Kwahiyo baada ya hapo dirisha lifungwe tu! Yaani tumekuwa klabu ya kushangaza sana sijui tunalenga nini msimu huu!
Nadhani hata Solkjaer ameshaanza kuwa disappointed na hii hali.

Mpaka sasa wachezaji wake watatu wa kikosi cha kwanza hawataungana na timu mechi ya kwanza.

Pogba ana corona virus
Rashford injured
Greenwood ameitwa National team.
 
tapatalk_1598812929384.jpeg
 
Manchester United imefanya mazungumzo na Aston Villa wakati inajitahidi kufikia makubaliano ya mchezaji Muingereza Jack Grealish, 24. (Mail)
 
Manchester United imejiunga na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati ya Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 29. (Dagbladet TV, via Sun)
 
Mashabiki wameaminishwa kwamba Maguire hana shida ila shida ni Lindelof na wamekubali. Wote wanasema atafutwe CB wa kusaidiana na Maguire means Lindelof ni kiazi.

Tangu day one kwenye game ya Arsenal na Man U watu walitakiwa wajue Maguire hamna kitu. Aubameyang alipigiwa pasi, Maguire akamkimbia Auba. Auba akascore, ikasemwa ni offside marudio yakamuonyesha Maguire akikimbia majukumu yake.

Kisha amekuja na mtindo wa kumark team mates. Kona, faulo au krosi inapigwa yeye yuko busy kummark Bailly au Lindelof hii tabia ikasababisha amrukie kichwa Bailly mpaka akampasua, hapo Bailly alikua nje majeruhi kwa ajili ya kichwa hicho hicho, Maguire akamrudisha mwenzake majeruhi.

Mpira utapigwa kulia yeye ataangalia kushoto, online siku hizi kuna usemi unasema "No look defense" yaani ni kama 'No look pass' za Messi au Pogba au Ronaldo.

Uzuri mpira hauchezwi chumbani, unachezwa nje wote tunashuhudia. CB mpya atakuja halafu tutaona kama madai ya kwamba Lindelof ndiye tatizo ni ya kweli.

Mwingine ambaye ni kiazi ni Bisaka.

Mashabiki wanataka acheze kama attacking fullback wana hamu kali juu ya hili mpaka wanamfananisha na Arnold wa Liver lakini Bisaka hajui kupiga krosi wala faulo wala hana skills za kupangua watu. Kwa kifupi Bisaka hana tofauti na Young ambaye aliuzwa kwenda Inter.

Both suck as players. Lakini mashabiki utawasikia "Anapiga tackling hatari one on one humpiti" nikumbushe hizi justifications tulizisikia kwa nani vile? Kwa Ashley Young. The Captain. Na leo yupo Inter anacheza kama winger.

So waliposema aje CB wa kusaidiana na Maguire walimaanisha aje CB ambaye atafunika makosa ya Maguire siyo kusaidiana as they claimed.

Waweza nipinga ukiona nimekosea.
 
Hapa safi naona tumeanza ku-execute transfer plans very strategic, bado beki wa kati na mtu mmoja mbele tuimarishe timu. Japo kwa sasa napendelea tuongeze na mtu mwingine beki ya kushoto ile nafasi Luke Shaw hatufai kwa mipango ya muda mrefu. Tunahitaji mchezaji anayeweza kutupa mechi zisizopungua 30 za ligi kuu na angalau 15 na michuano mingine.
 
Back
Top Bottom