Manabii wa sasa V/S Manabii wa zamani

Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
1,227
2,197
Unabii ni moja ya huduma 5 za Mungu za kuliongoza kanisa, iliyo muhimu sana kulingana na Biblia. Ukisoma vizuri maandiko utaona kuna tofauti kubwa iliyopo kati ya manabii wa sasa na wale wa zamani. Hizi baadhi ya tofauti:-

1. Nabii wa zamani mara nyingi walitabiri kuhusu mambo makubwa yatakayoikumba nchi au ufalme fulani na yalitokea km walivyotabiri.Manabii wa leo wanatabiri sana mambo ya mtu mmoja mmoja km kujenga nyumba,kuzaa watoto, kuolewa, kununua gari au kupanda cheo kazini.

Wakijaribu kutabiri mambo makubwa ya nchi huwa inaenda kinyume kabisa.Yaaani wananoa.
Mfano gonjwa la Covid-19. Manabii wengi tunaowafahamu walichemka. Hata kifo cha Mh. Rais hawakuoteshwa chochote! Km kweli ni manabii wa kweli sijui Mungu atakuja kuwapa unabii gani watuambie km haya yote yamepita kapa.

2. Manabii wa zamani muda mwingi walijitenga na jamii na kwenda kuishi nyikani huku wakifunga na kuomba.Manabii wa sasa wanatumia mda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii kujitangaza na kuuza bidhaa wanazoziita za upako km maji,Sticker,vitambaa,chumvi na mafuta na kukusanya sadaka kupitia M- PESA na Acc.za benki.

3. Manabii wa Zamani hawakuhusudu mali na utajiri wa dunia km biblia inavyosema katika 1Yoh2:15-17.Manabii wa sasa wanajivunia utajiri na mali km fedha, majumba, magari, ndege n.k.

4. Manabii wa zamani walikuwa hawajivuni i nguvu ya upako waliyobarikiwa na Mungu. Waliendelea kunyenyekea hata walipoinuliwa sana. Manabii wa sasa wengi ni wenye kujiinua,wanapenda kusifiwa.Mahubiri yamejaa vitisho ili watu wajione ni wenye mikosi na laana nyingi. Lengo ni kupigia debe maji na mafuta yao ya upako.

5.Manabii wa zamani hawakutabiri ovyo ovyo.Walitabiri baada ya vipindi fulani fulani. Hawa wa leo wanatabiri kila wakati tena kwa mbwembwe na makelele ya kujisifu.Tena wanajipa majina ya kuvutia( Brand names) km Bulldozer,Major One,The Anointed One,Mzee wa Upako,Chief, General n.k.

6.Manabii wa zamani walipewa"Specific" Mission ( ujumbe) fulani na Mungu ili kuufikisha kwa watu. Hawa wa leo wengi wao hawana "Mission"inayoeleweka. Utabiri wao ( Prophecy) ni wa aina ile ile. Ndoa,kazi, nyumba kupata watoto au kutoa mapepo n.k.

Tujiulize kwanini miaka ya nyuma 2000 kurudi nyuma, hakukuwa na hawa manabii uchwala na bado maisha yalikuwa rahisi kuliko leo?

Jibu ni ni rahisi."All these are due to high level of unemployment and religion has become one of the easiest way to make money".
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom