Mamuzi kama haya yanatuweka na hofu wahamiaji na majumba yetu ya ibada tuliojenga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamuzi kama haya yanatuweka na hofu wahamiaji na majumba yetu ya ibada tuliojenga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Black Jesus, May 7, 2009.

 1. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali yavunja wodi ya Raza Z'bar
  Tuesday, 05 May 2009 16:45
  Na Said Mwishehe
  HATUA ya kuvunjwa jengo la wodi ya wazazi ya Hospitali ya Kivunge iliyoko Mkoa wa Kaskazini 'A' Unguja imezua mtafaruku mkubwa huku baadhi ya wadau wakidai kuwa jambo hilo limefanywa kwa fitna .


  Akizungumza na Majira jana, mfadhili aliyejenga wodi hiyo, Bw. Mohamed Raza, alidai kitendo cha kuvunja wodi hiyo si cha kiungwana na kina lengo la kudhoofisha maendeleo ya Zanzibar.

  Alisema alijitolea kujenga wodi hiyo kutokana na matatizo makubwa yaliyowakabili wanawake wa Mkoa wa Kaskazini A ambayo yalichangia ongezeko kubwa la vifo vya watoto na wajawazito. Ujenzi huo ulianza Februari 19 , 2007 na kukamilika Julai 18, 2007 mwaka huo.

  Alisema kabla ya hapo, wajawazito hospitalini hapo walilazimika kuchangia kitanda kimoja watu wawili hadi watatu, hali iliyoleta mateso makubwa kwa wanawake hao.

  Tatizo hilo lilikera Kamati ya Maendeleo Visiwani humo inayoongozwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi na kuchukua hatua kadhaa kunusuru jambo hilo ambapo, Bw. Raza alijitolea kujenga wodi hiyo.

  "Wodi hiyo iliyokuwa na vitanda 10, chumba cha kujifungua na huduma zingine zote , ujenzi wake uligharimu jumla ya sh. milioni 20 ilisadia kwa kiasi kikubwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini 'A' alisema Bw. Raza.

  Alisema Mei mosi mwaka huu alipewa taarifa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, imevunja jengo lote la wodi hiyo.

  "Nilishtuka sukari na presha vikapanda kutokana na ujumbe nilioambiwa. Siku iliyofuata nilizuru hospitali hiyo na kuhakikisha jambo hilo. Nilikuta jengo nililojenga limebomolewa."

  Alisisitiza kuwa hatua hiyo si sahihi kwani imechangia kurudisha nyuma jitihada za kuboresha sekta ya afya visiwani humo.

  Alisema kama wizara iliona jengo hilo ni dogo hapakuwa na sababu kulibomoa kwani bado kuna maeneo ya kutosha hospitalini hapo, wangeweza kujenga sehemu nyingine bila kufanya uharibifu huo.

  Alidai hatua hiyo imefanywa kibabe na kamwe maamuzi ya namna hiyo hayajengi nchi bali yanarudisha nyuma maendeleo ya watu wa Zanzibar.

  Alisema kitendo hicho kamwe hakitamvunja moyo wa kujitolea kuchangia maendeleo na ataendelea kujitolea kwa hali na mali bila kujali jinsia rangi wala itikadi.

  " Maana ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwaletea watu maendeleo, leo tunakwenda kuvunja hospitali bila kuwepo sababu za msingi! Wanawaonea wananchi masikini wa mashambani, kwasababu wao hawategemea kupata huduma hapo" alidai Bw. Raza.

  Alisema aliamua kujitolea kujenga wodi hiyo kwa heshima ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt Salamin Amour anayetoka eneo hilo na pia njia ya kuonesha kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Kamati ya Maendeleo ya Zanzibar katika kueleta maendeleo.

  Majira lilipozungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Sultan Mugheiry kujua undani wa jambo hilo, alisema wanazo taarifa hizo na wanatarajia kutoa ufafanuzi kamili leo.
   
 2. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lazima kuwe na maelezo ya upande wa pili! Haiwezekani wakavunja tu! Pili labda wanampango mwingine wa papo kwa papo!

  Unataka kuniambia wanawezavunja maternity ward wakati hakuna eneo lingine inayoshughulikia maswala ya uzazi? Utakuwa wendawazimu huo!
   
Loading...