=================

ujio wa thomas tuchel ndani ya chelsea umekuwa ni faida kwa upande wa chelsea kwa sababu ya mafanikio alioyaleta kwa kubeba makombe, pia kitendo cha thomas tuchel kuimpelement falsafa ngeni ya kiuchezaji ndani ya chelsea na kueleweka kwa muda mfupi na wachezaji pia linaweza kuwa ni tusi kubwa kwa kocha wetu ambaye mpaka mchana wa leo hajulikani anachokisimamia ndio maana si ajabu hata rafiki yake anayeitwa gary ameonekanwa kushitushwa mwenendo wa timu kiuchezaji na si kimatokeo. Ole ana takwimu bora sana kuliko kocha mwengine wowote baada ya kuondoka kwa ferguson kimatokeo na rekodi nyenginezo ukiondoa makombe ndio maana mjadala wake unakuwa ni mgumu..

mimi bado nina imani na ubora wa kikosi kilichopo tunaweza kufanya vizuri, sikubaliani na mawazo ya wengineo wanaojaribu kuonyesha matatizo fulani kuwa ndio sababu ya timu kufanya vibaya kiuchezaji na baadae kimatokeo, kumekuwepo na vuguvugu la kuwalaumu wachezaji wanaocheza CDM (fred, matic, scott) na RB (wan bissaka, dalot) kuwa ni kikwazo cha timu kucheza vizuri. Kocha bora mfano wa klopp ameweza kumfanya jordan henderson aonekane kuwa ni mchezaji bora mbele ya hadhira japokuwa wengi wetu hatuamini hivyo yote ni kwa sababu amemtengenezea structure ilio bora.

ndani ya muda mfupi tumeshuhudia thomas tuchel akiwasuka baadhi ya wachezaji na kuwafanya waonekane tishio haliyakuwa mwanzoni walionekana ni wa kawaida na waliokwishapitwa na wakati, baadhi ya wachezaji hao ni jorginho, rudiger, thiago silva, christensen.

Legendary Fergie aliweza kuwafanya zaidi wachezaji 20 wenye viwango vya wastani kuonekana kuwa ni wa umuhimu ndani ya kikosi na hatimaye waliweza kuwa sehemu ya vikosi tofauti vilivyoshinda makombe makubwa kwa mihula tofauti (fletcher, sylvestre, oshea, phil neville, wes brown, quinton fortune). Kwa mukhtadha huo ni wajibu wa kocha kutransform kiwango cha mchezaji husika kutoka level moja kwenda nyengine na si tu kusubiria kila tatizo litatuliwe kwa njia ya usajili.

Ni kipofu pekee ndiye atakayepingana na huu ukweli wa kwamba tatizo letu kubwa lipo kiufundishwaji zaidi na si wachezaji tunaopenda kuwatoa kafara ( lack of a well-drilled structure and pattern of play). ukitaka kuuona kwa uwazi kabisa udhaifu wa mwalimu wetu eneo la structure ya kiuchezaji jaribu kumchunguza siku anayofanya rotation ya wachezaji, wakati zipo timu mfano man city, liverpool hata kama watabadili nusu ya kikosi bado pattern ya kiuchezaji inabaki kuwa ni ile ile.

pia kutokuwa na mchezaji bora kwenye eneo moja au mawili haiwezi kuwa sababu ya timu kucheza na presha kubwa kila wiki, Ole anahitaji kufanya mapinduzi makubwa ya kimbinu kwa takribani mechi zote na si kusubiria mechi kubwa (hapa anakuwa anajiandaa vizuri sana mpaka tunashangazwa).

kama yeye ameshindwa basi asione tabu kufanya mapinduzi ya benchi lake la ufundi either kwa kuajiri assitant mwenye uzoefu au hata kwa kumtafuta rafiki yake aliyepo molde anayeitwa eric laurie anayejishughulisha na ukufunzi pamoja na uchambuzi wa mifumo ya kiuchezaji (sipo serious), teh teh bila ya shaka fuentte anamfahamu. Kama ameweza kuleta kocha maalumu wa kufundisha set piece basi na hayo maeneo mengine ayatazame kwa jicho ang'avu

Hata sir alex ferguson kwa nyakati tofauti tulishuhudia akifanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa sababu tofauti, kwa mfano aliwahi kufanya kazi na Brian Kidd (kwa sasa yupo man city kwa takribani miaka 10), Rene Meulensteen, carlos queroz (hapa tukashuhudia mapinduzi ya mifumo kama 4-3-3, steven mcClaren, Walter Smith japo kwa muda mfupi, Archie Knox (huyu alifanya naye kazi akiwa aberdeen na baadae manchester united).

Moyoni sifurahishwi kabisa na kelele za kumuondoa Ole Gunnar kwa sababu ya alichotufanyia akiwa mchezaji na haya mapinduzi yake ya ujengaji wa timu, ametufanya tuhame katika dunia ambayo tulikuwa hatufahamu changamoto kubwa za timu yetu ni zipi mpaka kuikaribia kwa asilimia 80 nchi ya ahadi, leo sote tunafahamu usajili gani tufanye hata dirisha lijalo (RB, DM, CF) na hiyo imetokanwa na kazi bora iliofanywa na Ole kwa kutuanzia upya structure ya ujengwaji wa timu (cha ajabu structure ya kiuchezaji kwa kila wiki ndio inamshinda).

Nitasikitishwa sana kama atakubali kuivunja nyumba hii kwa mikono yake mwenyewe, kwangu mimi nawafikiria zaidi hawa vijana wa academy na mustakabali wao, Je atakuja mwanadamu anayeamini soka la kuwapa nafasi vijana?
======================


mkataba wa kazi haufanani na maagizo ya vitabu vya dini, muda wowote mkataba unavunjika
Hans-Dieter-Flick2.jpg
Hata Norwich huwa wanacheza kwa pattern ya kueleweka kuliko man United.

Ni heri Ole angemrejesha Rene Moulisten kwenye coaching staff akawaondoa Carrick na Kierian Mackena.

Timu gani duniani inayocheza hovyo kama united kwa sasa ?.

Mbeya kwanza wanacheza mpira mzuri kuliko Manchester United.
 
Hata Norwich huwa wanacheza kwa pattern ya kueleweka kuliko man United.

Ni heri Ole angemrejesha Rene Moulisten kwenye coaching staff akawaondoa Carrick na Kierian Mackena.

Timu gani duniani inayocheza hovyo kama united kwa sasa ?.

Mbeya kwanza wanacheza mpira mzuri kuliko Manchester United.
Mbeya kwanza mbali ivyo simba sports club inacheza mpira mzuri kuliko united yangu
 
View attachment 1955452
Borrusia Dortmund CEO Hans- Joachim Watzke alipokuwa akihojiwa na kituo cha habari kinachoitwa Sport 1 amedai ya kwamba moja kati ya sababu kubwa iliomfanya jadon sancho ashinikize usajili wa kuelekea manchester united ni kule kukoseshwa nafasi ya uhakika (kipaombele) cha kucheza timu ya taifa licha ya kufanya vizuri sana alipokuwa bundesliga (Dortmund) kitakwimu.
===============
kwani huko manchester united ukimuondoa harry maguire kuna mchezaji mwengine wa kiengereza mwenye uhakika wa kucheza kila mechi ya timu ya taifa (najua atatajwa luke shaw aliyerudishwa msimu huu kikosini).

halafu kama kucheza premier league inaweza kuwa sababu kuu ya kucheza timu ya taifa ya england mbona alexander arnold hapewi nafasi haliyakuwa kitakwimu ni bora zaidi kuliko trippier, tumuache gareth southgate na balaa lake la 3-4-3

zamani tuliambiwa england walikuwa na kizazi cha dhahabu kilichokuwa na uwezo wa kuwapa mafanikio jambo ambalo ukikaa ukilifikiria utagundua ya kwamba hilo suala halina ukweli wowote (na mimi niliuamini uzushi huu) .

ukweli ni kwamba baadhi ya maeneo waingereza walikuwa na wachezaji wazuri sana waliokuwa na uwezo wa kugombania namba taifa lolote ila kuna baadhi ya maeneo walikuwa hawana wachezaji wenye viwango vya uhakika ndio maana walikuwa wanasumbuka kuvuka hata robo fainali especially pindi inapotokezea mchezaji fulani amekosekana au amecheza chini ya kiwango.
  • goalkeeper walikuwa ni kawaida sana (david james, paul robinson, robert green)
  • mpinzani wa gary neville alikuwa ni danny mills, wes brown, phil neville (wote hao ni wachezaji wenye viwango vya kawaida sana)
  • mpinzani wa ashley cole alikuwa ni wayne bridge (fullback wa kawaida sana)
  • walinzi wa kati walijaaliwa kuwa na kizazi bora sana hilo halina ubishi
  • DM hawakuwa naye, baadae alikuja michael carrick ila hakupewa nafasi
  • playmaker walijaaliwa kizazi bora sana (lampard, gerrard, scholes)
  • winga (beckham na joe cole pekee ndio wenye ubora), ila hao wengine wakiemo darius vassel na kieron dyer walikuwa na kiwango cha wastani
  • mshambuliaji walijaaliwa kizazi bora (michael owen, wayne rooney, alan shearer, andy cole, robbie fowler)


kizazi hiki kilichoanzia world cup ya 2018 wamejaaliwa kuwa na kundi kubwa la vijana wenye vipaji kwa kila eneo (position), eneo pekee walilonyimwa mchezaji mwenye kiwango bora ni namba 8, laiti kama wangelikuwa na mchezaji mmoja anayefikiwa kiwango cha scholes, lampard au gerrard pengine tungelikuwa tunazungumza hadithi nyengine.

kwa miaka 10 hii waingereza wataendelea kuzalisha kundi kubwa sana la vijana wenye ari ya kucheza mpira kutokana na mikakati bora walioiwekana na kuitekeleza, jukumu lililobakia ni la benchi la ufundi wanatakiwa kuhakikisha wanaunganisha wachezaji hawa na kutengeneza strucuture inayoeleweka ya kiuchezaji kama walivyo spain haijalishi ni kocha yupi ameletwa kikosini.
 
Sir Alex Ferguson on the player he wished #mufc signed: "In reality, you have to say, the only one that always comes to my mind and that's Gascoigne. He was absolutely fantastic. I think if we'd have got him, he would have had a great career, I really do."

manutd |
#GGMU
 
Back
Top Bottom