Management of the New Tanzania National Stadium

Jul 14, 2008
1,820
1,031
Wakulu;

Leo kuna Tender imetoka katika Gazeti la Daily News kwa ajili ya Management ya Uwanja Wetu Mpya wa Taifa (Naambatanisha Tangazo katika PDF Format). Kwa waliofuatilia miezi michache iliyopita kulikuwa na Invitation inayofanana na hii. Kwa hiyo ina maana Invitation inarudiwa.

Baada ya kufuatilia kwa nini inarudiwa inaonekana hakukuwa na serious response kutoka kwa Bidders wazuri. Aidha walioomba walikuwa wachache kuruhusu mchakato wa kupata kampuni bora kuendelea.

Wito wangu:

Uwanja wetu mpya wa Taifa ni mmoja kati ya vivutio vikubwa vya Mechi za Kimataifa, pia ni moja kati ya vitu vichache ambavyo Watanzania tunaweza kujivunia.

Ili kuhakikisha kuwa tunapata Managers Wazuri wa Uwanjaa huu, natoa wito kuwa kila ambaye ana contact za Kampuni Nzuri, awajulishe ili wajitokeze katika kushiriki kwenye Tender hii. Vinginevyo . . . . yanaweza kuwa yale yale . . . Binafsi niko tayari kusaidia nikihitajika.
 
Attachments

  • ITB Tanzania National Stadium.pdf
    402.8 KB · Views: 89

....

Ni kweli Mtsimbe tunahitaji kuutunza sana ule uwanja....Ni kivutio cha aina yake to be honest...
 
....

Ni kweli Mtsimbe tunahitaji kuutunza sana ule uwanja....Ni kivutio cha aina yake to be honest...

Mkuu Kipanga;

Kama utakumbuka, kulikuwa na Match ya Tanzania na Msumbiji miezi michache iliyopita. Uharibifu uliofanyika ni wa kutia aibu sana hasa ukizingatia kuwa Uwanja ulikuwa ni mpya na haujakabidhiwa rasmi kwa Serikali. Sijui hata tuna matatizo gani wakati mwingine.

Nadhani tukipata Manager mzuri atasaidia kwanza kuweka mfumo mzuri wa Ulinzi na pia kuboresha mapato n.k.
 
Kule sehemu ya michezo(sio mbali ni hapa hapa JF) kuna bandiko zuri kama hili la uwanja mpya wa taifa hapo jijini Dar...
 
Ukilisoma hilo tangazo la tenda liko fishy kidogo kwa sababu linaelezea kuwa bids ziwe zimetumwa au zimefikishwa by saa nne asubuhi tarehe 29-sept, na kuwa zitafunguliwa public in the presence of bidders or their representative, tangazo halioneshi bids zitafunguliwa tarehe ngapi na wapi, bidders watajua vipi lini bids na wapi zinafunguliwa au ndio hapa wamasiliano ya siri yataanza kwa ambao wameishachaguana. kama wanaweka kila kitu hadharani hakukuwa na sababu ya kutoweka tarehe na mahali pa kufungua bids. Watu wanapenda kupanga ahead of time sio kushtuliwa kuwa leo au kesho tunafungua bids haya njoo sasa.
 
Interested Observer,

Oh yes, and a yahoo email account these people are really amateurs at play, surely, any serious business will never use a yahoo or hotmail email account! thanks, I had not noticed that!!

au ndio ka mchezo ka Richmond kanaanza tena?!...
 
Mkuu Kipanga;

Kama utakumbuka, kulikuwa na Match ya Tanzania na Msumbiji miezi michache iliyopita. Uharibifu uliofanyika ni wa kutia aibu sana hasa ukizingatia kuwa Uwanja ulikuwa ni mpya na haujakabidhiwa rasmi kwa Serikali. Sijui hata tuna matatizo gani wakati mwingine.

Nadhani tukipata Manager mzuri atasaidia kwanza kuweka mfumo mzuri wa Ulinzi na pia kuboresha mapato n.k.

Inasemekana ule uharibifu ulifanywa na wachina wenyewe kwa sababu walikuwa wanataka kuongezewa muda kuumalizia uwanja.Walitaka kuweka hasara iliyopatikana kutokana na uharibifu huo juu sana,kwa sababu pia kulikuwa na fununu kuwa walikuwa wanaishiwa na funds.
Siku ya mechi na Cameroon,nilishuhudia kwa macho yangu watu kama wanne wakipigwa na washabiki wengine kwa kusimama kwenye viti.Maneno yao yalikuwa msituharibie uwanja kwa hao waliosimama kwenye viti.
 
Ni kosa kuanza kutumia uwanja kabla haujakabidhiwa rasmi! ndiyo maana waingereza walisubiri mpaka mkandarasi alipokabidhi Wembley ndiyo wakaanza kuutumia. kabla ya siku ya kukabidhiwa uwanja ulibidi kukaguliwa na consultant anayemwakilisha mshitiri kuhakikisha kuwa umejengwa kulingana na mkataba. Mshitiri anakubali kuupokea pale tu anapohakikishiwa kuwa hitilafu zilizopo ni ndogo na zinaweza kurekebishwa wakati wa muda wa defect liability. Na wakati huu wa defect liability, uwanja unaangaliwa tena ili kuona kama kuna matatizo yatajitokeza wakati wa utumiaji. Haya matatizo nayo yanatakiwa yarekebishwe na mkandarasi katika muda huo kabla ya hesabu za mradi kufungwa na mkandarasi kulipwa malipo yake ya mwisho. Hitilafu ambazo zitaonekana ni kutokana na matumizi mabaya ya mshitiri si jukumu la mkandarasi kusahihisha. Kwa kuomba kutumia kabla ya kukabidhiwa tumemfungulia mkandarasi mlango mkubwa wa kuweza kuepuka majukumu yake.

Hili suala la meneja linabidi liangaliwe kwa makini. Tukumbuke ya Net Group!
 
tangazo halioneshi bids zitafunguliwa tarehe ngapi na wapi, bidders watajua vipi lini bids na wapi zinafunguliwa au ndio hapa wamasiliano ya siri yataanza kwa ambao wameishachaguana.

Mzalendo GM, inawezekana mpangilio wa lugha haueleweki vema. Nadhani walichoandika "Bids will be opened thereafter promptly in public" inaweza ikawa ina maanisha ni siku hiyo hiyo mara tu baada ya submission saa 4 asubuhi siku hiyo ya tarehe 29-09-2008. Kwa mazoea Tenders nyingi hapa TZ huwa zinafunguliwa siku hiyo hiyo mara tu baada ya submission.
 
tUKIUENDEA PUPA ULE UWANJA TUTAUHARIBU....KAMA KAZI ZIPEWE KAMPUNI ZENYE UWEZO NA PIA WAPELEKE WATU WAO TRAINING KABISA HATA S.A AU HATA EGYPT TU WAKAPATE EXPOSURE...WASIUFANYIE DEAL LA KISIASA .....LETS WAIT AND SEE...
 
GM, yote uliyosema yanajieleza kwenye item 7 ya hilo tangazo.
 
Back
Top Bottom