Man United Vs Brigthton

Ramosi255

Member
Aug 24, 2016
11
8
Nini kimewakuta Man U weekend hii??

Hakuna asieona kama leo Man u walikutana na Beki bora iliowasumbua sana mashetani hao wekundu kwenye uwanja wa Amex stadium.
Kuna mambo kadhaa yakuojili leo lakini lazima tuseme haya ya wazi kabisaa.

UWEZO WA KUZUIA WALIONAO BRIGTHON. (DEFENCE ABILITY)

Hawa jamaa leo mbali ya kiongozi wao mzuiaji Lewis kutoka kwa majelaha ila waliendelea kuipa tabu sana safu ya Man u kwenye ushanbuliaji.

Brighton walilazimisha mashumbulizi (high pressing). Man u walijikuta wakikubali kukabiwa kwao mara kadhaa na kufanya viungo wao watatu kushindwa kutanua uwanja na kupita kwemye winga zao. Wakati wote viungo wa Brighton . Knockaert, Propper, Stephens March na Gross walikiua kiungo cha Man u na kumfanya Murray kupata nasafi nyuma ya defenceline ya man u.

Pia winga wa Brighton walikuwa hodari sana leo kiasi cha mimi binafsi kusahau Martial na Matta wanafanya nini uwanjani. Hongera sana Brigthton leo.

Walitumia vema uzembe wa man u.
Jamaa walikuwa sharp sana man u walipotoa ruhusa ya aina yoyote ya uzembe walitimia nafasi hzo vema sana wakati wote. Goal la kwanzi ni uzembe wa Matta kito kumfuata au kufuatilia winga yule wa Brighton aliekuwa anamtengenezea Murray. Mara kadhaa tumeona Bailly pia akizawadia kona iliozjiliwa kizembe lia na man u kabla ya Fred kilazimisha kufanya makosa na kuwafanya hawa madogo leo nyota yao kuwa brigth kama jina lao.

MAKOSA YA MAN U.

Matta kashindwa kuwa winga au kiungo wa pembeni leo na mara kadhaa kawa anaingia kati na kumuacha Bong na wengine wakimpa shida Young huku mchango wa Matta kukaba ukiwa finyu.

Kukosekana kwa kiungo mzuiaji kama (Enchor) au holding midfilder kumewaghalimu sana Man u mtu kama Matic leo ndio wengi wanajua anaumuhimu. Matic hana manjonjo ila anauwezo wa ku shield mpira na ku jenga mashambulizi taratibu kutokea nyuma kitu ambacho leo hakikuwepo.

Kukosekana kujituma kwa Pogba na martial, ni kama walikuwa wanamkomoa mtu au abiria wanaojichanganya kwa watu wenye kujua safari. Yaan jamaa walikuwa flopy na wako wako bila commitment. Bailly pia toka kaanza vaa jezi ya mashetani leo kawa mwenye kupanic na matumizi ya nguvu bila akili na kwa nafasi anayocheza haikupaswa kuwa na tempo kiasi cha kupoteza tracking ya mpira.

Yangu ni haya ila hongera san brighton wamefanya la muhimu kwa kupata nafasi na kuzotimia vema.
Mbaka week ijayo tena....
IMG_20180819_223136_362.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom