GenuineMan
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 5,247
- 11,592
Hapo kwenye coaching staff umehit penyewe.Mechi ya Crystal Palace tulifungwa kwa ujinga wa benchi letu la ufundi, Paul alikuwa hana match fitness na hakuwepo ktk programs za timu kwa zaidi ya wiki tatu ali-train siku nne tu lakini wakamuanzisha. Upande wa beki Luke Shaw pia naye hakupaswa kuanza ahead ya Brandon naye hakuwa na match fitness compared to Brandon, kosa lingine kubwa sana hili ndilo lilotugharimu sana mpaka muda huu sijajua kigezo gani kilitumika kuwaanzisha Mensah na Daniel James badala ya Aaron na Mason?
Nina mashaka sana na uwezo wa kiakili wa benchi letu la ufundi hapa Ed (japo nae ni wale wale same WhatsApp group) anapaswa hata aongeze nguvu tutafute hata kocha msaidizi mpya Mike Phelan hafai hata kipindi cha Fergie baada ya kuondoka Carlos Queiroz tulianza kupwaya hana mipango, first team coaches we all know wote ni average tu Michael Carrick & Kieran McKenna.
Kuelekea kesho, golini anapaswa aanze Dean huyu yupo motivated sana na ana kiu ya kuji-prove wakati David kwa sasa anapambana kutuaminisha hajaisha, kulia Aaron arejee huyo Mensah akae benchi, kushoto Luke abaki, kati kati Harry na Eric yule mjinga Victor asikae hata bench, kiungo cha chini Nemanja arejee Scott akae bench, juu yake Bruno na Paul, na front 3 irejee ya siku zote Mason, Marcus na Anthony.
My lineup vs Brighton & Hove ; Dean Henderson , Aaron Wan Bissaka, Luke Shaw, Harry Maguire, Eric Bailly, Nemanja Matic, Bruno Fernandes, Paul Pogba, Mason Greenwood, Marcus Rashford na Anthony Martial.
Umemsahau msela wake na OLE, anaitwa Mark Dempsey.
Huyu walikuwa nae Molde. Wakaenda wote Cardiff city, then kaja nae Man U.