Mananasi(PINAPPLE) Nianzie wapi?

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
205
Wafanya biashara kutoka nje ya Tanzania wanataka kujua kama wanaweza kupata mananasi kutoka Tanzania. Mwenye kujua ni wapi yanapatikana kwa kiwango kizuri (quality & quantity) anijuze na kama kuna wafanya biashara ambao tiyari wanafanya shughuli hiyo ya kupeleka manasi nje niwasiliane nao.
 
in Tanzania upatikanaji wa mananasi ni kwa season ... kwani kilimo chake si cha kisasa (siyo cha umwagiliaji).... hivyo basi msimu ukiisha mzigo unakwisha .... siyo biashara endelevu katika mwaka
 
Wafanya biashara kutoka nje ya Tanzania wanataka kujua kama wanaweza kupata mananasi kutoka Tanzania. Mwenye kujua ni wapi yanapatikana kwa kiwango kizuri (quality & quantity) anijuze na kama kuna wafanya biashara ambao tiyari wanafanya shughuli hiyo ya kupeleka manasi nje niwasiliane nao.

Kwa hapa Tanzania kilimo cha mananasi ( na matunda kwa ujumla) sio cha kibiashara, hivyo kupata supply ya mananasi bora kwa ajili ya soko la nje inaweza kuwa ngumu kidogo.
Mananasi yanatoka kwa msimu tu kwa sababu hayalimwi kwa kilimo cha umwagiliaji. Pia mananasi mengi yanayozalishwa hayana ubora kwa ajili ya soko la nje.
Wanunuzi hao wa nje wanachoweza kufanya ni kuingia mikataba na wakulima wa Tanzania ili wakulima hao wawe na uhakika wa soko, ili waweze kulima mananasi kibiashara kwa kilimo kikubwa cha umwagiliaji.
Pia wanunuzi hao wanaweza ku-finance wakulima wa Tanzania kwa makubaliano ya kununua mavuno ya mananasi kwa bei watakayokubaliana nao.
Wakulima wengi hapa Tanzania (hasa wakulima wa matunda) huwa wanatakishwa tamaa na soko la matunda yao. Hivyo kilimo cha matunda huwa sio kikubwa na sio kilimo endelevu kwa sababu ya ukosefu wa uhakika wa soko.
Hao wanunuzi wa nje wakifanikiwa kuhakikisha uwepo wa soko la uhakika, watapata mananasi mengi na yenye ubora.
Jaribu kuwaelezea hali hii uone kama watahamasika.
 
Kwa kuongezea katika post yangu hapo juu, kama wanunuzi hao wa nje watahamasika kuhusu makubaliano / mikataba kati yao na wakulima wa Tanzania, sisi wakulima tupo tayari kwa mchakato huo.
Uhakika wa soko ndio nguzo kuu katika kuendeleza kilimo kikubwa cha kibiashara.
Ukishapata response yao, utupe feedback ili tujue.
 
Wafanya biashara kutoka nje ya Tanzania wanataka kujua kama wanaweza kupata mananasi kutoka Tanzania. Mwenye kujua ni wapi yanapatikana kwa kiwango kizuri (quality & quantity) anijuze na kama kuna wafanya biashara ambao tiyari wanafanya shughuli hiyo ya kupeleka manasi nje niwasiliane nao.

Sisi tuko kikundi cha watu 12 tunalima mananasi huko Rufiji, tuna jumla ya ekari 100 za ardhi, na tumeshapanda ekari kama 50 kwa sasa tumeanza kuvuna kwenye ekari 20 za mwanzo na tuna uwezo wa kusupply nanasi kati ya 1000-2000 kila wiki kuanzia sasa hadi march 2013 ambapo ni mwisho wa msimu. kama unataka mazungumzo zaidi ya biashara ni PM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom