Management chuo kikuu cha Ardhi watinga ofisi za BAVICHA

Mdutch

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
214
77
Kulikuwa na habari hapa kuwa CHADEMA imemwaga kitita cha milioni 9 kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Ardhi jambo ambalo limesemwa lilikuwa ni "umbea", sasa hivi uongozi wa Chuo cha Ardhi ukiongozwa na Dean of Students umetinga Makao Makuu ya BAVICHA kumfuatilia mmoja wa wagombea wa urais Ardhi wakidai wanataka kuverify kama huyo mgombea si kiongozi wa BAVICHA kule Ilemela Mwanza.

Kwa wale tuliopita vyuo vikuu tunajua kuwa hata kama mtu angekuwa kiongozi wa Magamba, utawala wa chuo ungehakikisha mtu huyo anakuwa rais kwenye serikali ya wanafunzi.

Taarifa kutoka ardhi zinadokeza kuwa jamaa huyo ni tishio na anatarajiwa kushinda uchaguzi huo jambo ambalo utawala wa chuo hautaki.

Hii ni aibu kwa utawala wa chuo kufanya mambo ya kitoto kama haya.
 
Kwani ni jinai kiongozi wa siasa kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi ikiwa naye ni mwanafunzi wa chuo husika!!?

Watu badala wafuatilie mitaala wanafuatilia upuuzi toka Mz hadi Dar!! Pathetic!!
 
Nchii ya wagagagigioko makubwa siwezi amini kama tuko century ya 21
 
siasa vyuoni matokeo yake ni taifa la wavivu
Unajua maana ya siasa wewe? Hivi kuna mahali ambako hakuna siasa? Hujui kuwa siasa ni uhai, ndiyo maisha na ndiyo moja ya misingi ya maendeleo? Au wewe siasa ni huko kwa Magamba wenzio ambako matokeo yake ni ufisadi? Kwanza una elimu gani wewe? Isije kuwa nahangaika na F4 wa 2012 ambaye badala ya ku-resit mtihani NECTA imeamua ku-resit yenyewe kurudia kutoa matokeo mapya! Shwaini!
 
Baadae wakae wawaze jinsi ya kuwajengea wanafunzi hostel za kukaa wanatumika kwa mambo ambayo si ya msingi.
 
...wamvalishe gwanda huyo dean,naye arudi akatangaze chadema...
 
Back
Top Bottom