Manchester United F.C:Historia ndefu yenye kusisimua!

Manchester United ni kilabu cha kandanda cha
Uingereza, ambacho ni mojawapo ya vilabu
maarufu sana ulimwenguni, na kina makao
katika Old Trafford eneo la Greater Manchester.
Kilabu hiki kilikuwa mwanachama mwanzilishi
wa Ligi ya Primia mwaka 1992, na kimeshiriki
katika divisheni ya juu ya kandanda ya
Uingereza tangu mwaka wa 1938 , isipokuwa
msimu wa 1974-75. Mahudhurio ya wastani
kwenye kilabu yamekuwa ya juu kuliko timu
nyingine yoyote katika kandanda ya Uingereza
kwa misimu yote isipokuwa sita tangu
1964-65. [1]
Manchester United ndiyo bingwa wa sasa wa
Uingireza na washikilizi wa Kombe la Dunia la
Vilabu, baada ya kushinda Ligi ya Primia
2008-09 na Kombe la Dunia la FIFA . Kilabu hicho
ni miongoni mwa vilabu vyenye ufanisi mkubwa
katika historia ya kandanda ya Uingereza na
kimeshinda mataji makubwa 22 tangu Alex
Ferguson alipochukua wadhifa wa meneja wake
mnamo Novemba 1986. Mwaka wa 1968,
kilikuwa kilabu cha kwanza kushinda Kombe la
Uropa kwa kucharaza Benfica 4-1. Walishinda
kombe la pili la Ulaya kama sehemu ya ushindi
wa mataji matatu mwaka 1999, na la tatu mwaka
wa 2008, kabla ya kumaliza katika nafasi ya pili
mwaka wa cha 2009. Kilabu hicho kinashikilia
rekodi mbili ya kushinda mataji mengi ya Ligi ya
Uingereza mara 18 na pia kushikilia rekodi kwa
wingi wa kutwaa kombe la FA ikiwa imeshinda
mara 11. [2]
Tangu mwisho wa mwaka ya 1990, kilabu hicho
kimekuwa mojawapo ya vilabu tajiri duniani
kilicho na mapato ya juu kuliko kilabu
chochote, [3] na sasa kinatajwa kama kilabu
chenye thamani zaidi katika mchezo wowote, na
makisio ya thamana ya takriban bilioni £ 1.136
(bilioni € 1.319 ) Aprili 2009. [4] Manchester
United ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa
kundi la vilabu la G-14 la Vilabu kuu vya
kandanda Uingereza, ambalo halipo tena, na
European Club Association, muungano
uliochukua nafasi yake. [5]
Alex Ferguson amekuwa meneja wa kilabu hicho
tangu 6 Novemba 1986 alipojiunga na kilabu
hicho kutoka Aberdeen baada ya kung'atuka kwa
Ron Atkinson. [6] Nahodha wa kilabu wa sasa ni
Garry Neville, aliyechukua nafasi ya Roy Keane
Novemba 2005. [7]
Historia
Miaka ya mwanzo(1878–t 555)
Chati inayoonyesha maendeleo ya
Manchester United F.C katika mfumo wa
ligi ya kandanda Uingereza tangu kujiunga
kama Newton Heath mwaka 1892-93 kwa
sasa
Kilabu kilianzishwa kikijulikana kama Newton
Heath L & YR F.C. mwaka wa 1878 kama timu
ya kazi ya bohari la Reli la Lancashire na
Yorkshire huko Newton Heath. Mashati ya kilabu
hiyo yalikuwa ya kijani na nusu dhahabu.
Walicheza kwenye uwanja mdogo, uliochakaa
huko North Road kwa miaka kumi na mitano,
kabla ya kuhamia Bank Street katika mji wa
karibu wa Clayton mwaka wa 1893. Kilabu
kilikuwa kimeingia ligi ya kandanda ya Football
Leagu mwaka uliotangulia na kuanza kukatiza
uhusiano wake na bohari la reli, na ikawa
kampuni ya kujitegemea, ikimteua katibu wa
kilabu na kudondoasha herufi “L&YR” kutoka jina
lao na kujiita Newton Heath F.C. Muda mrefu
haukupita, mwaka 1902, kilabu kilikaribia
kufilisika, kikawa na madeni ya zaidi ya £2,500.
Wakati mmoja, uwanja wao wa Bank Street
ulifungwa na wadai wao. [8]
Kabla ya kufungwa kabisa, kilabu kilipokea
uwekezaji mkubwa kutoka kwa J. H. Davies,
mkurugenzi mtendaji wa Manchester
Breweries. [9] Kuna tetesi kuwa Harry Stafford,
nahodha wa kilabu alikuwa akijivunia mbwa
wake wa thamani wa aina ya St. Bernard katika
mkutano wa kuchangishia kilabu fedha, wakati
Davies alipomwendea ili kumnunua mbwa huyo.
Stafford alikataa, lakini aliweza kumshawishi
Davies kuwekeza katika kilabu na kuwa
mwenyekiti wake. [10] Iliamuliwa katika kikao
cha bodi ya mapema kuwa kilabu kilihitaji
kubadilishwa jina ili kuashiria mwanzo huo
mpya. Manchester Central na Manchester Celtic
ni miongoni mwa majina yaliopendekezwa kabla
ya Louis Rocca, mhamiaji mchanga kutoka Italy
aliposema "Ndugu zangu, mbona tusijiite
Manchester united?"[11] Jina hilo lilibakia hivyo,
na Manchester United likawa jina rasmi tarehe
26 Aprili 1902. Davies pia aliamua itakuwa
vyema kubadili rangi za kilabu, walitupilia
mbalirangi za kijani na nusu dhahabu za Newton
Health na kuchagua nyekundu na nyeupe kuwa
rangi za Manchester United.
Ernest Mangnall aliteuliwa kama katibu wa kilabu
baada ya James West ambaye alikuwa
amejiizulu kama meneja tarehe 28 Septemba
1902. Mangnall alitwikwa jukumu la kujitahidi
kukifika kilabu kwenye Divisheni ya kwanza, na
kushindwa kidogo tu katika jaribio la kwanza
kusudio hilo kwa jaribuio la, walipomaliza katika
nafasi ya tano katika Divisheni ya pili. Mangnall
aliamua kwamba ilikuwa muhimu kuleta
machipukizi katika klabu, na kuwasajili
wachezaji kama vile Harry Moger katika lango,
Dick Duckworth, beki wa nyuma na Jack Picken
mbele lakini ilikuwa na beki wa nyuma mwingine
kwa jina la Charlie Roberts aliyeleta mabadiliko
makubwa. Alinunuliwa kwa £750 kutoka
Grimsby Town Aprili 1904, na kuisaidi klabu
kumaliza msimu wa 1903-04 kikiwa kimekosa
alama moja tu kipandishwe ngazi iliyofuata.
Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu, kilabu
kilipandishwa cheo hadi Divisheni ya Kwanza
kwa mara ya kwanza chini ya jina mpya na
kumaliza katika nafasi ya pili katika Divisheni ya
Pili mwaka wa 1905-06. Msimu wa kujiiimarisha
ulifuatia, huku kilabu ikimaliza katika nafasi ya
nane, kabla ya kutwaa taji lao la kwanza la ligi
mwaka wa 1908. Katika siku za
karibuni,Manchester City ilikuwa ikichunguzwa
kwa kuwalipa baadhi ya wachezaji wao
mshahara uliozidi kiwango kilichopendekezwa na
masharti ya FA. Walipigwa faini ya £250 na
wachezaji wao kumi na wanane wakapigwa
marufuku kuwachezea tena. United hawakusita
kukabiliana na hali hiyo na kuwatwaa Billy
Meredith (almaarufu Welsh Wizard) na Sandy
Turnbull, miongoni mwa wengine. Vijana hao
wageni kutoka mji jirani hawakuruhusiwa
kucheza hadi tarehe mosi mwaka wa 1907, kwa
sababu ya marufuku yao, kwa hivyo hatua hiyo
iliahirishwa hadi msimu wa 1907-08 ili waweze
kuendeleza jitihada za united kutwaa taji. Na hilo
walifanya, walianza kampeni yao kwa kishindo
kwa kuishinda Sheffield United 2-1 na kuanzisha
msururu wa ushindi mfululilizo mara kumi. Licha
ya msimu kuonekana wenye tatizo mwishoni,
United ilifaulu kushikilia na kumaliza msimu kwa
pointi tisa mbele ya wapinzani wao wa karibu
Aston Villa.
Msimu uliofuatia ulianza kwa United kujitwalia
fedha nyingine, Charity Shield,[12] ambayo
ilikuwa ya kwanza kuwahi kutolewa na kumalizia
kwa taji jingine, taji la kwanza kwa kilabu cha FA,
ambalo lilipanda mbegu njema ya kile kimekuwa
rekodi ya mataji ya FA. Jinsi walivyokuwa katika
kampeni ya taji la kwanza la klabu, Turnbull na
Meredith walikuwa na umuhimu katika msimu
huu, Turnbull akifunga bao la ushindi katika
Finali ya kombe la FA. Ilibidi Klabu kusubiri
miaka mingine miwili kabla ya kushinda
makombe mengine zaidi, kilishinda Divisheni ya
Kwanza kwa mara ya pili katika msimu wa
1910-11. Wakati huo huo, United ilihamia uga
wao mpy wa Old Trafford. Walichezea
mmchuano wao wa kwanza huko tarehe 19
Februari 1910 dhidi ya Liverpool, lakini
wakapoteza 4-3 baada ya kupoteza ushindi wao
wa 3-0. Kisha wakasalia bila kombe tena katika
msimu wa 1911-12, ambao haukuwa tu wa
mwisho kwa Mangnall kuhusikia (alihamia
Manchester City baada ya miaka kumi na
United), lakini pia wakati wa mwisho kwa klabu
kushinda Divisheni ya Kwanza baada ya miaka
41, muda mrefu zaidi ambao klabu imekaa bila
kushinda ligi katika historia yake.
Kwa miaka kumi iliyofuata, klabu kilishuhudia
hali ya kudidimia polepole kabla ya kushushwa
ngazi ya chini, Division ya pili katika 1922.
Walipandishwa ngazi tena mwaka 1925,
wakang'ang'ana kufika nusu ya msimamo wa
ligi, na wakashushwa ngazi tena mwaka wa
1931. Katika miaka minane iliyotangulia Vita vya
Pili vya Dunia, klabu kilididimia na kuwa klabu
yo-yo, kikafikia kiwango chao cha chini zaidi
cha nafasi ya 20 katika Divisheni ya Pili mwaka
wa 1934. Walipandishwa tena katika msimu wa
mwisho kabla ya Vita vya Pili vya Dunia.
Walijihakikishia nafasi yao katika kiwango cha
juu baada ya vita kwa kumaliza katika nafasi ya
14 katika msimu wa 1938-39.
Kipindi cha Busby (1945-1969)
1945 ilishuhudia kuteuliwa kwa Matt Busby kuwa
msimamizi katika Old Trafford. Alitumia mtindo
usio wa kawaida kufanya kazi yake, akisisitiza
kuwa aruhusiwe kuchagua timu yake
mwenyewe, kuchagua wachezaji atakaowaajiri
na kuwafunza mwenyewe. Mwenyewe alikuwa
tayari amepoteza kazi ya usimamizi kwenye
kilabu chake cha awali, Liverpool, kwa sababu
klabu kiliona kazi hizo kama za wakurugenzi
lakini United ikaamua kujaribu mawazo bunifu ya
Busby. Wa kwanza kusajiliwa na Busby hakuwa
mchezaji, bali meneja msaidizi mpya kwa jina la
Jimmy Murphy. Hatua hatari ambayo klabu
ilichukulia kumteua Bushy ilileta mazao ya mara
moja, klabu kilipomaliza katika nafasi ya pili
katika ligi ya 1947, 1483 na 1949 na kushinda
kombe la FA 1948, kutokana na juhudi za wazao
wa hapo watatu, Stan Pearson, Jack Rowley na
Charlie Mitten (Rowley na Pearson walifunga
katika fainali ya kombe la 1948), na pia kiungo
wa kati kutoka Kazini Mashariki, Allenby Chilton.
Charlie Mitten alikuwa amekimbilia Kolombia
kutafuta mshahara bora,lakini wachezaji
waliobaki waliweza kushinda taji la Divisheni ya
Kwanza baadaye mwaka 1952. Hata hivyo,
Busby alijua kwamba timu za kandanda zilihitaji
zaidi ya tajriba, kwa hivyo alitumia sera ya kuleta
wachezaji kutoka katika timu ya vijana pale
ilipowezekana. Mara ya kwanza, wachezaji
wachanga kama vile Roger Byrne, Bill Foulkes,
Mark Jones na Dennis Viollet, walichukua muda
kuzoea timu kuu, na kuteremka hadi nafasi ya
nane mwaka 1956, lakini timu hiyo ilishinda ligi
tena katika mwaka wa 1956 kwa umri wa
wastani miaka 22 tu, na kufunga mabao 103
wakati huo. Sera ya kuteua vijana iliyowekwa na
Busby sasa imekuwa fadhila mahususi kwa
vipindi vilivyofanikiwa zaidi katika historia ya
klabu (katikati ya 1950, kati na mwisho wa
miaka ya 1960 na miak 1990). Kundi asilia la
vijana wachezaji lilijulikana kama Busby Babes,
ambapo aliyevuma sana alikuwa kiungo wa
pembeni Duncan Edwards. Kijana huyo kutoka
Dudley, West Midlands aliichezea United kwa
mara ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka
16 tu mwaka 1953. Ilisemekana kuwa Edwards
angeweza kucheza katika nafasi yoyote
uwanjani, na wengi waliomwona akicheza
walisema kuwa yeye ndiye alikuwa mchezaji
maarufu kabisa katika historia ya mchezo huo.
Msimu uliofuata, 1956-57, walishinda ligi tena na
kufikia fainali ya Kombe la FA, na kupoteza kwa
Aston Villa. Pia ilikuwa timu ya kwanza ya
Uingereza kushindana katika kombe la Uropa,
kwa amri ya FA, ambayo ilikuwa imeiinyima
Chelsea fursa sawa na hiyo msimu uliotangulia,
na kufika nusu fainali kabla ya kung'olewa na
Real Madrid. Ikielekea nusu fainali hizo, United
pia iliacha rekodi kwa ushindi ambayo bado ipo
kama washindi wakuu katika mashindano yote,
kwa kuwachapa mabingwa wa Ubelgiji
Anderlecht mabao 10-0 ugani Maine Road.
Bamba la taarifa Old Trafford kwa
heshima ya wachezaji walikufa katika
ajali ya ndege ya Munich.
Janga liliikumba msimu uliofuata, wakati ndege
iliyokuwa imewabeba wachezaji kurejea
nyumbani kutoka mchuano wa European Cup
ilipoanguka pindi ilipoanza kupaa baada ya kutua
kujaza mafuta huko Munich, Ujerumani. Ajali hiyo
ya ndege Munich ya 6 Februari 1958 ilisababisha
vifo vya wachezaji - Geoff Bent, Roger Byrne,
Eddie Colman, Duncan Edwards, Marko Jones,
Daudi Pegg, Tommy Taylor na Liam "Billy"
Whelan - na abiria wengine kumi na watano,
pamoja na wafanyikazi wa United Walter
Crickmer, Bert Whalley na Tom Curry. [13] Tayari
kulikuwa na majaribio mawili ya kupaa kabla hilo
la tatu lililoishia maafa, lilisababishwa na
kujazana kwa tope mwishoni mwa barabara ya
ndege na hivyo kupunguza kasi ya ndege hadi
kiwango kisichotosha kupaa. Ndege iliteleza nje
ya mwishoni mwa barabara ya kupaa, kupitia
uani na kuingia katika nyumba ambazo hazikuwa
na watu watu. Mlindalango wa United Harry
Gregg alifanikiwa kutozirai baada ya ajali, na kwa
kuhofia kulipuka kwa ndege wakati wowote,
aliwakamata Bobby Charlton-ambaye alikuwa
ameichezea United mechi yake ya kwanza
kabisa miezi 18 tu iliyopita – na Denni Viollet
viunoni na kuwavuta mahali salama. Wachezaji 7
wa United walikufa katika eneo la tukio, huku
Duncan Edwards akifa majuma mawili baadaye
hospitalini. Wing'a wa kulia Johnny Berry pia
alinusurika ajali hiyo, lakini majeraha aliyopata
kwenye ajali yalisitisha ghafla uchezaji wa
kandanda. Matt Busby hakutumainiwa kuishi
zaidi na madaktari wa Munich na wakati mmoja
alifanyiwa Maombi ya Mwisho, lakini alipata
afueni kimiujiza na hatimaye aliruhusiwa kutoka
hospitalini baada ya kulazwa kwa zaidi ya miezi
miwili.
Kulikuwa na uvumi kuwa klabu ingefilisika na
kujiondoa kutoka mashindano yote, lakini Jimmy
Murphy aliposhikilia usukani kama meneja huku
Busby akiendelea kupona majeraha, klabu
kiliendelea kucheza kwa timu hafifu. Licha ya
ajali hiyo, walifika fainali ya kombe la FA tena,
ambapo walipoteza dhidi ya Bolton Wanderers.
Mwishoni mwa msimu, UEFA iliipa FA nafasi ya
kuwasilisha United na mabingwa wa msimu
Wolverhampton Wanderers, kushiriki kombe la
Uropa mwaka 1958-59 kama heshima kwa
waathiriwa lakini FA ilikataa. United ilimudu
kuikaba Wolves koo msimu uliofuata, huku
ikimaliza katika nafasi ya kuridhisha ya pili;
haikuwa mbaya kwa timu iliyokuwa imepoteza
wachezaji tisa katika ajali ya ndege ya Munich.
Busby aliijenga upya tena timu hiyo mapema
miaka ya 1960, akisajili wachezaji kama vile
Denis Law na Pat Crerand, wakati huo huo akilea
kizazi chake kipya cha vijana chipukizi. Huenda
maarufu zaidi katika kundi hili jipya alikuwa
kijana kutoka Belfast aliyeitwa George Best. Best
alikuwa na uanariadha wa kipekee , lakini kipawa
chake cha thamani zaidi kilikuwa kudhibiti mpira.
Miguu yake ya kasi ilimruhusu kupenya kwenye
mwanya wowote katika ngome ya wapinzani,
hata uwe mdogo kiasi gani. Timu hiyo ilitwaa
Kombe la FA mwaka wa 1963, ingawa ilimaliza
katika nafasi ya 19 katika Daraja la Kwanza.
Shangwe za ushindi wa Kombe la FA zilionekana
kuwaimarisha wachezaji, waliosaidia klabu
kufikia nafasi ya pili 1964, na kuimarika zaidi
kwa kushinda ligi katika mwaka wa 1965 na
1967. United ilishinda kombe la Uropa 1968 kwa
kuinyuka Eusébio's Benfica 4-1 kwenye fainali
na kuwa kilabu cha kwanza Uingereza kushinda
shindano hilo. Timu hii ya United ilikuwa maarufu
kwa kuwa na wanakandanda watatu bora wa
Mwaka barani Uropa: Bobby Charlton, Denis Law
na George Best. Matt Busby alijiuzulu kama
meneja 1969 na nafasi yake kuchukuliwa na
kocha wa akiba na pia aliyekuwa mchezaji wa
United, Wilf McGuinness.
1969-1986
United ilijitahidi kujaza nafasi ya Busby, na timu
ilitatizika chini ya Wilf McGunness katika msimu
wa 1969-70, ilipomaliza katika nafasi ya
kukatisha tamaa ya nane, na kufuatiwa na
kuanza vibaya katika msimu wa 1970-1971,
McGunnies alishushwa madaraka na kuwa
kocha wa timu ya akiba. Busby alishawishwa
kurudi klabuni, japo kwa miezi sita pekee.
Matokeo yalikuwa bora chini ya uongozi wa
Busby, lakini hatimaye aliondoka klabuni kwa
mara ya mwisho katika majira ya joto ya 1971.
Hayo yakijiri, United ilikuwa imewapoteza
wachezaji wa hali ya juu kama Nobby Stiles na
Pat Crerand.
Licha ya kumwomba maneja aliyeiongoza Celtic
kushinda kombe la Uropa Jock Stein, kuwa
meneja wake, Stein alikubali kwa mkataba wa
mazungumzo kujiunga na United, lakini akaghairi
msimamo dakika za mwisho- Frank O’Farrell
aliteuliwa kumrithi Busby. Hata hivyo, kama Mc
Guinness, O’Farrell alidumu chini ya miezi 18,
tofauti kati ya wawili hao ni kuwa O’Farrell
aliitikia matokea ya timu yasiyo ya kuridhisha
kwa kuleta vipaji vipya, wakutajika hasa ni
Martini Buchaman kutoka Aberdeen kwa malipo
ya £125,000. Tommy Docherty akawa meneja
mwishoni mwa 1972. Docherty, au "Doc",
aliiokoa United kutoshushwa ngazi msimu huo
lakini walishushwa mwaka 1974, wakati ambapo
nyota watatu , Best, Law na Charlton walikuwa
wamekihama klabu. Denis Law alikuwa
amehamia Manchester City katika majira ya joto
ya 1973, na kuishia kufunga bao ambalo watu
wengi husema liliishusha ngazi ya United, kwa
adabu alikataa kusherehekea pamoja na
wanatimu wenzake. Wachezaji kama vile Lou
Macari, Stewart Houston na Brian Greenhoff
waliletwa kuchukua nafasi za Best, Law na
Charlton lakini hakuna aliyefikia kimo cha watatu
hao waliotangulia.
Timu iliweza kupandishwa ngazi katika jaribio la
kwanza, huku kijana Steve Coppell akishiriki
mchuano wake wa kwanza kuelekea mwisho wa
msimu baada ya kujiunga na klabu kutoka
Tranmere Rovers na kufika fainali za Kombe la
FA mwaka 1976, lakini walishindwa na
Southampton. Walifika fainali tena mwaka 1977,
walipoishinda Liverpool 2-1. Pamoja na
mafanikio na umaarufu wake miongoni mwa
mashabiki, Docherty alipigwa kalamu mara
baada ya fainali ilipopatikana kuwa alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtaalamu wa
tibamaungo (physiotherapist).
Dave Sexton alichukua nafasi ya Docherty kama
meneja katika majira ya joto ya 1977 na kuifanya
timu kucheza mtindo wa kujihami zaidi. Mtindo
huu haukupendwa na mashabiki ambao
walikuwa wamezoea mtindo wa kandanda ya
kushambulia iliyopendelewa na Docherty na
Busby. Usajili mkuu wa wachezaji uliofanyika
chini ya Sexton ulihusisha Joe Jordan , Gordon
McQueen, Gary Baileyna na Ray Wilkins lakini
kwa sababu ya mtindo wa kujihamu wa Sexton,
United ilishindwa kutoka katika safu ya kati
isipokuwa mara moja tu, ilipomaliza katika nafasi
ya timu mbili bora na ikaweza kufikia finali ya
kombe la F.A mara moja, ilipoteza kwa timu ya
Arsenal. Kwa sababu ya ukosefu huu wa
vikombe, Sexton alifutwa mwaka wa 1981,
ingawa alikuwa ameshinda michuano yake yote
saba ya mwisho.
Nafasi yake ilichukuliwa na mshaufu Ron
Atkinson ambaye fikra zake za ucheshi
zilidhihirika katika vilabu alivyosimamia. Mara
moja alivunja rekodi ya Uingereza ya ada ya
uhamisho kwa kumsajili Bryan Robson kutoka
klabu yake ya zamani, West Bromwich Albion.
Robson aliibuka kuwa kile wengi[ who?]
walifikiria kuwa mchezaji bora kiungo cha kati
wa United tangu Duncan Edwards. Timu ya
Atkinson iliweza kushuhudia usajili mpya wa
wachezaji kama vile Jesper Olsen, Paul McGrath
na Gordon Strachan ambao walicheza na
wliokuwa wachezaji wa timu ya vijana
wakiwemo Norman Whiteside na Mark Hughes.
United ilishinda Kombe la FA mara mbili katika
miaka mitatu, katika mwaka wa 1983 na 1985,
walipigiwa upatu kushinda Ligi katika msimu wa
1985-86 kabla ya kushinda mechi zao kumi za
kwanza ligini jambo lililopelekea kuwepo na
tofauti ya pointi kumi kati yao na wapinzani wao
mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba. Hata hivyo,
muundo wa timu uliporomoka na United
ikamaliza msimu huo katika nafasi ya nne.
Uhafifu wa timu uliendelea katika msimu
uliofuata, na United ilikuwa ikichungulia
kushushwa ngazi kuanzia mwanzo wa Novemba
1986, Atkinson alifutwa.
Enzi ya Alex Ferguson, Kabla ya-
Treble [1986-1998]
Alex Ferguson amekuwa meneja wa
Manchester United tangu Novemba 1986.
Alex Ferguson aliwasili kutoka Aberdeen
kuchukua nafasi ya Atkinson siku hiyo hiyo
aliyofutwa Atkinson, alikuja pamoja na meneja
msaidizi wake, Archie Knox. Ingawa mechi yake
ya kwanza uongozini, dhidi ya Oxford United
tarehe 8 Novemba 1986 alishindwa 2-0,
Ferguson aliiongoza klabu kumalizia nafasi ya 11
katika ligi. Kumaliza katika nafasi ya pili
1987-88, pamoja na Brian McClair kuwa
mchezaji wa kwanza wa United tangu George
Best na kufunga mabao ishirini katika msimu wa
ligi, huenda kuliwafanya mashabiki kuwa na
matumaini kidogo kwa siku za usoni lakini
walirejelea haraka uhafifu kwa kumalizia nafasi
ya 11 mwaka 1989.
Wachezaji wengi waliosajiliwa na Ferguson
hawakufikia matarajio ya mashabiki, na meneja
iliripotiwa nusura aachishwe kazi mwanzoni
mwa 1990, wengi waliamini kwamba kushindwa
kwao na Nottingham Forest katika duru ya tatu
ya Kombe la FA kungetia muhuri hatma yake.
Bao la Marko Robins kunako dakika 56
liliiwezesha United kushinda mchuano huo na
kuwaweka katika king'ang'anyiro
kilichowapeleka hadi fainali iliyofanyika
Wembley, ambapo waliitinga Crystal Palace 1-0
katika mchuano wa marudio baada ya sare ya
3-3 katika mechi ya awali. Mwaka uliofuata,
United ilifika fainali ya League Cup na kupoteza
kwa bao 1-0 kwa timu ya aliyekuwa meneja wao
Ron Atkinson Sheffield Wednesday. Hata hivyo,
msimu ulimalizika kwa ushindi wa kwanza wa
Kombe la Washindi wa Vilabu (Cup Winners
'Cup), walipoiadhibu Barcelona 2-1 katika fainali
ugani Rotterdam. Ushindi wa taji la Cup Winners
uliiruhusu timu kucheza katika UEFA Super Cup
mwaka 1991 ambapo waaliwashinda waliokuwa
washindi wa Kombe la Ulaya Red Star Belgrade
1-0 uwanjani Old Trafford. Mechi hiyo ilipaswa
kuchezwa kwa michuano miwili lakini kutokana
na ukosefu wa utulivu wa kisiasa nchini
Yugoslavia wakati huo, UEFA iliamua kwamba
mchuano wa Old Trafford tu ndio utakaochezwa.
Kushiriki kwa mara ya pili mfululizo katika fainali
ya kombe la Ligi kulitokea mwaka 1992, United
wakati huo iliifunga Nottingham Forest 1-0 ugani
Wembley.
Wakati huo huo, matukio yalikuwa yakiendelea
nje ya uwanja mwishoni mwa mwongo, huku
mwenyekiti Martin Edwards akijaribu kuiuza
klabu kwa mkwasi Michael Knighton mwaka
1989. Uuzaji huo wa milioni £20 ulikuwa karibu
kuthibitishwa huku Knighton akiingia Old Trafford
akiwa na sare ya Manchester United na akifanya
mbwembwe kadha kabla ya kuvurumisha mpira
kuelekea langoni upande wa Stretford ugani
humo. Knighton aliweza kuona rekodi za kifedha
za klabu, lakini, kabla ya mkataba wa uuzaji
kukamilishwa washauri wake wa kifedha
walikataa na mpango huo ukafutiliwa. Hata
hivyo, kwa kuwa Knighton alikuwa na ufahamu
wa jinsi mambo yalivyokuwa yakiendeshwa
klabuni, alipewa wadhifa katika bodi ya klabu
kama njia ya kumfanya kubaki kimya kuhusu
jambo hilo. Mwaka 1991, ikihitaji msaada zaidi
wa kifedha kufuatia Ripoti ya Taylor klabu ilianza
uuzaji katika Soko la Hisa la London kwa
thamana iliyokisiwa kuwa paundi milioni 47, na
kuleta katika macho ya umma hali yake ya
kifedha. Martin Edwards alihifadhi wadhifa wake
kama mwenyekiti, lakini sasa klabu ilikuwa
ikimilikiwa na umma.
Majira ya joto ya mwaka 1991 pia yalishuhudia
kuwasili kwa mlindalango raiya wa Denmak
Peter Schmeichel, ambaye kutofungwa kwake
katika michuano 17 kuliipa United rekodi bora ya
kujihami katika Divisheni ya kwanza msimu wa
1991-92na kuwasaidia kumaliza katika nafasi ya
pili nyuma ya Leeds United, ndani ya safu hizo
kulikuwa na sogora fulani Mfaransa aliyeitwa
Eric Cantona. Alex Ferguson alitambua haja ya
United ya kuwa na mshambulizi kama njia ya
kumzuia Mark Hughes na Brian McClair na
alijaribu - na kushindwa - mara kadhaa kumsajili
mshambuliaji wa Sheffield Wednesday David
Hirst, lakini wakati meneja wa Leeds Howard
Wilkinson alipompigia Martin Edwards mwezi
Novemba 1992 kuuliza kuhusu uwezekano wa
kupatikana kwa Denis Irwin, mazungumzo hayo
yaligeuka haraka na kumhusu Cantona. Kwa
mshangao wa Edward na Ferguson, vilabu hivyo
viwili viliweza kukubaliana kwa ada ya pauni
milioni 1.2 ili kumpata Mfaransa huyo thabiti.
Kuwasili kwa Cantona kuliipa United mwamko
muhimu sana na kuisaidia timu hiyo kuweza
kujishindia taji la kwanza la Ligi tangu mwaka
wa 1967. Baada ya kusajiliwa kwa Roy Keane
kutoka Nottngham Forest mnamo mwaka wa
Julai 1993, United iliweza kushinda taji la pili
mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa
1957 kwenye mwaka uliofuata, kabla ya
kushinda kombe la FA ili kukamilisha "Ushindi
pacha" wa kwanza katika historia ya Kilabu hiyo.
Mwaka huo, hata hivyo, klabu kiliomboleza
kufuatia kifo cha aliyekuwa meneja na
mkurugenzi wa klabu Matt Busby, aliyekufa
tarehe 20 Januari 1994.
Msimu wa 1994-95 ulikuwa wa kwanza kwa
klabu kumaliza bila kombe tangu 1988-89,
ingawa walicheza vizuri hadi katika wiki ya
mwisho wa msimu na kufikiwa fainali ya FA Cup,
ambapo walipoteza kwa Everton. Andy Cole
alisajiliwa kutoka Newcastle United kwa
gharama iliyoweka rekodi Uingereza ya paundi
milioni £6 pamoja na Keith Gillespie. Hata hivyo,
baada mchuanio wa kwanza wa Cole akiwa
United, Eric Cantona alipokea marufuku ya miezi
nane kwa kuruka ndani ya eneo umati na
kumuumiza Mathayo Simmons shabiki wa
Crystal Palace, ambaye alikuwa amemdhihaki
Cantona kutokana na rangi ya ngozi yake
akiondoka uwanjani wakati wa mchuano wa
United ugani Selhurst Park. Kusimamishwa kwa
Cantona kulitolewa na baadhi kama sababu ya
United kushindwa kukamilisha kwa mataji
matatu "hat-trick" msimu huo. Kutofanikiwa
kama ilivyotarajiwa msimu huo kulimsababisha
Ferguson kufanya marekebisho makuu katika
timu aliwauza Paul Ince, Andrei Kanchelskis na
Mark Hughes na kujaza nafasi zaoo kwa
wachezaji kutoka katika timu ya vijana wa klabu
hiyo, akiwemo David Beckham, Gary Neville, Phil
Neville na Paul Scholes. Baada ya kushindwa
3-1 na Aston Villa katika siku ya ufunguzi wa
msimu 1995-96, mwanahabari wa televisheni
maarufu Alan Hansen alitoa kauli maarufu kwa
kusema "kamwe hamtashinda chochote mkiwa
na watoto." [14] Wachezaji kadhaa wapya,
ambao baadhi yao kwa haraka walijumuishwa
katika michuano ya kimataifa ya mara kwa mara
na timu ya Uingereza, waliitikia vizuri na
kutokana na motisha ya kurejea kwa Cantona
Oktoba 1995, United ikawa klabu ya kwanza ya
Uingereza kuwahi kushinda mataji mawili mara
mbili, ufanisi uliokuja kujulikana kama "Double
Double". [15]
Nahodha Steve Bruce aliondoka kuelekea
Birmingham City mwezi Julai 1996, na Alex
Ferguson akamtaja Eric Cantona kama nahodha
mpya wa klabu. Aliiongoza timu kutwaa taji la
nne la ligi kati ya miaka mitano katika 1996-97
kabla ya kustaafu kutoka kandanda akiwa na
umri wa 30 ilipofika mwisho wa msimu huo.
Teddy Sheringham aliletwa kuchukua nafasi
yake, na shati yake tambulika nambari 7
ikakabidhiwa David Beckham. Walianza msimu
wa 1997-98 vizuri, lakini wakapoteza michuano
mitano baada ya Krismasi na kumaliza katika
nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya washindi
mara mbili Arsenal. Baada ya kipindi bila
mshindani wa kila mara kuwania taji ligi, hii
ilikuwa dhibitisho ya kuwasili kwa Arsenal kama
mshindani halisi ambao wangegombea katika
miaka michache iliyofuata.
Ushindi mara tatu, Treble (1998–99)
Mataji ya Utatu - ya Ligi Kuu, Ligi ya
Mabingwa na Kombe la FA (kushoto
kuelekea kulia)
Msimu wa 1998-99 kwa Manchester United
ulikuwa na mafanikio sana katika historia ya
vilabu vya kandanda nchini Uingereza kwani
walikuwa timu ya pekee ya Uingereza iliyowahi
kushinda mataji matatu - Ligi Kuu (Premier),
kombe la FA na taji la mabingwa UEFA
Champions Leaguae katika msimu huo. [16]
Baada ya msimu wa wasiwasi wa Ligi ya
Premier, Manchester United ilitwaa taji hilo
kwenye siku ya mwisho ya fainali kwa
kuwashinda Tottenham Hotspur mabao 2-1,
huku Arsenal ikiishinda Aston Villa bao 1-0. [17]
Kutwaa taji la Ligi ya Premier kulikuwa sehemu
ya kwanza ya ushindi mara tatu (treble), sehemu
moja ambayo meneja Alex Ferguson aliieleza
kuwa ngumu zaidi. [17] Katika Fainali ya kombe
la FA United ilikabiliana na Newcastle United na
kushinda 2-0 kwa mabao kutoka kwa Teddy
Sheringham na Paul Scholes.[18] Katika mechi
ya mwisho ya msimu wa 1999 walicheza UEFA
Chapions League Final na kuishinda timu ya
Bayern Munich katika kile kinafikiriwa kuwa
mwamko mkuu sana kuwahi kushuhudiwa,
mchuano ulikuwa umeingia muda wa ziada
wakiwa wameshindwa kwa bao moja kabla ya
kutoka nyuma na kufunga mara mbili na hivyo
kushinda 2-1. [16] Ferguson baadaye
alipongezwa kwa huduma zake katika kandanda
na kutunukiwa heshima ya taifa inayompa
ruhusa kuitwa "sir". [19] Kuhitimisha mwaka huo
wa kuvunja rekodi, Manchester United ilishinda
kombe la Intercontinental baada ya kuinyuka
Palmeiras bao 1-0 mjini Tokyo. [20]
Baada ya kipindi cha ushindi Mara
Tatu (1999-hadi sasa)
United ilishinda ligi mwaka 2000 na 2001, lakini
vyombo vya habari vikaona kana kwamba klabu
kimeshindwa msimu huo kwa sababu
kilishindwa kutwaa tena taji la Ulaya.
[ onesha uthibitisho ] Mwaka 2000, Manchester
United ilikuwa mojawapo ya timu 14 waanzilishi
wa G-14, kundi la vilabu vya soka mashuhuri
Ulaya.[21] Klabu hicho pia kilikataa kushiriki
kombe la FA 1999-2000 na badala yake kushiriki
katika mashindano ya uzinduzi wa taji la FIFA la
Klabu Bingwa Duniani Brazil, kilitaja shinikizo
kutoka kwa FA, UEFA na kamati ya Uingereza
iliyokuwa ikishughulikia kombe la dunia la 2006.
Ferguson aliweka mikakati ya kujihami ili
kufanya iwe vigumu kwa United kushindwa
Ulaya, lakini mikakati hiyo haikuwa na mafanikio
kwani United ilikamilisha msimu wa Ligi Kuu ya
2001-02 katika nafasi ya tatu. Walitwaa tena ligi
msimu uliofuata (2002-03) na kuanza msimu
uliofuata vizuri, lakini hali yao ilishuka kwa kiasi
kikubwa baada ya Rio Ferdinand kupokezwa
marufuku tata ya miezi minane kwa
kutohudhuria upimaji wa madawa ya kulevya.
Walishinda kombe la FA 2004, hata hivyo,
waliibandua nje Arsenal (hatimaye Arsenal
ilishinda taji la Ligi Kuu msimu huo) wakiwa
njiani kuelekea fainali ambako waliishinda
Millwall.
Msimu wa 2004-2005 ulijawa na hali ya
kutofunga mabao, hasa kutokana na jeraha la
mshambulizi Ruud van Nistelrooy na United
ikamaliza msimu huo bila taji lolote na katika
nafasi ya tatu. Wakati huu, hata kombe la FA
liliwaponyoka kwani Arsenal iliishinda United kwa
mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare baada
ya kucheza kwa dakika 120. Nje ya uwanja,
hadithi kuu ilikuwa uwezekano wa klabu
kuchukuliwa, tarehe 12 Mei 2005 na
mfanyibiashara wa Kimarekani Malcom Glazer
ambaye aliweza kupata udhibiti wa klabu hiyo
kupitia uwekezaji kutumia kampuni yake ya Red
Football Ltd. katika ununuzi uliothaminiwa kufikia
kima cha takribani milioni £800 (wakati huo
ikikisiwa kuwa sawa na dola bilioni 1.5). [22][23]
Tarehe 16 Mei, aliziongeza hisa zake hadi 75%
zinazohitajika kukiondoa klabu hicho kutoka
Soko la Hisa na kukifanya kuwa binafsi tena,
alitangaza nia yake kufanya hivyo katuka muda
wa siku 20.[23] Tarehe 8 Juni, aliwateua
wanawe katika bodi ya Manchester United kama
wakurugenzi wasio watendaji.[24]
United ilianza vibaya msimu wa 2005-06, huku
kiungo wa kati Roy Keane akiondoka kujiunga na
Celtic baada ya kuwakosoa hadharani wachezaji
wenzake kadhaa. Klabu pia ilikuwa imeshindwa
kuhitimu kufuzu kwa awamu ya mwondoaano wa
UEFA Champions League kwa zaidi ya mwongo
mmoja, baada ya kupoteza kwa Benfica. Msimu
huu pia walikumbwa na mikosi kadhaa ya
majeraha kwa wachezaji wakuu kama vile
Gabriel Heinze, Alan Smith, Ryan Giggs na Paul
Scholes. Hata hivyo, walizuiliwa kuachwa
mikono mitupu katika misimu mifululizo-
masikitiko ambayo yalikuwa hayajashuhudiwa
kwa miaka 17 iliyopita-kwa kushinda kombe la
Ligi ya 2006, baada ya kuwalaza majirani zao
waliopandishwa cheo Wigan Athletic katika
fainali kwa mabao 4-0. United pia ilijihakikishia
nafasi ya pili na kufuzu moja kwa moja kushiriki
michuano ya Ligi ya Mabingwa (Champions
League) siku ya mwisho ya msimu kwa
kuishinda Charlton Athletic 4-0. Mwishoni mwa
msimu wa 2005-06, mmoja wa washambuliaji
wa United, Ruud van Nistelrooy, alikihama klabu
na kujiunga na Real Madrid, kutokana na ugomvi
baina yake na Alex Ferguson. [25]
Mnamo Julai 2006, klabu kilitangaza mpango wa
ufadhili mpya. Kiasi cha jumla kitakuwa £ milioni
660, ambayo italipiwa riba ya £ milioni 62 kwa
mwaka. [26] Matokeo ya mpango huu mpya wa
ufadhili utakuwa punguzo la asilimia 30 ya
malipo ya kila mwaka. [27] Uwanjani, msimu wa
2006-07 ulishuhudia United ikirejea na mtindo
wao wa kandanda ya kushambulia ambao ndio
ulikuwa msingi wa miaka yao ya ufanisi
mwishoni mwa miaka ya 1990, wakifunga
takriban mabao 20 zaidi ya Chelsea waliokuwa
katika nafasi ya pili baada ya michuano 32.
Januari 2007, United ilimsajili Henrik Larsson
kwa mkopo wa miezi miwili kutoka Helsingborg
ya Uswidi, mshambuliaji alitekeleza jukumu
muhimu sana katika kuisaidia United kuingia
nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, [28] huku ikiwa
na matumaini ya kushinda mataji matatu kwa
mara ya pili, hata hivyo, baada ya kufikia nusu
fainali, United iliaibishwa na Milan kwa jumla ya
mabao 3-5. [29] Miaka minne baada taji lao la
mwisho, United ilishinda taji la Premier League
tarehe 6 Mei 2007 baada ya Chelsea kutoka sare
na Arsenal jambo lililoiacha The Blues pointi
saba nyuma ikiwa imesaza michuano miwili ili
kumaliza, kufuatia ushindi wa United wa 1-0
katika mchuano wa timu kutoka mji wa
Manchester "Derby" siku iliyopita na kuifanya
kombe lao la 9 la Ligi ya Premier katika misimu
15 ya uwepo wa ligi hiyo. Hata hivyo, ushindi
pacha "Double" wa mara ya nne ambao
haukutarajiwa haukutokea baada ya Chelsea
kuifunga United 1-0 katika muda wa ziada katika
kombe la kwanza la FA kufanyika katika uwanja
mpya wa Wembley; wa kwanza kufanyika nchini
Uingereza tangu uwanja wa zamani kubomolewe
miaka saba iliyopita.
Kipindi cha kati ya 2007-08 kilishuhudia United
ikimaliza kwa kushinda mataji mawili ya Ulaya
licha ya kuanza vibaya msimu huo walipojipata
katika nafasi 17 katika Ligi Kuu baada ya
kushiriki katika mechi tatu. Hata hivyo, tarehe 11
Mei 2008, United ilihifadhi taji la Ligi ya Premier
kufuatia ushindi dhidi ya Wigan Athletic. Huku
washindani wao katika taji hilo Chelsea
wakiweza tu kutoka sare na Bolton Wanderers,
United iliweza kumaliza msimu kwa alama mbili
mbele. Klabu pia ilifika fainali ya Kombe la Ulaya
kwa mara ya tatu katika historia yake, baada ya
kuvishinda vilabu kama Barcelona na Roma ili
kufuzu kwa fainali. Waliifunga Chelsea katika
mikwaju ya penalti 6-5 katika fainali ugani
Luzhniki Moscow baada ya kutoka sare ya 1-1
katika muda wa kawaida tarehe 21 Mei 2008.
Kupitia ushindi huu , walijipatia taji lao la tatu la
Ulaya na kuweka rekodi yao kutowahi kupoteza
fainali kubwa ya Ulaya. Kisadfa, msimu huu
ulikuwa wa miaka 100 tangu Manchester United
iliposhinda taji lao la kwanza la Ligi, ilikuwa
miaka 50 baada ya ajali ya ndege ya Munich na
miaka 40 baada ya Manchester United kuwa
timu ya kwanza ya Uingereza kushinda taji la
Ulaya. Fainali ya Kombe la Ulaya ilishuhudia pia
Ryan Giggs akiichezea klabu hiyo kwa mara ya
759, na kumpita Bobby Charlton aliyekuwa
akishikilia rekodi ya kuichezea mara nyingi zaidi
klabu hicho.
Kabla ya kuanza kwa msimu wa 2008-09, United
walishiriki na kushinda tuzo ya ngao yaFA
Community Shield ya 2008. United walifunga
Portsmouth katika mikwaju ya penalti 3-1,
washindi wa Kikombe cha FA cha 2007-08,
baada ya mechi kukamilika kwa sare tasa ya
0-0 ndani ya dakika 90. Mnamo tarehe 21
Desemba 2008, United waliongezea nishani zaidi
kwenye hazina yao ya tuzo kwa kushinda katika
fainali ya Kombe la Ulimwengu la Vilabu vya
FIFA kwa kuishinda LDU Quito kutoka Ecuador
kwa bao 1-0 kule Japan, Wayne Rooney ndiye
aliyefunga bao la ushindi. Miezi miwili baadaye,
waliliongezea kombe la Ligi ya 2009 katika
hazina yao ya tuzo kwa kuishinda Tottenham
Hotspur mabao 4-1 kwenye mikwaju ya
penalti. [30] Mnamo tarehe 16 Mei, United
waliweza kuwahi taji la 11 katika Ligi ya Primia -
na taji la ujumla la 18 katika Ligi – baada ya
kuenda sare tasa ya 0-0 nyumbani kwao
wakicheza na Arsenal huku wakishinda mataji
matatu mtawalia ya Ligi ya Premier kwa mara ya
pili. [31] Mnamo tarehe 27 Mei 2009, Barcelona
waliweza kuishinda Manchester United mabao
2-0 katika fainali ya Ligi Mabingwa kule Rome,
yaliyofungwa na Samuel Eto'o na Lionel
Messi. [32] Fainali ya Ligi ya Mabingwa ilitokea
kuwa mechi ya mwisho kwa Carlos Tévez –
ambaye mkataba wake ulikamilika mnamo
tarehe 30 Juni – na Christiano Ronaldo –
aliyeuzwa kwa Real Madrid kwa gharama ya
milioni £80, kuvunja rekodi ya dunia ya
kuhamisha na kusajiliwa kwa Kaka na Real
Madrid kutoka Milan kwa gharama ya milioni
£56. Hata hivyo, United waliitikia hasara hizo
kwa kumhamisha na kumsajili Michael Owen bila
gharama yoyote, Antonio Valencia kwa milioni
£17 na Gabriel Obertan kwa gharama ya milioni
£3.
Msimu wa 2009-10 ulianza vizuri kwa timu ya
Manchester United, licha ya kushindwa 1-0 na
timu ya Burnley kule Turf Moor iliyokuwa pigo
kubwa kwao. Wingi wa ushindi ukafuata
hatimaye, pamoja na ushindi wa kusisimua dhidi
ya Manchester City kwa mabao 4-3, uliopatikana
mnamo dakika ya 96 kutokana na bao lake
Michael Owen. Hata hivyo, mchezo isioridhisha
uliwafanya kushindwa mabao 2-0 na Liverpool
uwanjani Antfield. Kufikia 1 Novemba,
Manchester United ni ya pili katika ligi, alama 2
nyuma ya Chelsea. Katika Ligi ya Mabingwa,
United kwa sasa ndio washindi wa kwanza
kwenye kundi lao, pamoja na ushindi dhidi ya
Beşiktaş na CSKA Moscow na ushindi dhidi ya
Wolfsburg huko nyumbani kwao. Mnamo tarehe
3 Novemba, Manchester United waliweza
kuhifadhi na kuhitimu kutoka katika kikundi kwa
kupata mabao sare 3-3 dhidi ya CKSA Moscow.
Nembo na rangi za klabu
Katika enzi zake kama Newton Heath, klabu
kilitumia mavazi ya rangi tofauti, inayotambuliwa
zaidi ni shati la rangi ya manjano na kijani
lililovaliwa kuanzia 1878 hadi 1892, na tena
1894-1896; vazi hili la milia lilitumika tena katika
michuano ya ugenini mapema miaka ya 1990.
Mavazi mengine yaliyovaliwa na Newton Heath
ni pamoja na shati jekundu lililokuwa na weupe
robo yake (1892-1894) na shati jeupe lisilo kuwa
na milia (1896-1902), zote hizi zilivaliwa na
kaptura ya rangi ya samawati.[33] Katika mwaka
wa 1902, pamoja na klabu kubadili jina na kuwa
Manchester United, klabu pia kilibadili rangi zake
kuwa jezi nyekundu, kaptura nyeupe na soksi
nyeusi, ambayo imesalia kuwa sare wastani ya
Man Utd katika michuano ya nyumbani tangu
wakati huo. Kilicho tofauti na haya ni jezi
ambazo timu ilivaa ikicheza fainali ya kombe la
FA 1909 na Briston City ambayo ilikuwa nyeupe
na mshipi mwekundu wa muundo wa “V”. [34]
Mtindo huu ulifufuliwa katika miaka ya 1920
kabla United kurudia mashati yenye rangi
nyekundu pekee, pia ilitumika kwa ajili ya
michuano ya nyumbani na ugenini katika msimu
wa 2009-10 kama njia ya kusherehekea miaka
100 katika Old Trafford. [35][36]
Jezi za kuchezea ugenini kawaida huwa nyeupe
na kaptura nyeusi na soksi nyeupe, lakini rangi
nyingine zimetumika, ikiwa ni pamoja na shati
iliyokuwa na milia ya samawati na nyeupe
iliyotumika kati ya 1903-1916, sare nyeusi kila
kitu kilichotumika mwaka 1994, 2003 na 2007 na
shati la blue iliyokuwa na mistari myembamba
mwaka 2000. Mojawapo ya sare iliyokuwa
maarufu kwa wengi, japo haikudumu, ni sare ya
United iliyokuwa ya michuano ya ugenini ya
rangi ya kijivu pekee iliyotumika kati ya 1995-96,
iliacha kutumiwa baada ya timu kushindwa
mchezo mmoja wakati walikuwa wameivaa.
Katika muda wa mapumziko wakicheza dhidi ya
Southampton, wakati united ilikuwa imetingwa
3-0, walibadilisha mavazi na kuvaa sare ya
samawati na nyeupe lakini bado wakashindwa
3-1. Kulingana na wachezaji, mavazi ya kijivu
hayakuwa yakionekana vyema jambo
lililosababisha matokeo duni.[37] Sare nyingine
maarufu ya kucheza ugenini ya Man Utd ilikuwa
uweza wa kuvalika pande zote, ilikuwa na milia
ya nyeupe na mikono mieusi na mstari wa
kidhahabu upande mmoja na milia ya kidhahabu
na mstari mweusi upande mwingine. Shati hii
ilitolewa kama sare ya mwisho iliyoshonwa na
Umbro kwa klabu kabla ya kuanza kuhudumiwa
na Nike, na iliadhimisha miaka 100 tangu klabu
kilipobadili jina lake kutoka Newton Heath kuwa
Manchester United.
Sare ya tatu ambayo huvaliwa katika michuano
ya nyumbani ni samawati tangu shati hadi sokisi
kwa heshima ya sare iliyovaliwa 1968 timu
iliposhinda Kombe la Ulaya, ukumbusho wa moja
kwa moja ulifanywa na klabu 2008-09
kukumbuka miaka 40 ya jezi la tatu la 1968.
Kinyume na desturi hii ni kuwa ni pamoja na
sare ya rangi ya manjano iliyovaliwa katika
miaka ya 1970, sare iliyotajwa hapo awali ya
mistari ya samawati na nyeupe kuanzia 1996,
ambayo ilionekana kuwapendeza sana
mashabiki, na shati jeupe iliyokuwa na mikato ya
mlazo wa rangi nyeusi na nyekundu kuanzia
2004. United pia imetumia shati zilizo wahi
kutumika kama ya mazoezi kuwa sare zao za
tatu, iliwahi kutumia sare nyeusi toka juu hadi
chini katika msimu 1998-99 na shati samawati
iliyokuwa na rangi ya damu ya mzee ubavuni
mwaka 2001 kwa michuano dhidi ya
Southampton na PSV Eindhoven.
Hivi sasa, jezi ya nyumbani ya Manchester
United ni nyekundu na iliyo na tepe nyeusi
isiyokolea kifuani. Nembo ya klabu huwa juu ya
ngao nyeusi yenye ukubwa sawa upande wa
kushoto wa V, ilihali alama ya Nike ni nyeupe na
huwa upande wa kulia; nembo ya AIG pia ni
nyeupe. Katika kukumbuka miaka 100 tangu
kufunguliwa kwa uwanja wa klabu hicho cha Old
Trafford kuna kitambulisho kinachosoma
“Uwanja wa ndoto tangu 1910”(The Theatre of
Dreams Since 1910 )kilichoshikishwa upande wa
mshono. Shati la nyumbani huvaliwa na kaptura
nyeupe iliyo na mistari myekundu inayoteremka
pande zote mbili za miguu, na soksi nyeusi iliyo
na mkato mwekundu. [35] Hivi karibuni sare ya
kucheza ugenini imekaribiana katika muundo na
sare ya nyumbani, lakini shati ni jeusi lililo na
utepe wa samawati kifuani na nembo ya klabu
huwa juu ya ngao ya samawati. Sawa na sare ya
nyumbani, nembo ya wadhamini iko katikati na
kwa rangi nyeupe. Kaptura pia ni nyeusi na milia
ya samawati ikielekea chini, huku soksi nazo
zikiwa nyeusi na tepe ya samawati. [36] Sare ya
ugenini ya klabu ya msimu wa 2008-09,
inayojumuisha shati jeupe lililo na mstari wa
samawati kwenda chini ubavuni na ukosi wa
samawati ilio na mkato mwekundu, unaotumiwa
kama sare ya tatu ya msimu wa 2009-10.
Ikivaliwa pamoja na kaptura za samawati na
soksi nyeupe, jezi la tatu lina nembo za wafadhili
kwa rangi ya samawati pamoja na herufi "MUFC"
nyuma ya ukosi. Beji ya klabu inakalia nguo
nyeupe kushoto mwa kifua. [38][39]
Nembo ya Manchester United imebadilishwa
mara chache, lakini umbo la kimsingi limebakia
sawa. Beji hiyo imechukuliwa kutoka kwa nembo
ya jiji la Manchester. Picha ya Shetani kwenye
beji ya klabu ilitokana na lakabu ya klabu “Red
Devils” (Shetani Wekundu); lililoanza kutumika
mapema miaka ya 1960 baada ya Matt Busby
kusikia likirejelea timu ya raga ya Salford
kutokana na jezi zao nyekundu. [40] Kufikia
mwisho wa miaka ya 1960 nembo hiyo ya
shetani ilianza kujumuishwa katika utaratibu na
shali za klabu kabla ya kujumuishwa kwenye
beji ya klabu mnamo 1970 ikishikilia mkuki
wenye ncha tatu. Katika mwaka wa 1998, beji
iliundwa upya tena, wakati huu maneno "Footbal
Club" yakiondolewa. [41]
Wachezaji
Kikosi cha timu ya kwanza
Kama ilivyokuwa 29 Oktoba 2009,kulingana na
vyanzo mseto katika tovuti rasmi.[42][43]
Note: Flags indicate national team as has been
defined under FIFA eligibility rules . Players may
hold more than one non-FIFA nationality.
Na. Nafasi Mchezaji
1 GK Edwin van
der Sar
2 DF
Gary
Neville
( captain )
3 DF Patrice
Evra
4 MF Owen
Hargreaves
5 DF Rio
Ferdinand
6 DF Wes Brown
7 FW Michael
Owen
8 MF Anderson
9 FW Dimitar
Berbatov
10 FW Wayne
Rooney
11 MF
Ryan Giggs
( vice-
captain )
12 GK Ben Foster
13 MF Park Ji-
Sung
14 MF Zoran
Tošić
15 DF Nemanja
Vidić
16 MF Michael
Carrick
17 MF Nani
18 MF Paul
Scholes
Na. Nafasi
19 FW D
20 DF F
21 DF R
22 DF J
O
23 DF J
E
24 MF D
F
25 MF A
V
26 FW G
O
27 FW F
28 MF D
G
29 GK T
K
30 DF R
D
31 MF C
E
38 GK
R
R
Z
41 FW J
K
42 MF
E
43 MF J
Wa mkopo
Note: Flags indicate national team as has been
defined under FIFA eligibility rules . Players may
hold more than one non-FIFA nationality.
Na. Nafasi Mchezaji
35 MF
Tom
Cleverley
(at
Watford
until 3
Januari
2010) [44]
36 MF
David
Gray (at
Plymouth
Argyle
until 18
Desemba
2009) [45]
37 DF
Craig
Cathcart
(at
Watford
until 4
Januari
2010) [46]
Na. Nafasi
40 GK
Be
Pet
Uni
29
200
— FW
Ma
Dio
Mol
31
200
Wa ziada na walio chuoni
Kwa kikosi cha wachezaji wa ziada na walio
chuoni, tazama Manchester United F.C.
Reserves and Academy.
Waliokuwa wachezaji hapo awali
Kwa maelezo juu ya wachezaji wa zamani,
tazama Orodha ya wachezaji wa klabu ya Soka
ya Manchester United na Category:Manchester
United F.C. players
Manahodha wa klabu
Tarehe [49] Jina Maelezo
1878-1882 Haijulikani
1882 E.
Thomas
Nahodha wa
kwanza wa klabu
anayejulikana
1882-1883 Haijulikani
c.1883-1887 Sam
Black
c.1887-1890 Jack
Powell
1890-1892 Haijulikani
1892-1893 Joe
Cassidy
1893-1894 Haijulikani
c.1894 James
McNaught
1894-1896 Haijulikani
c.1896-1903 Harry
Stafford
Nahodha wa
kwanza wa
Manchester United
1903-1904 Haijulikani
c.1904-1905 Jack
Peddie
c.1905-1912 Charlie
Roberts
1912-1913 George
Stacey
1913 Dick
Duckworth
1914 George
Hunter
1914-1915 Patrick
O'Connell
1915-1919 Hamna
Hakuna kandanda
iliyochezwa wakati
wa Vita vya
Kwanza vya Dunia
1919-1922 Haijulikani
c.1922-1928 Frank
Barson
c.1928-1931 Jack
Wilson
1931-1932 George
McLachlan
1932 Louis
Page
1932-1935 Haijulikani
c.1935-1939 Jimmy
Brown
1939-1945 Hamna
Hakuna kandanda
iliyochezwa wakati
wa Vita vya Pili vya
Dunia
1945-1953 Johnny
Carey
Nahodha wa
Kwanza wa baada
ya Vita, na wa
kwanza kutoka nje
ya Uingereza
1953-1954 Stan
Pearson
1954-1955 Allenby
Chilton
1955-1958 Roger
Byrne
Alikufa mwaka wa
1958 katika ajali ya
ndege ya Munich
1958-1959 Bill
Foulkes
1959-1960 Dennis
Viollet
1960-1962 Maurice
Setters
1962-1964 Noel
Cantwell
1964-1967 Denis
Law
1967-1973 Bobby
Charlton
1973 George
Graham
1973-1975 Willie
Morgan
1975-1982 Martin
Buchan
1982 Ray
Wilkins
1982-1994 Bryan
Robson
Nahodha
aliyehudumu kwa
muda mrefu zaidi
katika historia ya
United
1994-1996 Steve
Bruce
1996-1997 Eric
Cantona
Nahodha wa
kwanza wa United
kutoka nje ya
Uingereza na pia
Jamhuri ya Ireland
1997-2005 Roy
Keane
Tuzo nyingi zaidi
zilishindwa akiwa
nahodha
2005-hadi
leo
Gary
Neville
Nahodha wa
kwanza wa kilabu
wa kuzaliwa katika
eneo la Greater
Manchester tangu
enzi za Dennis
Viollet
Rekodi za wachezaji
Kwa mujibu wa mechi iliyochezwa tarehe 8
Novemba 2009 na kulingana na takwimu ya
tovuti rasmi. [50] Wachezaji walioandikwa kwa
maandishi kolezo ndiyo bado wanaichezea timu
ya Manchester United.
Walioshiriki michuano mingi
# Jina Muda
klabuni Kushiriki Mabao
1 Ryan
Giggs
1991-hadi
sasa 817 150
2 Bobby
Charlton 1956-1973 758 249
3 Bill
Foulkes 1952-1970 688 9
4 Paul
Scholes
1994-hadi
leo 616 144
5 Gary
Neville
1992-hadi
leo 578 7
6. Alex
Stepney 1966-1978 539 2
7 Tony
Dunne 1960-1973 535 2
8 Denis
Irwin 1990-2002 529 33
9. Joe
Spence 1919-1933 510 168
10 Arthur
Albiston 1974-1988 485 7
Waliofunga zaidi
# Jina Muda
klabuni Mabao Kushiriki
U
M
1 Bobby
Charlton
1956-1973 249 758
2 Denis
Law 1962-1973 237 404
3 Jack
Rowley 1937-1955 211 424
4
= Dennis
Viollet 1953-1962 179 293
4
= George
Best
1963-1974 179 470
6. Joe
Spence 1919-1933 168 510
7 Mark
Hughes
1983-1986
1988-1995
163 467
8
=
Ruud
van
Nistelrooy
2001-2006 150 219
8
= Ryan
Giggs
1991-hadi
leo 150 817
10 Stan
Pearson 1937-1954 148 343
Washindi wa matuzo
Ballon d'Or
Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa
Ballon d'Or wakati wakiichezea Manchester
United:
Denis Law - 1964
Bobby Charlton - 1966
George Best - 1968
Cristiano Ronaldo - 2008
European Golden Shoe ( taji la kiatu cha
dhahabu cha Ulaya)
Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa
European Golden Shoe wakati wakiichezea
Manchester United:
Cristiano Ronaldo (mabao 31 ) - 2008
Tuzo la UEFA kwa mwanakandanda wa klabu
bora wa mwaka
Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa tuzo
la UEFA kwa mwanakandanda wa klabu bora wa
mwaka wakati wakiichezea Manchester United:
David Beckham - 1999
Cristiano Ronaldo - 2008
Mchezaji wa mwaka wa FIFA
Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa tuzo
la Mchezaji wa mwaka wa FIFA wakati
wakiichezea Manchester United:
Cristiano Ronaldo - 2008
Timu ya akina dada
Timu ya soka ya akina dada ya Manchester
United yaani Manchester United Ladies FC
ilianzishwa mwaka 1977 kama klabu ya
mashabiki akina dada yaani Manchester United
Supporters Club Ladies. Walijiunga na ligi ya
Three Counties League mwaka 1979, na wakawa
wanachama waanzilishi wa ligi ya wanawake wa
eneo la kaskazini (North West Women's
Regional Footbal League) mwaka 1989,
walipogeuza jina lao rasmi na kuwa Manchester
United Ladies FC. Ingawa walishushwa kutoka
katika ligi msimu wao wa kwanza,
walipandishwa ngazi tena baada ya msimu huo
na kushinda taji ya ligi ya 1995-96. Msimu wa
1998-99, timu hiyo ilijiunga na Northern
Combination, hatua mbili chini ya Ligi Kuu ya
wanawake ya FA. Waliletwa rasmi chini ya
mwavuli wa Manchester United FC mwanzo wa
msimu wa 2001-02, lakini walivunjiliwa mbali
kiutata mwanzo wa msimu wa 2004-05 kwa
sababu za kifedha. Uamuzi huo ulikumbwa na
upinzani ikizingatiwa faida inayopatikana na
Manchester United na pia kutokana na ukweli
kuwa timu ziliondolewa ligi zao zote kabla hata
wachezaji kuarifiwa kuhusu uamuzi huo. Hata
hivyo, klabu bado kilishiriki katika kandanda ya
wasichana kwa kutoa mafundisho kwa
wasichana chini ya umri wa miaka 16.[51]
Maafisa wa klabu
Mmiliki: Malcolm Glazer
Rais wa heshima: Martin Edwards
Manchester United Limited
Wenyekiti wenz: Joel Glazer & Avram Glazer
Afisa mkuu mtendaji: David Gill
Afisa mkuu wa utekelezaji: Michael
Bolingbroke
Mkurugenzi wa Kibiashara: Richard Arnold
Mkurugenzi mtendaji: Ed Woodward
Wakurugenzi wasio watendaji: Bryan Glazer,
Kevin Glazer, Edward Glazer & Darcie Glazer
Manchester United Football Club
Wakurugenzi: David Gill, Michael Edelson, Sir
Bobby Charlton, Maurice Watkins
Katibu wa Klabu: Ken Ramsden
Naibu katibu wa klabu: Ken Merrett
Balozi wa kimataifa: Bryan Robson
Maafisa wa ukufunzi na wa kimatibabu
Meneja: Sir Alex Ferguson
Naibu meneja: Mike Phelan
Mkufunzi wa timu ya kwanza: René
Meulensteen
Mkufunzi wa walindalango: Eric Steele
Mkufunzi wa mazoezi: Tony Strudwick
Mkufunzi wa nguvu & uzoefu: Mick Clegg
Mkuu wa utendaji wa binadamu: Dr. Richard
Hawkins [52]
Meneja wa timu ya ziada: Ole Gunnar
Solskjær
Mkufunzi wa timu ya ziada: Warren Joyce
Skauti mkuu: Jim Lawlor
Skauti mkuu wa Ulaya: Martin Ferguson
Mkurugenzi wa chuo cha vijana: Brian McClair
Mkurugenzi wa kandanda ya vijana: Jimmy
Ryan
Daktari wa klabu: Dr. Steve McNally
Naibu daktari wa klabu : Dr. Tony Gill
Mwanatibamaungo wa timu ya kwanza: Rob
Swire
Historia ya usimamizi
Tarehe Jina Maelezo
1878-1892 Hajulikani
1892-1900 AH
Albut
1900-1903 James
West
1903-1912 Ernest
Mangnall
1912-1914 John
Bentley
1914-1922 Jack
Robson
1922-1926 John
Chapman
Meneja wa kwanza
kutoka nje ya
Uingereza
1926-1927 Lal
Hilditch
1927-1931 Herbert
Bamlett
1931-1932 Walter
Crickmer
1932-1937 Scott
Duncan
1937-1945 Walter
Crickmer
1945-1969 Mtt
Busby
Meneja wa kwanza
wa baada ya Vita ya
Pili ya Dunia na
meneja aliyehudumu
muda mrefu katika
historia ya United
1969-1970 Wilf
McGuiness
1970-1971 Mtt
Busby
1971-1972 Frank
O'Farrell
Meneja wa kwanza
kutoka nje ya
Uingereza
1972-1977 Tommy
Docherty
1977-1981 Dave
Sexton
1981-1986 Ron
Atkinson
1986-hadi
leo
Alex
Ferguson
Meneja aliyefaulu
sana kwa mujibu wa
vikombe
Ufuasi
Kabla ya Vita ya Pili vya Dunia, mashabiki
wachache wa kandanda wa Uingereza walisafiri
mbali kutazama michezo kwa sababu ya muda,
gharama, na vikwazo vya kivifaa kama vile
uhaba wa magari miongoni mwa wakaazi.
[ onesha uthibitisho ] Jinsi City na United
walivyocheza michuano ya nyumbani kwa
kubadilishana siku za Jumamosi,
Wanamanchester wengi wangetazama United
juma moja na juma lifuatalo City, lakini baada ya
vita, ushindani mkali ukaibuka na ikawa kawaida
zaidi kwa shabiki kuchagua kufuata timu moja
pekee. [onesha uthibitisho ]
United iliposhinda ligi mwaka 1956, walikuwa na
ufuasi wastani wa juu zaidi wa mahudhurio ya
ligi nyumbani, rekodi iliyokuwa inashikiliwa na
Newcastle United kwa miaka michache
iliyotangulia. Kufuatia ajali yao ya ndege Munich
mwaka wa 1958, watu zaidi walianza kushabikia
United na wengi wakaanza kuhudhuria
michuano. Hii illisababisha ushabiki kwa United
kupanuka sababu moja inayofanya United kuwa
mahudhurio ya juu katika ligi ya kandanda ya
Uingereza kwa takribani kila msimu tangu
wakati huo, hata wakati waliposhushwa ngazi na
kuwa katika Divisheni ya Pili 1974-75. [1] Kwa
kweli, kwa misimu miwili ambayo United
haikuwa na mahudhurio ya ligi, Old Trafford
ilikuwa ikifanyiwa kazi kubwa ya ujenzi (1971-72
na 1992-93).
Ripoti ya mwaka 2002, kwa anwani Do You
come From Manchester?, Ilionyesha kuwa
asilimia kubwa ya wanunuzi wa tiketi za msimu
za Manchester City huishi katika wilaya za posta
za Manchester, wakati United ilikuwa na idadi
kamili juu ya wanunuzu wa tiketi za msimu
wanaoishi katika eneo moja. [53]
Katika miaka ya 1990 na mapema miaka ya
2000, chanzo cha wasiwasi kwa mashabiki
wengi wa United kilikuwa uwezekano wa klabu
kununuliwa. Kundi la wafuasi IMUSA
(Independent Manchester United Supporters'
Association) lilijihusisha sana katika kupinga
ununuzi uliotarajiwa wa Rupert Murdoch mwaka
1998. Kundi lingine lililotoa shinikizo klabu
kisiuzwe, Shareholders United against Murdoch
(ambalo baadaye lilikuwa Shareholders United
na sasa ni Manchester United Supporters' Trust)
liliundwa wakati huu kuhamasisha wafuasi
kununua hisa za klabu, ili kwa kiasi
kuwawezesha wafuasi kuwa na usemi zaidi
katika masuala yaliyowatia wasiwasi kama vile
bei na mgao wa tiketi, na kwa kiasi kupunguza
hatari ya watu wasiohitajika kununua hisa za
kutosha kumiliki klabu. Hata hivyo, mpango huu
ulishindwa kumzuia Malcolm Glazer kuwa
mmiliki mwenye hisa nyingi. Wafuasi wengi
walikasirishwa, na baadhi walibuni klabu asi kwa
jina F.C. United of Manchester. Licha ya hasira
ya baadhi ya wafuasi kwa wamiliki wapya,
mahudhurio yameendelea kuongezeka.
Hisia zilizotolewa na mashabiki hao, wakati
mwingine umeshutumiwa. Mwaka 2000, maoni
yaliyotolewa kuhusu baadhi ya mashabiki katika
Old Trafford na nahodha wa wakati huo Roy
Keane, kwamba baadhi ya mashabiki hawawezi
hata " kuendeleza neno kandanda, acha
kuielewa" yalipelekea wao kutajwa kama
"mashabiki wanaohudhuria mchuano kufurahia
ukarimu wa klabu na wala si kuishabikia". [54]
Alex Ferguson pia ametoa maoni kadhaa kuhusu
mashabiki kiasi kwamba alidai kuwa hali
iliyoshuhudiwa tarehe 1 Januari 2008 ilikuwa
kama "matanga". [55] Baadaye aliongeza,
"Nadhani kumekuwa na siku kama hizi hapo
nyuma. Ilitokea miaka michache iliyopita, wakati
tulipotawala". [55] Baada ya ushindi maarufu wa
1-0 dhidi ya Barcelona ugani Old Trafford,
ambao uliiwezesha United kushiriki katika fainali
ya Ligi ya Mabingwa ( Champions League)
Moscow, Ferguson alisema kwamba mashabiki
wa United "walikuwa wapevu sana" na kwamba
wao "walituwezesha kufanikiwa". [56][57]
Uwanja
Klabu kilipoanzishwa mara ya kwanza, Newton
Heath alicheza michuano yao ya nyumbani
kwenye uwanja mdogo ulio North Road, Newton
Heath. Hata hivyo, timu geni zilizokuja kucheza
uwanjani humo zililalamikia hali yake, ambayo
ilikuwa "bwawa upande mmoja na uliojaa
miamba kama ya timbo upande mwingine". [8]
vyumba vya kubadilishia nguo pia havikuwa vya
kujivunia, vilikuwa umbali wa kutembea dakika
kumi katika baa ya Three Crowns iliyokuwa
Oldham Road. Baadaye walihamishiwa Shears
Hotel, mkahawa mwingine uliokuwa Oldham
Road, hata hivyo mabadiliko yalihitajika kama
klabu ilitaka kuendelea katika Ligi ya Kandanda.
Heath walibaki katika uwanja wao wa North
Road kwa miaka kumi na mitano 1878-1893,
mwaka mmoja baada ya kuingia Football League
na baadaye kuhamia makao mapya Bank Street
hapo Clayton. Uwanja mpya haukuwa mzuri
sana, vipande vichache vya nyasi vilijipenyeza
usoni mwa changarawe na mawingu ya moshi
yalifuka kutoka katika kiwanda kilichokuwa
karibu. Wakati mmoja, Walsall Town Swifts
ilikataa kucheza kutokana na hali mbaya ya
uwanja. Changarawe ilimwagwa uwanjani na
walinda uga, hatimaye wageni wakawashawishi
kucheza na kupoteza 14-0. walipinga matokeo
hayo, wakitaja hali mbaya ya uwanja kama
sababu ya wao kushindwa, mchuano ukarudiwa.
Hali haikuwa nzuri sana wakati wa marudiano,
timu ya Walsall ilishindwa tena, ingawa wakati
huu walibugia 9-0 tu.[8]
Mwaka wa 1902, klabu karibu kifilisike na
uwanja wa Bank Street ulifungwa na mdai
kutokana na klabu kushindwa kulipa deni lake.
Klabu kiliokolewa katika dakika za mwisho na
nahodha Harry Stafford ambaye aliweza
kuchangisha fedha za kutosha kulipia mchuano
wa ugenini Bristol City na kupata uwanja wa
muda karibu na Harpurhey kwa kuchezea duru
nyingine dhidi ya Blackpool. [59]
Kufuatia uwekezaji kuimarisha klabu tena, jina
lilibadilishwa na kuwa Manchester United,
ingawa kulikuwa na hamu ya kupata uwanja
uliokubalika. Wiki sita kabla ya mchuano wa
kwanza wa United kuwania Kombe la FA Aprili
1909, Old Trafford ilitajwa kuwa nyumbani kwa
Manchester United kufuatia ununuzi wa ardhi
muhimu kwa takribani £ 60,000. Msanifumijengo
Archibald Leitch aliajiriwa na mwenyekiti wa
United John Henry Davies na kupewa bajeti ya £
30.000 kwa ajili ya ujenzi. Mipango asilia
ilionyesha kuwa uwanja ungefaa kujengwa
kuhimili watu 100.000, ingawa idadi hiyo
ilipunguzwa hadi 77,000. Licha ya hilo, rekodi ya
mahudhurio ya 76,962 ilirekodiwa, ambayo hata
sasa ni zaidi ya idadi rasmi inayokubalika katika
uwanja huo. Ujenzi ulifanywa na Messrs Brameld
na Smith wa Manchester. Katika ufunguzi wa
uwanja, tiketi za kusimama ziligharimu peni sita,
wakati viti ghali zaidi katika jukwaa kuu zililipiwa
shilingi tano. Mchezo wa ufunguzi ulikuwa tarehe
19 Februari 1910 dhidi ya Liverpool FC, na
wageni wakashinda kwa 4-3. Kama ilivyotokea,
mabadiliko ya uwanja yalitokea wakati mwafaka
zaidi - siku chache tu baada ya klabu kucheza
mchuano wao wa mwisho ugani Bank Street,
mojawapo ya jukwaa liliangushwa chini na
dhoruba. [60]
Kupigwa kwa bomu wakati wa Vita vya Pili vya
Dunia, tarehe 11 Machi 1941, kuliharibu sehemu
kubwa ya uwanja, hasa jukwaa kuu. Handaki la
kati katika South Stand ndilo la pekee lililobakia
katika robo hiyo ya uwanja. Baada ya vita, United
iliwasilisha ripoti kwa Tume ya Madhara ya Vita
na kupokea fidia ya £ 22.278 kwa ajili ya
ukarabati wa uwanja huo. Ingawa uwanja
ulijengwa upya tena 1949, hakuna mchuano
uliosakatwa Old Trafford kwa takribani miaka 10
michuano ya "nyumbani" katika kipindi hicho
ilichezwa katika uwanja wa Manchester City,
Maine Road. Manchester City iliilipisha United £
5,000 kwa mwaka kwa matumizi ya uwanja wao,
pamoja na asilimia fulani ya ada ya kiingilio. [61]
Marekebisho mengine yalitokea baadaye,
yakianza na kuwekwa paa upande wa Stretford
End kisha ikawekwa pande za North Stand na
East Stand. Hata hivyo, mtindo wa zamani wa
paa uliwazuia mashabiki wengi kutazama na
hivyo, kupelekea kuboreshwa kwa paa hizo
kuwa zilizoinuka na ambazo bado zipo katika
uwanja huo leo. Stretford End lilikuwa jukwaa la
mwisho kufanyiwa ukarabati wa kuinuliwa paa,
kazi iliyokamilika kwa muda ufaao kuruhusu
michuano ya msimu wa 1993-94. [62]
Taa za uwanjani ziliwekwa kwa mara ya kwanza
uwanjani katikati ya miaka ya 1950. Viunzi180-
foot (55 m) vinne vikuu vilijengwa, kila kimoja
kikiwa na taa 54. Mfumo mzima wa taa
uliigharima klabu £ 40,000, na kutumika mara ya
kwanza katika mechi ya tarehe 25 Machi 1957.
Hata hivyo, taa mtindo zamani zilibomolewa
mwaka wa 1987, na kubadilishwa na taa za
kisasa zilizowekwa katika paa la kila jukwaa,
zinadumu hadi leo.
Mwaka 1990, kufuatia janga la Hillsborough
Disaster, ripoti ilitolewa iliyotaka viwanja vyote
kukarabatiwa ili kuruhusu mashabiki wanaoketi
pekee, hilo lilipelekea ukarabati ulioshusha idadi
ya mashabiki wanaoruhusiwa hadi takribani
44,000. Hata hivyo, umaarufu wa klabu
ulimaanisha kuwa maendeleo zaidi yangetokea.
Mwaka 1995, North Stand ilijengwa kuwa na
daraka tatu na kuongeza idadi inayoruhusiwa
hadi takribani 55,000. Hii ilifuatiwa na upanuzi
kwanza wa jukwaa la East na kisha West
kufikisha jumla ya idadi ya 68,000. Upanuzi wa
hivi karibuni zaidi ulikamilika mwaka 2006,
ambapo robo iliyopo North-East na North West
ilifunguliwa, na kufikisha rekodi ya idadi ya sasa
ya 76,098, 104 tu chini ya upeo wa idadi
inayoruhusiwa. [62]
Imekadiriwa kwamba kwa maendeleo zaidi
kufanyiwa uwanja, hasa Southern Stand ambayo
ndio hadi sasa ina daraka moja tu, gharama ya
uboreshaji inaweza kukaribia £ million 114
ambazo tayari zimetumika kuboresha uwanja
huo katika miaka kumi na minne iliyopita. Hii ni
kutokana na ukweli kwamba ingebidi takriban
nyumba hamsini kununuliwa na klabu, hilo
huenda likaongeza usumbufu kwa wakazi wa
mtaa huo,na upanuzi wowote ungelazimika
kujengwa juu ya laini ya reli inayopita karibu na
uwanja huo. Kwa kweli , upanuzi huo
utajumuisha kuifanya South Stand kuwa na
angalau daraka mbili na kujaza jukwaa za South-
West na South-East kuhifadhi umbo la "bakuli" la
uwanja huo. Makadirio ya sasa yanaashiria
kuwa uwanja huo ukijengwa hivyo utakuwa na
uwezo wa kuhimili takriban mashabiki 96,000,
zaidi wa uwanja mpya wa Wembley. [62]
Udhamini
AIG ndio wadhamini wakuu wa Manchester
United, na kama sehemu ya mpango huo wa
udhamini nembo yao imebandikwa mbele ya
mashati ya klabu na bidhaa nyingi nyinginezo za
klabu. Udhamini wa AIG ulitangazwa na afisa
mtendaji wa Manchester United David Gill tarehe
6 Aprili 2006, ina thamani ya £ milioni 56.5 rekodi
ya aina yake nchini Uingereza na ya kulipwa kwa
takribani miaka minne (£ milioni 14.1 kila
mwaka). [63] Udhamini huo ulikuwa wenye
thamani zaidi dunia mwezi Septemba 2006
baada ya kubatilishwa kwa udhamini wa £
milioni 15 kila mwaka kati ya Juventus na
kampuni ya mafuta ya Tamoil .[64] Tarehe 21
Januari 2009, ilitangaza kuwa AIG haitafanya
upya udhamini wao wa klabu ifikapo mwisho wa
udhamini wa sasa Mei 2010. Hata hivyo, si wazi
ikiwa mkataba wa AIG kusimamia MU Finance
utaendelea. [65] Kampuni ya bima ya marekani
Aon ilitajwa kama mdhamini mkuu wa klabu
tarehe 3 Juni 2009, huku udhamini wao kwa
klabu ukianza kutekelezwa mwanzo wa msimu
wa 2010-11. [66] Masharti ya mpango huo
hawakufichuliwa, lakini imeripotiwa kuwa una
thamani ya takriban £ million 80 kwa takriban
miaka minne, ambayo itaifanya kuwa mdhamini
mkuu zaidi katika historia ya kandanda.[67]
Klabu kimekuwa na wadhamini wakuu watatu tu
wa shati. Wa kwanza na waliohudumu kwa muda
mrefu zaidi walikuwa Sharp Electronics, ambao
walifadhili klabu kuanzia 1982 hadi 2000, ilikuwa
moja ya udhamini wa faida kubwa na wa muda
mrefu katika Soka ya Uingereza.[68][69] Nembo
ya Sharp ilikuwa mbele ya shati za United katika
miaka hiyo 17, wakati ambao timu ilishinda
mataji saba ya Ligi Kuu, tano za Kombe la FA ,
moja la Football League, moja la Washindi wa
makombe ya Ulaya na moja la Kombe la Ulaya.
Vodafone ilichukua udhamini kwa mkataba wa
awali wa miaka minne wa £ million 30 tarehe 11
Februari 2000, udhamini ulianza mwanzo wa
msimu wa 2000-01. [68][69] Mnamo Desemba
2003, udhamini ulirefushwa kwa miaka minne na
Vodafone ikakubaliana kulipa £ million 36 zaidi
kwa miaka minne ya 2004-2008. [70] Hata hivyo,
tarehe 23 Novemba 2005, Vodafone ilitangaza
kuwa itakomesha udhamini wake Mei 2006 ili
kuangazia zaidi udhamini wao wa UEFA
Champions League. [71]
Vivyo hivyo, klabu imekuwa na washonaji huru
nne tu wa sare yake, wa kwanza walikuwa
kampuni ya Uingereza UMBRO. Admiral ilichukua
usukani mwaka 1975, na kuwa kampuni ya
kwanza ya kuweka nembo yao kwenye shati la
Manchester United mwaka wa 1976.[72] Adidas
ilifuatiwa mwaka 1980, [73] kabla Umbro
kuanzaa kipindi chao cha pili kama
watengenezaji wa sare za klabu hiyo mwaka wa
1992. [74] Udhamini wa Umbro ulidumu kwa
miaka kumi zaidi kabla ya klabu kupata udhamini
wa kuvunja rekodi - £ million 302.9 kutoka kwa
Nike. Makubaliano na Nike yatadumu kwa miaka
13 ya awali, na kuendelea hadi angalau mwaka
wa 2015. [75]
Washindani
Kihistoria, washindani wa karibu wa Manchester
United wamekuwa Liverpool , Manchester City na
Leeds United.[76][77] Hivi sasa, mashabiki
wengi huona Liverpool kama washindani wao
wakubwa kutokana na mafanikio ya klabu zote
mbili, [78] ingawa bado wengine huiorodhesha
Manchester City kama wapinzani wao wakuu.
Ushindani na Liverpool ulianza katika miaka ya
1960 wakati klabu hizo mbili zilikuwa kati ya
klabu imara zaidi Uingereza, na zimekuwa
zikishindana kwa karibu sana kila msimu tangu
zamani. Ushindani wa Manchester City ulianza
wakati wa enzi ya Newton Heath ya miaka ya
1890 na imebakia kali kutokana na klabu hizi
mbili kuwa katika divisheni sawa kwa muda
mrefu wa historia yao. Huku ushindani ukiwa na
msingi wa ukinzani wa jadi kati yaYorkshire-
Lancashire , ushindani kati yao na Leeds United
ulianza mwishoni mwa miaka ya 1960 wakati
Leeds ilitawazwa mshindi, na kuendelea katika
miaka ya 1970 na 1980 kabla kufikia kilele
wakati Leeds ilipoiadhibu United katika taji la ligi
1992.
Tuzo
Nchini Uingereza
Ligi
Ligi Kuu:[79] 11
1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97,
1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03,
2006-07, 2007-08, 2008-09
Divisheni ya kwanza: [79] 7
1907-08, 1910-11, 1951-52, 1955-56,
1956-57, 1964-65, 1966-67
Divisheni ya pili: [79] 2
1935-36, 1974-75
Vikombe
Kombe la FA: 11
1909, 1948, 1963, 1977, 1983, 1985, 1990,
1994, 1996, 1999, 2004
Kombe ya Ligi: 3
1992, 2006, 2009
FA Charity / Community Shield: 17 (washindi
waziwazi mara 13, mara 4 imegawanywa)
1908, 1911, 1952, 1956, 1957, 1965 *, 1967
*, 1977 *, 1983, 1990 *, 1993, 1994, 1996,
1997, 2003, 2007, 2008 (* washindi wa
pamoja)
Ya Ulaya
Kombe la Ulaya / UEFA Champions League: 3
1968, 1999, 2008
UEFA Cup Winners' Cup: 1
1991
UEFA Super Cup: 1
1991
Duniani
Kombe la Mabara: 1
1999
Kombe la FIFA la Klabu za Dunia: 1
2008
Ushindi wa mataji mawili au matatu
Mataji mawili:
Ligi na Kombe la FA: 3
1994, 1996, 1999 (kama sehemu ya
Utatu)
Ligi na Kombe ya Ligi: 1
2009
Mataji mawili ya Ulaya (Ligi na Kombe la
Ulaya):2
1999 (kama sehemu ya ya Utatu), 2008
"Utatu" (League, Kombe la FA na Kombe la
Ulaya): 1
1999
Hasa mashindano mafupi kama vile Charity /
Community Shield, Kombe la mabara, Kombe la
FIFA la klabu za Dunia au Super Cup hazifikiriwi
kwa jumla kuchangia Ushindi mara mbili au tatu.
Taji kuu la peke ambalo Manchester United
haijashinda kamwe ni Kombe la UEFA, [80]
ingawa walifika robo-fainali mwaka 1984-85 na
nusu fainali ya mashindano tangulizi ya
michuano hiyo Inter-Cities Fairs Cup, mwaka wa
1964-65. [81][82]
sijamaliza kusoma:oops::oops:
 
Unaandika habari haina hata paragraph sasa nitasomaje namna hii?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom