Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Manara ambaye alikuwa anaiwakilisha Simba katika zoezi hilo, alisimama kwenda kumwakilisha klabu ya Yanga baada ya mabingwa hao kukosa mwakilishi.
Models waliovalia jezi za Yanga zitakazotumiwa msimu ujao walipanda kwenye stage lakini alipoitwa mwakilishi kutoka Yanga hakuwepo ndipo Manara akaenda jukwaani kuwawakilisha Yanga kutoka katika mitaa ya Jangwani.
Kwa upande wake Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika "Kila siku nawaambia hakuna uadui wala uhasama baina yetu, leo ni mimi mnayenitukana daily nilowanusuru kukosa vifaa, kwa kutoleta mwakilishi Vodacom, nileteeni jeuri mcheze vidari wazi msimu huu", ameandika Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Haji Manara.