Man Fongo: Singeli tunachukua soko la muziki sasa, wasanii wa bongo fleva watafute kazi nyingine

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
xMAN-FONGO.jpg.pagespeed.ic.gCTOyjY8Qy.jpg


Msanii wa muziki wa kisingeli, Amani Khamisi ‘Man Fongo’ amewataka wasanii wa muziki wa bongofleva kupokea ushindani mpya kutoka katika muziki wa kisingeli.
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Hainaga Ushemeji’ amesema muziki wa kisingeli una nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwa kuwa ni muziki wa uswahilini.

“Muziki tunaouimba ni wa mtaani ambapo ndiko chimbuko na watu wa uswahilini, kwa sasa huwaambii kitu kuhusu muziki wetu. Nawaambia ukweli kabisa wasanii wa Bongo Fleva, wakaze buti twende sawa au watafute kitu kingine cha kufanya,” Man Fongo aliliambia gazeti la Mtanzania.

“Ujue wao wanaimba vitu vya kubuni wakati sisi tunaimba maisha halisi hasa ya uswahilini kwa masikini wenzetu,”

Awali watu waliuita muziki wa kihuni kutokana na vijana kufanya matukio mbalimbali ulipokuwa unapigwa kwenye shughuli za mitaani nyakati za usiku maarufu vigodoro.

Pia muimbaji huyo kwa mara ya kwanza amepata shavu la kupanda kwenye jukwaa la Fiesta Mwanza.
 
Hatajuli ushemeji tunakulaga....kiatu kama hiki hauna huwezi nunua...teh teh kisingeli bhana.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Hizo kelele zichukue nafasi ya bongo fleva,maskini akipata bwana

Kumbe na wewe umegundua kuwa huo 'muziki' ni makelele eh?

Nilidhani labda ni mimi tu!

Sidhani kabisa kama [huo muziki] utadumu kwenye medani za burudani.

Muda si mrefu watu watauchoka tu.
 
Juzi huko Usukumani Mwanza walikuwa wanamshangaa tu...Labda ukiki huko Dar kwenu,Morogoro,Tanga,Lindi na Mtwara....Ila Chugga,Mwanza na Sehemu zingine Asahau
 
Juzi huko Usukumani Mwanza walikuwa wanamshangaa tu...Labda ukiki huko Dar kwenu,Morogoro,Tanga,Lindi na Mtwara....Ila Chugga,Mwanza na Sehemu zingine Asahau
Hapa umeongea. Huo mziki ni wa kieneo na umepata coverage sababu media zipo hapo.

Wasanii wa singeli wapo manzese hapo huko mbagala kwa mfuga mbwa na uswahilini dar tu ni ngumu kupata wajuzi wa huu mziki mikoani kutokana na style yake sasa kuipiku bongoflava ambayo mtu yeyote anaweza kuimba ni ngumu.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
bahati mbaya zaidi hawajajua kuwa wanatumiaka na mziki wao umepewa promo ili kuupa huu msimu wa fiesta watu wengi,sasa jiulize hapo nani anafaidika nao,na ambavyo hawana shule basi kipindi cha mpito kikipita watabaki tu kuvuta bangi zao.
ni mziki fulani non-sense.
 
Muziki una kelele ni maudhi tuuuu! Zipigwe huko mb:;$la mseme muziki mwingine umekwisha hahahahhhh mnachekesha
 
Back
Top Bottom