Unasema pogba alicheza vibaya? Ww unaangalia mechi gani?
Pogba amepangwa na mctominay ambaye hakuwa na msaada mkubwa sana kwake.. alipoteana pogba akawa amebaki kama yuko mwenyewe.. halaf unlaumu huku kiungo kilizidiwa.

Pogba ataonekana timu ikisajili kiungo mwenye uzoefu wa kucheza nae. Otherwise tutaendelea kuwa average.
Tatizo mna overambition. Scot so mbaya kiivo
 
Kukaba Sana sio sifa ya malegend vile vile, ukimtoa makelele na kidogo ngolo kante Ni nadra Sana kumkuta huyo mkabaji akiwa mchezaji mzuri Sana.

Juventus wanacheza na pirlo Kama no 6 Wala hakabi, Man U wanacheza na Carrick Kama no 6 Wala sio mkabaji Sana Kama Ndidi, bosquet wa Barcelona anapitwa na Ndidi ukabaji etc

Kuna wachezaji hawakabi ila Wana uwezo wa kuread mchezo, Wana instincts za kuzuia mashabulizi Bila kutumia minguvu, Wana control mechi hata Kama wapo nyuma etc.

Baada ya kusema hayo ukija kwenye stats website ya premier league Mc tominay ana tackling success 86% na Ndidi ana 65%, hivyo wachezaji Hawa wawili MCtominay ana chance kubwa ya kumpokonya adui mpira, sema Tu Ndidi amecheza mechi nyingi zaidi pengine ndio maana percentage zake Ni ndogo, ila still MCtominay si wa mchezo mchezo, alitoka na 100% tackle rate against Barcelona,
Ongeza na Joginyo
 
McTominay huwa anacomplete tackles ngapi per 90 mins? Tackle success rate hata Harry Winks huwa ana percentage nzuri ila njoo kwenye takwimu huwa anacomplete tackles ngapi per 90 mins ni kioja

Anyway anaweza kucheza namba 6 in lieu for Matic tatizo linakuja unapokutana na timu ambayo inaviungo wanaojua kudrible
 
Hio Hapo against Chelsea
Screenshot_20190813-102710__01.jpg
 
McTominay huwa anacomplete tackles ngapi per 90 mins? Tackle success rate hata Harry Winks huwa ana percentage nzuri ila njoo kwenye takwimu huwa anacomplete tackles ngapi per 90 mins ni kioja

Anyway anaweza kucheza namba 6 in lieu for Matic tatizo linakuja unapokutana na timu ambayo inaviungo wanaojua kudrible
Kuhusu viungo wanaojua kudrible Barcelona wanaqualify sio? Arthur, Rakitic kidogo na Hata Messi anasaidia kiungo.

Still Dogo pia aliregister perfect performance,
Screenshot_20190813-103410__01.jpg

Pia mechi ya psg against Kina Veratti
Screenshot_20190813-103713__01.jpg

Hizo zote Barca, Psg na Chelsea Ni mechi kubwa, na unaoona ana attempt Hadi tackling 5, Kama mtu anafanya Tackle 5 na zote anawin mpira tusemeje?

Na si tu tackling za miguu, ana almost 100% kwenye hizo mechi kwenye kuwin vichwa pia, anatumia vizuri urefu wake, Bila kusahau hizo recoveries na interception, na msimu uliopita Jamaa alikuwa anakimbia Kushinda average ya Timu, exactly quality anayoitaka Ole.
 
Kuhusu viungo wanaojua kudrible Barcelona wanaqualify sio? Arthur, Rakitic kidogo na Hata Messi anasaidia kiungo.

Still Dogo pia aliregister perfect performance,
View attachment 1180130

Pia mechi ya psg against Kina Veratti
View attachment 1180133

Hizo zote Barca, Psg na Chelsea Ni mechi kubwa, na unaoona ana attempt Hadi tackling 5, Kama mtu anafanya Tackle 5 na zote anawin mpira tusemeje?

Na si tu tackling za miguu, ana almost 100% kwenye hizo mechi kwenye kuwin vichwa pia, anatumia vizuri urefu wake, Bila kusahau hizo recoveries na interception, na msimu uliopita Jamaa alikuwa anakimbia Kushinda average ya Timu, exactly quality anayoitaka Ole.
Huyu dogo ni mad dog sema combination yake na Pogba huwa siyo rafiki sana
 
Mkuu naona upo upande wa MSIMAMO, jaribu kuwa flexible kwa kuangalia uhalisia

Sijui kwanini leo ghafla Chelsea imeonekana ni kipimo kinachotudanganya

Hivi ni kweli Chelsea ni wabovu kiasi hicho

Tulishinda mechi zote za Australia, watu wa kasema is just preseason, tukashinda dhidi ya Inter kisha Spurs ikaonekana is just pre season. Jana tumempiga Chelsea inaonekana ni timu dhaifu
kama nitakua sahihi mara ya mwisho kwa timu yetu kucheza dakika 90 bila ya kuruhusu goli ilikuwa ni mwezi februari hivyo basi kitendo cha kumaliza dakika 90 bila ya kufungwa goli haijalishi tunacheza na mbeya city kiupande wangu pia ni matokeo yalionifurahisha sana.

kivyovyote matokeo yale pia yamechangiwa kiupande fulani na mabadiliko tulioyafanya kwenye safu yetu ya ulinzi (ujio wa maguire na bissaka) kwa asilimia 50 bila ya kusahau ubora ule tuliouzoea kuushuhudia machoni mwetu mara kwa mara kutoka kwa david degea ambao msimu uliopita hatukuweza kuushuhudia

daniel james pia anaonekana yupo vizuri kiupande fulani na pengine inatokanwa zaidi na zawadi aliyopewa na muumba ya kujaaliwa speed and acceleration anapokuwa na mpira na hata asipokuwa na mpira, pace yake iliwapa tabu sana japo kwa muda mfupi mabeki wa chelsea jambo lililopelekea mlinzi mmoja apewe kadi ya njano, kikubwa anachopaswa kukifanyia kazi ni utulivu ili afikie level za gareth bale, kama ataendelea kukosa utulivu mwisho wa siku atajikuta anafuata nyayo za aron lennon, wright phillips au theo walcott.

jambo kubwa linalonifanya nisifurahishwe sana na hali iliopo sasa (kuendelea kuwa na msimamo) kwenye klabu yetu ni ikitendo cha klabu kuipoteza nafasi adhimu ya kujenga timu imara kwa kutumia dirisha moja tu la usajili kama wanavyofanya au walivyowahi kufanya baadhi ya wapinzani wetu (rejea usajili wa man city miaka miwili iliopita, liverpool mwaka uliopita, usajili wa spurs na real madrid msimu huu)

hata ukizisoma comment za wadau wengi humu ndani hata wale wanaosifia kiwango hicho kizuri tulichokionyesha kama inavyosemwa kwenye mechi ya chelsea pia utagundua ya kwamba wengi wao baadae wanarudi tena maeneo yale yale tunayoyalalamikia tokea msimu uliopita si ajabu utakuta mchangiaji ana andika:

midfield bado ipo ovyo inahitaji mabadiliko
bado hatupo vizuri kwenye eneo la umaliziaji kwani tunakosa utulivu tukifika mbele (clinicalness)
tunakosa kiungo wa kuongeza wigo wa ubunifu kama alionao pogba
bado hatupo vizuri eneo la kiungo ukabaji tunaruhusu ovyo
luke shaw anampa kazi kubwa sana maguire ya kumlinda n.k​

ukiangalia kwa umakini matatizo mengi yanayoelezwa unajifunza ya kwamba kumbe kunahitajika jitihada kubwa sana kupitia benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenyewe kuyatatua jambo ambalo si rahisi kuyatatua na kama ingelikuwa ni rahisi basi yangelikwisha tatuliwa tokea msimu uliopita alioanza kazi OGS au tokea mwezi uliopita (yalipoanza mazoezi na preseason) ndio maana naendelea kuwa na msimamo wa kuamini ya kwamba njia pekee ya kutatua baadhi ya matatizo hayo ni kufanya usajili ambao kwa makusudi tumeupotezea.

  • ninavyoamini mimi ni rahisi kumsajili bruno fernandez kwa dau kubwa baadae ukamsubiri ayazoee mazingira ya uingereza kuliko kuendelea kumsubiri andreas perreira abadilishe kiwango chake cha uchezaji mpaka kuwa na kiwango kinachokaribiana na bruno fernandez
  • ninavyoamini mimi ni rahisi kumsajili kiungo mfano wa james madison kwa dau kubwa baadae ukamsubiri aizoee style ya uchezaji ya klabu yetu kuliko kuendelea kumsubiri jesse lingard abadilishe style yake ya uchezaji ya kutoka kiungo asiyetengeneza nafasi ya goli mpaka kuwa kiungo anayetengeneza angalau nafasi 50 za magoli kwa msimu ukilinganisha na nafasi 100 alizotengeneza james maddison msimu uliopita akiwa na leicester city. Kama tungelifanikisha mfano wa target mbili hizi basi tungelikuwa na jeuri ya kucheza na timu kubwa yeyote duniani.​

halafu mkuu situations iliopo chelsea msimu huu ndio inayopelekea baadhi yetu tuamini ya kwamba chelsea si kipimo tosha cha kuifanyia tathimini klabu yetu kiubora. Naamini laiti kama chelsea wangelipata nafasi hii adhimu ya kusajili wachezaji kwenye dirisha lililoisha basi wangelifanya mabadiliko makubwa sana ya wachezaji kuliko tulivyofanya sisi kufuatia kuondoka kwa wachezaji wao muhimu mfano hazard, morata, david luiz, majeruhi ya wachezaji, bila ya kusahau kuondoka kwa gary cahill aliyemaliza mkataba wake.

nimeanza kuwa na majonzi kwa yale ninayoyashuhudia kwenye hii thread kuanzia siku chache zilizopita, nimeanza kunusa harufu ya kulazimisha uwepo wa mijadala inayofanana na ndege aina ya kasuku, ndege huyu inasemekana amejaaliwa uwezo wa kuweza kunukuu yale yanayozungumzwa na wengineo bila ya kuyafanyia tafakari ya kina, kwa sisi binadamu kuiga tabia hiyo tutakuwa tunabomoa na si kujenga endapo tutalazimisha sote tuwe na mawazo sawa humu ndani.

Naomba hii tabia ya ukasuku ibaki kule kwenye jukwaa la siasa na si humu ndani, jukwaa la siasa ndio utakutana na mpenzi wa chadema kwa zuri na baya vile vile utakutana na mshabiki wa ccm kwa zuri na baya lenye athari kwa wenzake.
GGMU
 
Mkuu hizi siku mbili umejifungia ndani. Ukajipiga ban kabisa. Nilikwambia na nitakwambia tena hamna uwezo.
Hakuna cha refa.. wala cha nn. Chelsea mlikosa mipango endelevu. Katikati mko vizur. Mbele na drfence hovyo.
Kumiliki mpira si magoli.. na mkikaa vibaya mnakuwa kama arsenal. Hao watoto si wa kuwaamini sana
Refa kawabeba sana hongereni kwa ushindi wenu wa kwanza ..

Magwaya na Bissaka bado hawaja improve chochote, ni gemu tu ilikuwa upande wenu..

#TukutaneDarajani
 
Kwa muono wangu mdogo, Maguire naona bado sana na mtakuja kumtukana ,mtu pekee ambaye mmepata ni Bisaka , huyu jamaa ana pandisha timu anakaba pia , ila kwakuwa mlishinda 4-0 ,basi Maguire anajificha kwenye takwimu ,ila tukija reality Maguire ni mzito ,hivo akikutana na viberenge au mchezo wa kasi sana ,anapotea ,hili wana man u wengi hamtaki kulisikia ,lakini muda utasema

Niungane na raisi wa Napoli aliyesema thaman ya Maguire ni £30-35m , natoa mech 5 ,mtakuja hapa kutafuta mchawi ni nani

Hebu fikiria Chelsea mbovu hii isiyo na matumain ya hata ya nafasi ya 10 ,ilikuwa ibatengeneza nafas clear mbele ya Maguire ,kinachoficha udhaifu niliouona kwa Maguire ni takwimu za hapa na pale ambazo hizo takwimu hata beki mbovu Mustafi au lovren wanazo kuzidi Maguire ,hivo wana manchesta msijipe moyo na matarajio makubwa kwa magwaya .

Kwa Bisaka sina neno ana kila kitu ambacho FB anatakiwa awe nacho, ila Maguire mhhh muda utasema.
 
Back
Top Bottom