Man Water: Ali Kiba hajanilipa, kaenda kurudia nyimbo tulizofanya kwingine

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
1577963159837.png

Man Water ni miongoni mwa ma producer hodari aliewatoa wasanii wengi kama kina 20% ila baada ya kutoelewana 20% akapotea.

Katika mahojiano na Azam TV, amesema kuwa kuna nyimbo kadhaa alizofanya na msanii Ali Kiba lakini hawajazirelease kwa sababu hazijalipiwa.

Anasema kuwa licha ya kwamba alishiriki kupiga promo kuwa kazi nyingi zinakuja lakini walitoa “Seduce Me” na “Mvumo wa Radi” pekee kwa sababu ndizo zilizolipiwa.

“Pamoja na mimi kusubiri malipo ya hizi nyimbo ili nipate maslahi, nazisikia zikiwa zimerudiwa kwingine huko na zimeshatoka hivyo mimi ni kama nimebaki na makapi ilhali ndio nilikuwa source” anazidi kulalamika Man Water

Hadi sasa Man Water amesema hana hamu ya kufanya kazi na Kiba.

My Take:

Kiburi cha Alikiba hadi kwa producer ni aibu tupu, kayumba sana kumkera uyu jamaa ambae ni fundi anaejua.

Kwa sasa Ali Kiba ameamua kuwa na studio yake ya Kings music ila naweza kusema kwamba ni ya kawaida sana.

Man Walter ye kwanini aliamua kuachia kazi ambazo hajalipwa? Maelewano yao yalikuaje? Hizi case ni kawaida sana kwenye mziki rejea bob junior alivolalamika kwa diamond.
Unasema king music ni studio ya kawaida, hivi ishaanza kufanya kazi? Producer wake ni nan? Na ukawaida wa studio unaangalia vitu gani?

NB: Mocco genius sio producer wa king music

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hapa bongo hili neno Producer lina maana gani?

Mana kwa ufahamu wangu mimi ilitakiwa msanii ndie alalamike kuwa hajalipwa na Producer na sio producer alalamike yeye hajalipwa na msanii.
 
Kwa ninavyofahamu, studio ya kings music bado ipo kwenye matengenezo na haijaanza rasmi kufanya kazi, na pia utaratibu wao ni kuwa watakuwa na in house producer kwa ajili ya kurekodi demo na wakihitaji kufanya kazi na producer mkubwa atakuja na kuifanyia kazi hapo studio kwao.
 
Mtu ambaye anampatia kiba kwa midundo mikali ni man water ngoma zote alizotoa kiba hiv karibuni ambayo hajafanya na man water hazijafanya vizuri.Manwater pia nifundisho kwake kwa kuingilia bifu isiyomuhusu Kati ya kiba na mondi sasa hiv anakula matapishi yake mwenzake s2kizzy anakula tu maisha uko.
 
Huyu jamaa nilimuona anafail baada ya kuingilia ugomvi wa kiba na mondi over yeye ni meneja wa kiba. kuna siku alienda clouds na kiba akawa anamkandia mond.
Nikawaza yeye kama producer inabidi asiwe na upande kama anataka tengeneza mkwanja
 
Hivi hapa bongo hili neno Producer lina maana gani?

Mana kwa ufahamu wangu mimi ilitakiwa msanii ndie alalamike kuwa hajalipwa na Producer na sio producer alalamike yeye hajalipwa na msanii.
Producer anamlipa msanii? ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako.
Msanii inabidi alipie studio session na bado producer abaki na royalities za ile kazi aliyotengeneza
 
Producer anamlipa msanii? ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako.
Msanii inabidi alipie studio session na bado producer abaki na royalities za ile kazi aliyotengeneza

Mkuu Unamfahamu producer ni nani?

Producer ndie mmiliki na muuzaji mkuu wa kazi za sanaa. Huyo msanii hulipwa na producer.
 
Mkuu Unamfahamu producer ni nani?

Producer ndie mmiliki na muuzaji mkuu wa kazi za sanaa. Huyo msanii hulipwa na producer.
soma hapa
msanii inabidi alipie studio session ana bado amlipe producer na bado producer abaki na royalities.
 
Kwa ninavyofahamu, studio ya kings music bado ipo kwenye matengenezo na haijaanza rasmi kufanya kazi, na pia utaratibu wao ni kuwa watakuwa na in house producer kwa ajili ya kurekodi demo na wakihitaji kufanya kazi na producer mkubwa atakuja na kuifanyia kazi hapo studio kwao.
Ndio mana nimeshangaa huyu jamaa anasema king music ni studio ya kawaida wakati Mimi najua hata kazi haijaanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Producer anamlipa msanii? ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako.
Msanii inabidi alipie studio session na bado producer abaki na royalities za ile kazi aliyotengeneza

Kwa sababu haujui maana ya producer
 
Kwa sababu haujui maana ya producer
najua sana maana ya producer. Producer siyo lazima ndiye awae ametengeneza beat au kuhsuika na kuingiza vocals vyote vinaweza fanywa na watu wengine halafu producer awe mwingine.
turudi kwenye point ya msingi unaweza kuniletea reference yoyote ya kuwa producer ndiye anamlipa msanii?
Mimi nimeuwekea link jinsi msanii anavyomlipa producer
 
maker wa mdundo huyo
we unabishana kkwa maneno mimi nitakupa links tu
haya tazama hapa hii blog ya music contracts
hakuna sehemu nimewahi kuona producer anamlipa msanii
 
Back
Top Bottom