Man Pac amdunda Keith Thurman kwa split decision

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,245
2,000
Bondia gwiji Man Pac amempiga tozi nyangema Keith Thurman katika pambano liloenda mpaka round ya 12.

Round ya kwanza Thurman alidondoshwa chini kwa ngumi za kushtukiza za Man PAC.
Kiufupi round ya kwanza mpaka ya sita Man Pac alikua very active na ile speed yake japo miaka imeenda, 40 years old sasa.
Round ya saba na kuendelea kama vile umri ukawa unamkwaza maana hata spidi ikapungua tena nimempa round ya 7 Thurman kwa kweli. Ila hizo round 6 za mwanzo yaani ni yule Man Pac wa miaka yote.
Round ya 8 mpaka ya 9 fifty fifty kwa kweli. Ila ya 10 Man Pac alimpa jamaa chembe moja ya moyo akawa hata kuhema hawezi sema Man Pac sijui kwa nini hajammaliza pale.
Round ya 12 Thurman sijui Athuman akajifanya anataka amkalishe Man Pac kwa fujo fujo maana ameshaona mambo siyo, baasi ilibaki kidogo tu yeye ndiye angekalishwa.
Mwisho wa mchezo the legend mwenyewe Man Pac akachukua ushindi kwa split decision.
 

dokolombwike

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
373
1,000
Mkuu nimeshangaa kwanini pacman hakumaliza mchezo wakati tozi alishainama kwa maumivu,ila tozi nae mmbaya akikutana na hawa mabondia wa kawaida
 

PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
10,335
2,000
Kwa mchezo ule huyo Pachiao wenu asikutane na Mwakinyo wetu
 

yitzhak

JF-Expert Member
Jul 3, 2019
620
1,000
IMG_20190721_105554.JPG

Sisi sio waongeaji ni vitasa tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom