Manara aiwakilisha Yanga kupokea vifaa vya michezo kutoka kwa wadhamini wa ligi Vodacom

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,408
2,000
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba SC Haji Manara leo Agosti 3, 2017 aliibuka na kwenda kuwa mwakilishi wa watani wao wa Jadi Yanga wakati Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wa ligi kuu Tanzania bara walipokuwa wakigawa vifaa vya kwa timu zitakazo shiriki VPL 2017-2018.

Manara ambaye alikuwa anaiwakilisha Simba katika zoezi hilo, alisimama kwenda kumwakilisha klabu ya Yanga baada ya mabingwa hao kukosa mwakilishi.

Models waliovalia jezi za Yanga zitakazotumiwa msimu ujao walipanda kwenye stage lakini alipoitwa mwakilishi kutoka Yanga hakuwepo ndipo Manara akaenda jukwaani kuwawakilisha Yanga kutoka katika mitaa ya Jangwani.

Kwa upande wake Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika "Kila siku nawaambia hakuna uadui wala uhasama baina yetu, leo ni mimi mnayenitukana daily nilowanusuru kukosa vifaa, kwa kutoleta mwakilishi Vodacom, nileteeni jeuri mcheze vidari wazi msimu huu", ameandika Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Haji Manara.
 

Mkidi Mwako

Senior Member
Jul 16, 2016
199
500
Soka la tz hata silielewi, inakuwaje siku kama hiyo timu inakosa mwakilishi?
Mkuu, sio soka tu hata mambo yetu mengine asilimia 75 yanaenda kienyeji sana, kipo kitu si bure. Timu inakosaje mwakilishi kwenye hafla kama hiyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom